Kitabu cha Enock (Henoko)

Kitabu cha Enock (Henoko)

Nimesikitika sana hivi huwa inawezekanaje mtu kuzungumza utumbo wa hivi halafu hadharani kabisa..... Walokole mna nn nyie, mbona Kila siku kuzidi kuithibitishia Dunia kuwa mmejaza ujinga kichwani
Kwa Hiyo kila mtu anayechangia hapa ni Mlokole...!?
Who are you by the way kuchagulia Watu Vitu vya kuandika!?
 
Niliwaambia hii dunia imezungukwa na kioo kikubwa sana kinachoitwa firmament ambapo juu yake kuna maji mengi. Ukisoma kitabu cha Mwanzo, kinasema kipindi cha Nuhu milango ya mbinguni ikafunguliwa na maji kujaa duniani.
Mkuu hapa tunachanganyana watu wanaenda Sayari ya Mars na Mwezini hivi vyote viko mbali na uso wa dunia inamaana hapa jamaa wanapitaje kwenye hii firmament na hapo umesema wanasayansi hawajawahi kuivunja
 
Ukielewa agano la kale ukija kuelewa agano jipya unajikuta kama unachanganyikiwa hivi.
Maana agano la kale linakataza hilo agano jipya linakuja kueuhusu jambo hilo.
 
Haya mambo yanahitaji mtu aliyesoma na kuelewa Kwa undani yeye mwenyewe halafu mwisho atafakari, Kwa kusoma vistari viwili vitatu na masimulizi ya viongozi wetu wa dini ambao tunawajua akili zao halafu unajikuta nondo, lazima mambo yagongane na kitu kibaya zaidi huwa hatutaki kusoma. Tufuatilie haya mambo maana Yana athari kwenye maisha yetu ya Kila siku.
 
Ukienda Katika Uislamu Shetani wako pande Mbili Kuna Shetani wa Kijini Na shetani wa Kininadamu..

Tuje katika Asili yenyewe Neno Shetani limetokana na Neno la Kihebrania neno shetani (שָּׂטָן)..
Linamaanisha Adui (Adversary) au Mshitaki (accuser)..

Ntakupa Mafungu kadhaa Ambayo Neno shetani Limetajwa ila halikumaanisha Shetani kama Mtu/Jini au Malaika aliyeasi..

Hesabu 22:22

In Hebrew

וַיַּכְעַס אֱלֹהִים כִּי הוֹלֵךְ וַיַּעֲמֹד מַלְאַךְ יְהוָה בַּדֶּרֶךְ לְשָׂטָן וְהוּא רֹכֵב עַל-אֲתוֹנוֹ וְשְׁנֵי נְעָרָיו עִמָּדוֹ

inatamkwa..

Va'yik'chas Elohim ki holech, va'ya'amad malach Yahwe baderech le'shetan; ve'hu rochev al-atonoh, ve'shnei ne'arav immo."

Kwa Kiswahili

"Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye."
Twende Kitabu kingine

1 Samuel 29:4:
וַיִּקְרוּ אֱלֹהִים אֶל-עַבְדֵי אֲכִישׁ לֵאמֹר: שָׁבוּ אִישׁ אֶל-מְקֹמוֹ אֲשֶׁר-נָתַתָּ לוֹ וְאַל-יֵרֵד אִתָּנוּ לַמִּלְחָמָה, פֶּן-יִהְיֶה לָּנוּ לְשָׂטָן בַּמִּלְחָמָה; וּמַה-יָּבִיא אֶת-לֵב אֲכִישׁ אֲחִישׁ הַיָּדָוְ

Inatamkwa

"Va'yik'ru Elohim el-avadey Achish le'mor: Shavu ish el-mekomo asher-natata lo ve'al-ye'red itanu la'milchamah, pen-yih'yeh lanu
le'shetan ba'milchamah; u'mah-yavi lev Achish achish hayad."
kiswahili fungu Hilo..


"Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?"

SO kama Ulivyouliza nitajibu Kuwa Shetani Haikuwahi kumaanisha Status ya Mtu mmoja au utambulisho wa Mtu fulani Hapo zaman..

