Kitabu cha Enock (Henoko)

Unafanya kazi nzuri Mtumishi..

Naomba sana Ndugu zangu wanaobeza Maandiko ya Manabii wengine kuita ni story za kufikirika na wengine kusema ni za mashetani wajitathimini sana..

SIRI AMBAYO WENGI HAWAJAWAHI KUIFAHAMU NI KUHUSU UNABII, MAANDIKO MATAKATIFU NA WAPI YAMEANZIA (ORIGIN)

Wengi wanaamini Biblia ya kwanza ni Hebrew Bible ila sio kweli, na hizi Bible za King James na Nyingine nazo sio za kwanza.. BIBLIA YA ETHIOPIA ndo BIBLIA KONGWE na imeandikwa kwa Lugha yao GE'EZ ina vitabu 81-88 na kitabu cha Nabii Enock kipo hakikutolewa..

SIRI AMBAYO WENGI WAMEFUNGWA HASA UFAHAMU ni kushindwa kukaa kutafakari hata kwa kupitia yaliyojili kwa Wana wa ISRAEL pale MISRI, WANA WA ISRAEL HAWAKUWA HAWA MNAOWATAJA (WAZUNGU)..

Kuna siri kubwa iliyofichwa ambayo inagusa KANISA LA ORTHODOX ambalo ni kongwe kabla ya Makanisa ya Roman Catholics, Lutheran na mengine yaliyoanzishwa na Falme zenye Nguvu na Wanaharakati wa kale kama Martin Luther nk.. Kanisa ya Orthodox pale Ethiopia bado linafundisha kwa Injili kwa kufuata miongozo na tamaduni za kale.

Kufanya story iwe fupi ni hivi.. Hao WAZUNGU (Waisrael wa sasa) HAWAJAWAHI KUWA WATUMWA CHINI YA PHARAO PALE MISRI.. Hata wakati Musa akionesha Ukuu wa Mungu mbele ya Pharao hadi anaweka mkono wake kwapani unatoka mkono ukiwa na weupe halafu anarudi hali ya kawaida hiyo isingotokea kwa Musa mzungu kama wa kwenye FILAMU zilizotengenezwa na Wazungu hadi za Nuhu, Yesu nk.. Haya yote yamefanikiwa baada ya Uvamizi wa Julius Ceaser hapa ndo walijua namna ya kuanzisha propaganda wakafanikiwa kututawala kupitia Explorer, Missionaries na MIFUMO waliyoiweka ambayo wamekuja kwa njia nyingine ya kisasa zaidi kututawala bila nguvu bali kwa akili kwa kuamini MAIGIZO YAO. ACHENI KUAMINISHWA KILA JAMBO!

KUMTAWALA MWAFRIKA IMETUMIKA AKILI KUBWA SANA HASA KUTUGOMBANISHA KWENYE DINI na lugha ndo imetumika kuleta tafsiri tofauti ili kutugawa na kuacha kufuata MUNGU WA KWELI WA MABABU ZETU tukaishia kufuata MIFUMO ya wanaotaka kututawala kupitia UDINI..

SIKU WAAFRIKA MKIACHA UDINI na KUFUATA IMANI kwa kumwamini MWENYEZI MUNGU PEKEE badala ya hizi vuta nikuvute za kutafuta Utajiri na Miujiza na kuamini Mataifa fulani ndo yamebarikiwa zaidi yako, ndo tutatoka kwenye kifungo au utumwa wa kifikra.. Fatilieni sana story ya Musa aliwapigania ndugu zake waliokuwa wanafanana nae na hata kwenye Pyramids zimechorwa picha watumwa walikuwa Waafrika pale misri ndo maana hata baada ya kuondoka pale Misri walienda umbali mrefu sana miaka 40 hawakuwa wamefika (inafikirisha sana).. Sasa Israel ya sasa kabla ya 1948 kupitishwa na Wamarekani na Waingereza tayari kulikuwa na nchi kama 7 kuchagua wapi waishi hata maeneo ya East Afrika yalikuwa kwenye list, Argentina pia ila Wazungu wakaona ili kutawala siasa za Middle East bora waingie eneo ambalo Wafilisti walivamia zamani wapewe hifadhi baadae wamewageuka Wafilisti wanasema ni eneo lao wakati wote wale eneo sio lao bali la Waafrika ambao walipewa na Mungu (fatilieni sitaki kuwaingiza kwenye siasa ila nawaonesha historia namna imepikwapikwa).

