Kabendera kapitia changamoto nyingi sana. Kukamatwa kwake, kukaa ndani na mateso kadhaa. Mpaka kufiwa na mama yake.
Kama binadamu lazima uelewe yupo katika hali gani anapotajiwa jina la Magufuli. Hawezi mpenda na hata wewe usingeweza mpenda.
Nimesoma kile kifungu anachosema Ben Saanane aliuawa na Magufuli mwenyewe kwa kupigwa risasi ya kichwa. Kaandika kiwepesi sana, kirahisi sana. Ile issue yenyewe tu ilipaswa kuandikiwa kitabu kizima.
Kwa maelezo yake yale hamna kitu kabisa. Yaani kaandika habari kubwa kama hiyo kama vile kaambiwa, kasikia kijiweni then yeye kaiweka kwenye kitabu. Hapo ni wazi Kabendera aither Elimu yake ni ya mgogoro au aliendeshwa sana na hisia.
Kile kitabu alipaswa aandike bila chuki, angeandika vizuri sana bila mihemko. Hisia si jambo baya ikiwa zinakuwa controlled na mtu ambaye atakuwa unbiased. Kabendera kaandika nadhani alipaswa awapatie watu wenye akili wapitie na wamshauri. Tukio la Rais kumpiga mtu risasi linahitaji maelezo mengi sana ya kitaalamu/kisheria ili kuleta uhalisia wenyewe. Na hii haiwi nimeambiwa.
Huwezi andika kitabu kama hicho bila uchunguzi wa kina bila kuchimba zaidi na zaidi kupata ukweli.
Nadhani Kabendera ashauriwe mapema kabla hajaki print aelekezwe aandike vipi hilo jambo zito. Si kwa maneno mepesi vile kama vile si kitu kikubwa.
Then mambo mengine yaendelee uhalisia wake ubainishwe.