Mpaka Kwenye Medieval Period au Tunaita Medidval thought of satan kuanzia Karne ya 4 C.E ambayo iliamza Kumsingularised Shetani kuwa ni mtu mmoja wakati haikuwa Mtu bali ilikuwa Ni sifa ..
Nadhani nimejibu swali lako labda kama una swali la nyongeza
Na pale Yesu alipomwambia Petro
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Math 16:23 Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”

Alimaanisha nini hasa?

Kwa mujibu wa tafiti zako kuna kiumbe au viumbe ambao ni adui wa binadamu kiroho??
 
Na pale Yesu alipomwambia Petro
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Math 16:23 Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”

Alimaanisha nini hasa?

Kwa mujibu wa tafiti zako kuna kiumbe au viumbe ambao ni adui wa binadamu kiroho??
JIbu ni Lile lile Mkuu..( Japo Jibu litakuwa Refu ila ningependa Usome Nimejibu With Mindset ya Dini Kabisa)

Lets View It on the Perspective unayotaka..

Agano Jipya Most of It imeandikwa Katika Lugha ya Kigiriki au Wenyewe wanaita Kiyunani..

Math 16:23, Origina kabisa inaandikwa hivi

" Ὁ δὲ στραφεὶς εἶπεν τῷ Πέτρῳ· Ὕπαγε ὀπίσω μου, σατανᾶ· σκάνδαλον εἶ ἐμοῦ, ὅτι οὐ φρονεῖς τὰ τοῦ Θεοῦ, ἀλλὰ τὰ τῶν ἀνθρώπων."

Kimatamshi

"Ho de strapheis eipen tō Petrō, Hypage opisō mou, satanâ; skandalon ei emou, hoti ou phroneis ta tou Theou, alla ta tōn anthrōpōn."

Tafsiri ya Kiswahili Umeshaitoa bhasi na mimi nakupa Tafsiri Ya Kule kwa Kina Trump

"But he turned and said to Peter, 'Get behind me, Satan! You are a stumbling block to me, for you are not setting your mind on God’s interests, but man’s.'"


Kwakuwa Tafsiri (Translation) Umeshaitoa
Naomba Nitoe Tafsiri Fafanuzi (Interpretation)

Kama unajua Kigiriki hata kidogo tu kwanza Angalia Neno Lenyewe baada ya Satanâ Likafuata neno ambalo alimuita "skandalon" (σκάνδαλον), Linalomaanisha Kiswahili "kizuizi" au Kkikwazo au Kwa sahz Tungesema Wewe Ni kizibo ila kwa Lugha ya Obama wangesema "stumbling block" or "offense." Kwa lugha ya Kigiriki kuna neno Jingine hapo "ὀπίσω" (opisō) ambalo linamaanisha Nyuma...

Sasa kwa pamoja Ukiangalia Maneno hayo yote yalivyotumika Na mpangilip Wake ni kwamba Peter au petro au Kefa alikuwa Anazuia Ama angezuia Yesu kukamatwa na Alikuwa ameanza kushinda kwa kupandikiza imani hiyo ya kuzuia ukamatwaji wa Yesu kwa wanafunzi wengine..

Jambo hilo lilikuwa Limeanza kuwaingia wanafunzi na Wao wakaanza Kuondoa Uoga na walianza kama kujenga Ujasiri wa Kuzuia Kukamatwa kwa Kiongozi wao kama Ilivyokuwa kwa Osama kwa Alqaida (Natania) 😅😅

Yesu alipoona Hilo aliona Ile Devine stability ya Ukombozi imeanza Kufifia Kutokana na Petro Kuingiwa na Tamaa ya kuwa na Yeye Milele ndipo alipotumia Ujasiri Kuikemea Ile Mindset Bila ya Kuogopa na wala Hakukusudia Kuwa petro ndo huyo Shetani sasa (Tunavyoamini baadhi yetu) ila Mawazo yake yalikuwa Pingamizi au ya Kiadui kutokana na Ukombozi ambao Uliokuwa Mbele..