Kuonekana Primitive leo ni suala la mifumo iliyowekwa kwa WAAFRIKA MUISHIE KUUANA kwasababu ya UDINI, UBINAFSI na ELIMU YA KUKARIRISHANA wao wanazidi kutengeneza vizazi vyenye IQ kubwa.. Kuna watu wanaamini kuna Mwanadamu kapendelewa zaidi kapewa IQ zaidi ya wengine kama Mbarikiwa.. Hii toka napata kuelewa mifumo ya kidunia.. IQ inajengwa na mazingira na mambo unayofuata, ukifuata story za mafundisho ya kupandikizana chuki kamwe huwezi wafikia wazungu wala wachina.. Acheni kuwalisha sumu watoto wenu na vizazi vingine ndo mtaona BARAKA MMEPEWA NA MUNGU..

Story imeanzia kwenye Kitabu cha Enock, ninaamini Manabii walikuwa Waafrika na nitaendelea kuamini mwanadamu wa kwanza kuumbwa na Mwenyezi Mungu alikuwa Mwafrika ndo maana wale waliokwisha vuliwa hili Taji wanabaki kuwabagua Waafrika ngozi yao ili sasa wajisikie vibaya waende kutumia CHEMICAL ZAO wapate Kansa kama wao.. Mwafrika ameumbwa kwa udongo akapewa ngozi yenye kuhimili hali yoyote ila kufuata Tamaduni za nje ndo imepelekea WAAFRIKA HAWANA LENGO MOJA WALA SIO WAMOJA TENA BALI WANAWAZA KUDHURUMIANA na KUUANA.. ACHENI MAFUNDISHO YA CHUKI. FUATA IMANI YA KWELI INAYOANZA NA WEWE, SHIRIKI NA KILA MMOJA KATIKA KUSAIDIANA NA KULETA MAENDELEO KWENYE JAMII ZETU.

ROHO ZA KIBINAFSI NDO UBEPARI WENYEWE UMEWAFANYA WATU KUWA NA ROHO MBAYA.. NITAFUATA UJAMAA SIKU ZOTE MAANA HUKO NDO KUNA UPENDO WA KWELI, SIO HII CAPITALISM KWA KIVULI CHA ELIMU NA UDINI. HATUTAFIKA POPOTE!
 
Sehemu ya tatu

Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika.
Weusi, meusi tii......!

Hivi weusi ni ubaya? Nimefikiria tu na kujiuliza kwa nini hao ambao waliasi wakawa weusi ? Hata machozi yao ni meusi. Weusi huashiria nini ndugu wataalamu?
 
Aliwaona malaika wamening'inizwa kama wananyongwa lakini hawafi, wanapitia mateso makali wanalia kila dakika. Alivyouliza akajibiwa kwamba hawa ni wale wanaompinga Mungu!
Dah kumbe mambo ya utekaji yalianzia huko, kweli hakuna jipya duniani na pengine wana hoja za msingi tu maana hao ndo hukaa meza moja na sir God kwa hiyo lazima wanajua siri nyingi lakini ndo hivyo wakihoji wanatekwa
 
Ngoja aone KILANGA !
 
mhh!
hii sehemu ya tano ina mahusiano yoyote na hiyo picha?
 
Swali kwanini mungu awatese watu wake kiasi hicho..je mungu ananufaika nini na mateso yao ya milele?
logic and reasoning.
 
Nimerudia kusoma comment Yako mara 2 na Bado sijaelewa, ntarudi Tena kuisoma labda ntailewa baadaye.
 
Kwahiyo jomba shetani hayupo ni nadharia tulizojiwekea sisi tu??
 
Wakati Enoch anaona aliyoyaona, hakua katika Mwili wa Kawaida, mambo mengi ya Mbinguni huwezi kuyaona ukiwa na Mwili huu wa Nyama...!

So ilibidi awe out of the body achukuliwe na kwenda huko Mbinguni...!

So baada ya Enoch kwenda Mbinguni alirudi kwenye Mwili wake na Maisha mengine yakendelea, angeweza kuchukuliwa wakati mwingine Tena na angerudi Tena Duniani...!

