Na pale Yesu alipomwambia Petro
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Math 16:23 Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”
Alimaanisha nini hasa?
Kwa mujibu wa tafiti zako kuna kiumbe au viumbe ambao ni adui wa binadamu kiroho??
JIbu ni Lile lile Mkuu..( Japo Jibu litakuwa Refu ila ningependa Usome Nimejibu With Mindset ya Dini Kabisa)
Lets View It on the Perspective unayotaka..
Agano Jipya Most of It imeandikwa Katika Lugha ya Kigiriki au Wenyewe wanaita Kiyunani..
Math 16:23, Origina kabisa inaandikwa hivi
"
Ὁ δὲ στραφεὶς εἶπεν τῷ Πέτρῳ· Ὕπαγε ὀπίσω μου, σατανᾶ· σκάνδαλον εἶ ἐμοῦ, ὅτι οὐ φρονεῖς τὰ τοῦ Θεοῦ, ἀλλὰ τὰ τῶν ἀνθρώπων."
Kimatamshi
"
Ho de strapheis eipen tō Petrō, Hypage opisō mou, satanâ; skandalon ei emou, hoti ou phroneis ta tou Theou, alla ta tōn anthrōpōn."
Tafsiri ya Kiswahili Umeshaitoa bhasi na mimi nakupa Tafsiri Ya Kule kwa Kina Trump
"But he turned and said to Peter, 'Get behind me, Satan! You are a stumbling block to me, for you are not setting your mind on God’s interests, but man’s.'"
Kwakuwa Tafsiri (Translation) Umeshaitoa
Naomba Nitoe Tafsiri Fafanuzi (Interpretation)
Kama unajua Kigiriki hata kidogo tu kwanza Angalia Neno Lenyewe baada ya
Satanâ Likafuata neno ambalo alimuita "
skandalon" (σκάνδαλον), Linalomaanisha Kiswahili "
kizuizi" au
Kkikwazo au Kwa sahz Tungesema Wewe Ni
kizibo ila kwa Lugha ya Obama wangesema "
stumbling block" or "
offense." Kwa lugha ya Kigiriki kuna neno Jingine hapo "
ὀπίσω" (opisō) ambalo linamaanisha Nyuma...
Sasa kwa pamoja Ukiangalia Maneno hayo yote yalivyotumika Na mpangilip Wake ni kwamba Peter au petro au Kefa alikuwa Anazuia Ama angezuia Yesu kukamatwa na Alikuwa ameanza kushinda kwa kupandikiza imani hiyo ya kuzuia ukamatwaji wa Yesu kwa wanafunzi wengine..
Jambo hilo lilikuwa Limeanza kuwaingia wanafunzi na Wao wakaanza Kuondoa Uoga na walianza kama kujenga Ujasiri wa Kuzuia Kukamatwa kwa Kiongozi wao kama Ilivyokuwa kwa Osama kwa Alqaida (Natania) 😅😅
Yesu alipoona Hilo aliona Ile Devine stability ya Ukombozi imeanza Kufifia Kutokana na Petro Kuingiwa na Tamaa ya kuwa na Yeye Milele ndipo alipotumia Ujasiri Kuikemea Ile Mindset Bila ya Kuogopa na wala Hakukusudia Kuwa petro ndo huyo Shetani sasa (Tunavyoamini baadhi yetu) ila Mawazo yake yalikuwa Pingamizi au ya Kiadui kutokana na Ukombozi ambao Uliokuwa Mbele..
Kwahyo Petro ndo alikuwa Katikati kati ya Ukombozi Wa Yesu Kufanyika na Kutokufanyika..
Kwa bahati mbaya ama Nzuri Petro alitaka Kushinda roho ya Kumsaliti Au kumuachia Yesu aende (Kibinadamu Ilikuwa Roho nzuri ila Kwa Kiimani haikuwa Roho nzuri) kwa sababu ingezuia Ukomboni (Nasema kwa Njia za Kiimani zaidi)
Au hata Wewe Jiulize Vipi kama Yuda angekuwa Mwema na Akakataa Offer ya Vipande alivyopewa na watesi (Kibinadamu angefanya Vyema ila vipi kuhusu Ukombozi??)
Sasa Fungu hilo uliloleta Halina Tofauti na
1 Samwel 29:4 ,
Pale ambapo Balaam Alitaka Kuwalaani Wana wa Israel na Malaika akasimama kumuuliza kwanini anakuwa Shetani...
Nimeelezea hilo kwenye Post uliyoQuote..
Nafikiri Umenielewa