Kwahyo Petro ndo alikuwa Katikati kati ya Ukombozi Wa Yesu Kufanyika na Kutokufanyika..
Kwa bahati mbaya ama Nzuri Petro alitaka Kushinda roho ya Kumsaliti Au kumuachia Yesu aende (Kibinadamu Ilikuwa Roho nzuri ila Kwa Kiimani haikuwa Roho nzuri) kwa sababu ingezuia Ukomboni (Nasema kwa Njia za Kiimani zaidi)

Au hata Wewe Jiulize Vipi kama Yuda angekuwa Mwema na Akakataa Offer ya Vipande alivyopewa na watesi (Kibinadamu angefanya Vyema ila vipi kuhusu Ukombozi??)

Sasa Fungu hilo uliloleta Halina Tofauti na 1 Samwel 29:4 ,

Pale ambapo Balaam Alitaka Kuwalaani Wana wa Israel na Malaika akasimama kumuuliza kwanini anakuwa Shetani...

Nimeelezea hilo kwenye Post uliyoQuote..

Nafikiri Umenielewa
 
Kwa mujibu wa tafiti zako kuna kiumbe au viumbe ambao ni adui wa binadamu kiroho??
Kwa Kuwa tumehamia Kiroho jibu ni kweli kabisa kuna Viumbe Vingi sana Ambavyo ni Adui (Satan) wa Binadamu kiroho Viumbe hivyo vinaweza kuwa Ni Visivyoonekana Na Vinavyoonekana..

Vinavyoliwa na Visivyoliwa..
Kuna Viumbe au Vyakula Pia Usisahau tunavyokula Vinaweza kusababisha Vikwazo vyetu kiroho..
 
Mkuu hapa tunachanganyana watu wanaenda Sayari ya Mars na Mwezini hivi vyote viko mbali na uso wa dunia inamaana hapa jamaa wanapitaje kwenye hii firmament na hapo umesema wanasayansi hawajawahi kuivunja
Hakuna Mtu aliyewahi Kwenda Sayari ya Mars Mkuu..

Kama unaye Unaweza Kuprove hilo kwenye Jukwaa hapa na Ninakuahidi Kama Utaprove kuna Mtu kafika sayari ya Mars..

Basi Naweka Ahadi kwa Moderator Kuwa Nitakupa Kiasi cha Tsh 2Milion huku nikifuatiwa na Adhabu ya Kufungiwa kwa Miezi Zaidi ya 12
 
Hakuna Mtu aliyewahi Kwenda Sayari ya Mars Mkuu..

Kama unaye Unaweza Kuprove hilo kwenye Jukwaa hapa na Ninakuahidi Kama Utaprove kuna Mtu kafika sayari ya Mars..

Basi Naweka Ahadi kwa Moderator Kuwa Nitakupa Kiasi cha Tsh 2Milion huku nikifuatiwa na Adhabu ya Kufungiwa kwa Miezi Zaidi ya 12
Duh🥺🤔🙇🏿‍♂
 
TURUDI NYUMA KIDOGO

Ukiendelea kusoma kitabu cha Enoko unakuja kugundua kuhusu asili ya Adam na Nuhu.

Nadhani nayo inaweza kuwa sababu ya kitabu hiki kunyofolewa kwenye Biblia kwa sababu hawakutaka ulijue hili.

Kitabu hicho kimemzungumzia Adam kama mtu mweusi, hakuwa Mzungu kama tunavyoaminishwa sehemu mbalimbali.

Lakini ukiachana na hilo, pia Nuhu alikuwa albino. Nenda kasome Enoko 105.

Inasema kwamba kwa namna Nuhu alivyokuwa mweupe sana mpaka watu walikuwa wakimshangaa, hakuwa kama watu wengine duniani. Na hakuwa Mzungu bali albino.

Kama watu walikuwa wakimshangaa kutokana na yeye kuwa mweupe sana na nywele zake nyeupe inamaanisha dunia nzima watu walikuwa weusi kama baba yao Adam. Sijui kama unanipata hapa.