Ila Mungu alipomnyakua kwenda Mbinguni the last time, haikua kumuonyesha maono yoyote, ilikua kumbeba Mazima.
 
Nimesikitika sana hivi huwa inawezekanaje mtu kuzungumza utumbo wa hivi halafu hadharani kabisa..... Walokole mna nn nyie, mbona Kila siku kuzidi kuithibitishia Dunia kuwa mmejaza ujinga kichwani
 
Kwahiyo jomba shetani hayupo ni nadharia tulizojiwekea sisi tu??
Ukienda Katika Uislamu Shetani wako pande Mbili Kuna Shetani wa Kijini Na shetani wa Kininadamu..

Tuje katika Asili yenyewe Neno Shetani limetokana na Neno la Kihebrania neno shetani (שָּׂטָן)..
Linamaanisha Adui (Adversary) au Mshitaki (accuser)..

Ntakupa Mafungu kadhaa Ambayo Neno shetani Limetajwa ila halikumaanisha Shetani kama Mtu/Jini au Malaika aliyeasi..

Hesabu 22:22

In Hebrew

וַיַּכְעַס אֱלֹהִים כִּי הוֹלֵךְ וַיַּעֲמֹד מַלְאַךְ יְהוָה בַּדֶּרֶךְ לְשָׂטָן וְהוּא רֹכֵב עַל-אֲתוֹנוֹ וְשְׁנֵי נְעָרָיו עִמָּדוֹ

inatamkwa..

Va'yik'chas Elohim ki holech, va'ya'amad malach Yahwe baderech le'shetan; ve'hu rochev al-atonoh, ve'shnei ne'arav immo."

Kwa Kiswahili

"Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye."
Twende Kitabu kingine

1 Samuel 29:4:
וַיִּקְרוּ אֱלֹהִים אֶל-עַבְדֵי אֲכִישׁ לֵאמֹר: שָׁבוּ אִישׁ אֶל-מְקֹמוֹ אֲשֶׁר-נָתַתָּ לוֹ וְאַל-יֵרֵד אִתָּנוּ לַמִּלְחָמָה, פֶּן-יִהְיֶה לָּנוּ לְשָׂטָן בַּמִּלְחָמָה; וּמַה-יָּבִיא אֶת-לֵב אֲכִישׁ אֲחִישׁ הַיָּדָוְ

Inatamkwa

"Va'yik'ru Elohim el-avadey Achish le'mor: Shavu ish el-mekomo asher-natata lo ve'al-ye'red itanu la'milchamah, pen-yih'yeh lanu
le'shetan ba'milchamah; u'mah-yavi lev Achish achish hayad."
kiswahili fungu Hilo..


"Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?"

SO kama Ulivyouliza nitajibu Kuwa Shetani Haikuwahi kumaanisha Status ya Mtu mmoja au utambulisho wa Mtu fulani Hapo zaman..

Mpaka Kwenye Medieval Period au Tunaita Medidval thought of satan kuanzia Karne ya 4 C.E ambayo iliamza Kumsingularised Shetani kuwa ni mtu mmoja wakati haikuwa Mtu bali ilikuwa Ni sifa ..
Nadhani nimejibu swali lako labda kama una swali la nyongeza
 
KUMTAWALA MWAFRIKA IMETUMIKA AKILI KUBWA SANA HASA KUTUGOMBANISHA KWENYE DINI na lugha ndo imetumika kuleta tafsiri tofauti ili kutugawa na kuacha kufuata MUNGU WA KWELI WA MABABU ZETU tukaishia kufuata MIFUMO ya wanaotaka kututawala kupitia UDINI..
 
Hiyo picha ya raisi na watu wengine inahusikaje na maandiko ya biblia!
Nahusika na maandiko yangu sihusiki na tafsiri zako.. Kwani hiyo picha yuko pekeyake? Yakhe vp Maalim mbona kama ....
 
Swali kwanini mungu awatese watu wake kiasi hicho..je mungu ananufaika nini na mateso yao ya milele?
logic and reasoning.
Hili linahitaji mada kamili inayojitegemea.. Na kwa kuandaa ithibati za kutosha
 
DR Mambo Jambo asante sana kwa ufafanuzi uliojaa weledi na Maarifa mengi 🙏🏿🙏🏿🙏🏿 kuna vitu vipya nimejifunza hapa.. Barikiwa...!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…