Nuhu alizaliwa na ngozi nyeupe, nywele nyeupe kiasi cha watu kumshangaa.

Nuhu hakuwa na muonekano kama wanadamu wengine.
Hii ilimpelekea mpaka Lameki kuhisi Nuhu alikuwa mtoto wa malaika kutokana na alivyokuwa.

Kumbuka miaka hiyo nao malaika walikuwa na watoto wao duniani walioitwa Wanefili. So watu walipokuwa wakimwangalia Nuhu walihisi alikuwa mmojawapo.

Sasa hapa kuna vitu hivi inabidi uvishike.

• Ngozi nyeupe haikuwa kawaida kwa binadamu kipindi hicho. So the whole world was black (Dunia nzima walikuwa weusi)
• Watoto wa malaika walioasi walikuwa weupe pee.

Sasa kwa nini watu waseme Nuhu alikuwa albino na si Mzungu? Kwa nini maelezo yake yaonyeshe kuwa ni albino?

Kama dunia nzima ilikuwa ni watu weusi na Nuhu, watoto wa malaika ndiyo waliokuwa weupe, je, unaona hii si sababu mojawapo iliyowafanya wazungu kukiondoa kitabu cha Enoko kwenye Biblia?

Wakimchora Adam, wanamchora mweupe, wakimchora Hawa wanamchora mweupe kumbe wanajua ukweli behind the scene.

IMG_0206.jpeg
 
Kwa mnaojua Kiingereza hebu someni hapa kwenye Kitabu cha Enoko 105;1-3. Nitajaribu na kuandika kwa Kiswahili tuelewe zaidi.

“After a time, my son Mathusala took a wife for his son Lamech. She became pregnant by him, and brought forth a child, the flesh of which was as white as snow, and red as a rose; the hair of whose head was white like wool, and long; and whose eyes were beautiful. When he opened them, he illuminated all the house, like the sun; the whole house abounded with light. And when he was taken from the hand of the midwife, opening also his mouth, he spoke to the Lord of righteousness. Then Lamech his father was afraid of him; and flying away came to his own father Mathusala, and said, I have begotten a son, unlike to other children. He is not human; but, resembling the offspring of the angels of heaven, is of a different nature from ours, being altogether unlike to us.” - Book of Enoch 105:1–3

Kwa Kiswahili…..

“Baada ya muda, mwanangu Mathusala alimwoa Lameki mwanawe. Akapata mimba kwa ajili yake, akazaa mtoto, ambaye nyama yake ilikuwa nyeupe kama theluji, na nyekundu kama waridi; nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu, na ndefu; na ambao macho yao yalikuwa mazuri. Alipozifungua, aliangaza nyumba yote, kama jua; nyumba nzima ilijaa mwanga. Naye alipotolewa mkononi mwa mkunga, akafumbua kinywa chake, akasema na Bwana wa haki. Ndipo Lameki baba yake akamwogopa; akaruka akamwendea babaye Mathusala, akasema, Nimezaa mwana, asiyefanana na watoto wengine. Yeye si mwanadamu; bali, anayefanana na watoto wa malaika wa mbinguni, ni wa namna tofauti na sisi, kwa kuwa tofauti kabisa na sisi.” - Kitabu cha Henoko 105:1–3
Umeelewa Hapo?

“Nimezaa mwana, asiyefanana na watoto wengine. Yeye si mwanadamu; bali, anayefanana na watoto wa malaika wa mbinguni, ni wa namna tofauti na sisi, kwa kuwa tofauti kabisa na sisi.”

Watoto wa malaika, watoto wa malaika....ndio wale wanefili ambao walizaliwa baada ya wanawake kufanya mapenzi na hao malaika.

Wanawake hao wakalaaniwa na kutupwa baharini na kuwa nguva, adhani nilielezea kuhusu hili.

IMG_0207.jpeg
 
Imani kitu Cha ajabu sana.
Kuna kipindi niliamua kuwa mtu wa Imani kweli kweli, nilikua nikiangalia sehemu kama Kuna kitu unadanganya au kinakuja kutokea nakwambia hapo hapo.

Mfano: nilimwambiaga jamaa yangu Moja pale morogoro miaka ya 2013/4 kwamba Kuna ajali inatokea angalia pale ilikua madawa pale stand. Kweli jamaa akawa anaangalia mi nika mwambia Tena nikiangalia Mimi mtu anaweza kuumia ila nisipo angalia itakua ajali ya kawaidatu. Jamaa akawa anaangalia hazikupita dakika tatu Kuna gari la manispaa likawa linavutwa Yale ma Isuzu ya kizamani tipper lilikua stealing haifanyi kazi likachomoka bomba likaamia upande wa pili like mfata jamaa alikua na boda boda mungu saidia likaingia kwenye msingi kama linaenda uelekeo wa masika ghafla boda nae akaingia kulifata huko huko. Hapo hakuumia mtu.

Dakika Tano nyingi nikamwambia jamaa Tena mi siangalii huko haikuchukua hata dakika tatu ikaja Noah nazani ilikua ya Moro tuliani jamaa anatoka kichangani kuingia bara bara kubwa kabla ya hiyo waliyo Jenga ya lami naye akaja mbele yetu akaingia kwenye mtalo mbele yetu jamaa akaniambia niondoke natoka siku hiyo ikawa na urafiki wetu umeisha.

Sempai mmoja alikua anafanya shughulizake pale sikuiz sijui Yuko wapi na hii ilianziaga kwenye meditation maana tulikua watu wa martial arts. Toka enzi za Makoto ..........


Nikahamia ngerengere Kuna Mzee pale anaitwa Msela. "A man with last life". Huyu jamaa mpaka leo bado anaweza kusikia hata tatizo kinakuja au laa. Alinifundisha tukaanza mi huwa mzuri kwenye maono kiasili. Aliniambia viashiria vya uadui,udui na namna ya kulock hatari Ili ujue inatokea wapi hii wanajifunza sana watu wa Special force na VIP protection. Japo Idara za ujasusi nao hujifumza. Uhisi, uhakiki na nauchukue maamuzi bila kukosea.

Kuna siku aliniambia kunawatu wanakuja kunitafuta akanipa sehemu nikakae na niwatambue hao watu ni akina nani ila kwa sharti Moja nisifumbue macho yaani nitumie six senses. Nilifeli kwa asilimia hamsini akaniambia Mimi ni mzuri ila nilitaka kuona nisione jinsia tofauti na yangu ikiwa haija jistiri. ( Nilikuja kuelewa baadae sana) Alicho maanisha yule Mzee.

Mimi hata unidanganye kama tupo hivi face to face najua hata nisipo kuwa nakuzingatia. Na inanipa shida sana kwenye mahusiano na huwa sikosei kwa Hilo. Niliachana na haya mambo ya jicho la sita baada ya kuiingia kwenye mtego wa dhiki.

Mungu mwema chembe ya haladai inatosha kuugeuza mlima. Mimi naamini hiyo na hiyo haijalishi unaamini kupitia nyumba ya kina nani.
 
Kwa Kuwa tumehamia Kiroho jibu ni kweli kabisa kuna Viumbe Vingi sana Ambavyo ni Adui (Satan) wa Binadamu kiroho Viumbe hivyo vinaweza kuwa Ni Visivyoonekana Na Vinavyoonekana..

Vinavyoliwa na Visivyoliwa..
Kuna Viumbe au Vyakula Pia Usisahau tunavyokula Vinaweza kusababisha Vikwazo vyetu kiroho..
Unavyojibu maswali ndio unazalisha maswali zaidi..

Vyakula/viumbe gani ukila vina madhara kiroho??

Uadui wetu na viumbe hivyo unasababishwa na nini? Tuna silaha ya kupambana navyo?
Vipi nikiungana navyo? Kuna madhara gani?
 
Unavyojibu maswali ndio unazalisha maswali zaidi..

Vyakula/viumbe gani ukila vina madhara kiroho?
Natamani Kuingia Deep sana nikueleweshe ila Naogopa Kwenda Deep Sana Nitakuchanganya Sana..

Mwili wa Binadamu Una Nishati (Energy) mbali mbali hiyo Energy ikiwa Vizuri ndo hufanya wewe Kuweza kumanifest Kwenye baadhi ya Dimension au kukuwa Kiroho Au Kuweka Kinga katika Maisha yako Au kukufanya wewe Uwe ulivyo hivyo...
Hasira, Furaha, Upendo chuki vyote hivyo Hutokana na Mwili wako Na utunzwaji wake..

Hujawahi kusikia Mtu anakuambia kuwa ameanza kula vyakula Fulani akaanza kujisikia Ana hasira hasira Kuliko kawaida??

Au Mwingine akila Vyakula fulani anakuwa Mpole?
Vipi kuhusu Kichuri kwa Wakurya?

Sasa Tulivyo sisi Nishati za mwili wetu na hata Mwili wetu unavyojijenga Ni jinsi tunavyokula kunywa vyakula vyetu..

kuna Baadhi ya wanyama Wanachangia katika Kushusha Nishati ya Mwili wako (Wana High negative energy) Au kwa Spiritual hutumia Neno wana evolve..

Japo Nyama nyekundu na zaidi ikiwemo Kitimoto Kwa ujumla Sio salama kwa sababu hupunguza energy (Lower Spiritual Vibration), Vyakula vya Viwandani Processing Food and Drinks pia sio Salama kabisa Navyo Huzuia Spiritual Vibration..

Kwa wale wanaofanya Meditation watakubaliana Na Mimi Kuwa Akitumia Vyakula Vya Majani (Vegeterian) kwa zaidi ya Wiki mbili halafu akafanya Meditation Hujikuta Hatumii nguvu nyingi sana kupata Matokeo mazuri..

Ila kama ukitumia Nyama na Vyakula Visivyoruhusiwa Hujikuta Anatumia Nguvu nyingi sana na Hasa Kupata Utulivu wa Nafsi kipindi cha kufanya meditation..

Processed na Sugary Foods kama nilivyosema mwanzoni Generally they are seen to "clog" the body and mind. Yaani Kunakuwa na kizuizi cha Mwili kwenda Kutap Into subconsious na Sio tu Hivyo Pia Inareduce mental clarity na kufanya meditation na spiritual practices harder.

Caffeine ,Sigara na Alcoho sio Nzuri kabisa kwa sababu Caffeine stimulates the mind, potentially leading to restlessness, while alcohol ina dulls awareness na kuwa considered toxic to both body and spirit..

Nafikiri mpaka Hapo unaweza kuwa umenielewa vizuri na hiyo Ndo maana Halisi Ya Wayahudi Kuzuia Hivyo vyakula Na Kula Vyakula Vilivyo KOSHER tu..
Ambavyo Utavipata Kwenye Mambo ya walawi 11..

Sasa ndo maana Paulo (Kwenye Biblia)

1 Wakorintho 6:19

"Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;"

Paulo alifuata Sana Hizo njia na ndiyo maana Paulo alikuwa anafanya Mpaka Astral Projection mpaka Mbingu ya Tatu..

Soma 2 Wakorinto 12:1-6..
Angalia Hapo chini anavyosema na anasema hawezi kujisifu kwa hayo, Ni experience ambayo yeye Mwenyewe Najisifu nayo na anasema kwenye Fungu la 5 kwa habari ya Mtu huyo Nitajisifu lakini kwakuwa nafsi imeumbwa na Kibuli (Ego) basi hatajisifu..
Screenshot_20241027_202607_Biblia Takatifu.jpg


Sasa Tuache Hayo unajua Watu pia Hawaelewi Kuhusu Lile Fungu la Kutoka 20:5

Kutoka 20:5
".........kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao...."


Kama Ukitaka Maelezo kuhusu Fungu hilo maana Lipo na Maelezo ya Kisayansi kidogo naweza kukuletea kama Unajua Maelezo yake Vizuri nalo linahusu Maswala ya Vyakula na Kujitunza kwa mwili
 
Back
Top Bottom