Kitabu cha Erick Kabendera: Ni vema atoe ushahidi wa tuhuma alizochapisha kuhusu Magufuli kuhusika kifo cha Ben Saanane

Hayo ni maneno ya Erick Kabendera ambaye anasema aliongea na watu walioshuhudia tukio hilo. Mambo hayo aliyasema wakati akitoa "teaser" ya kitabu chake "IN THE NAME OF THE PRESIDENT" ambacho kinaelezea madhila ya utawala wa awamu ya tano

Kwa uhondo zaidi wa habari hii, nenda kanunue kitabu.

Lakini aliyasema wapi, ni katika ukurasa wa YouTube wa Ghassan, pita huko fasta.
 
Hii sio story ya kutunga ni ukweli kabisa. Hakuna chochote kilixhobadirika kati ya aliyosema Kabendera na niliyoyasikia mimi pia almost 5 years ago. So huu sio uongo ni ukweli kabisa!
 
Gentleman,
nilitegemea upotoshaji mwisho ilikua 2024, naona kama umevuka na hadi2025, si utapata tabu sana?


halafu si naskia team ya mdomo na matusi iko retreat ubeligiji?


mwaka huu tufanye siasi, uchambuzi na ufafanuzi bila matusi tafadhali sana ndrugo zangu.

na ni vizuri mdau akilikoroga pekeyake basi alinywe mwenyewe pia na itapendeza zaidi πŸ’
 
kabendera alipitia wakati mgumu sana lakini ni kutokana na unadishi huu wa mihemko usiokuwa na vipimo ndio uliomingiza kwenye 19 za magufuli. Kuna makala moja aliiandika kwenye Jarida fulani, nadhani Newsweek au Economist a kutumia laughs kuwa "the stupid decision of the president" halafu editor wa jarida hilo akaitoa vivyo hivyo bila kuifanyia editing na ndiyo iliyomuweka matatani. Hakuwa na haja ya yeye kujifanya ni smart kuliko president na eti president ni stupid, Angetumia maneno kama ill advised decision, questionable decision, au dicey decision, lakini siyo kusema studid decision. Poor choice of words imeharibu maisha yake yote hata baada ya Magufuli kutangulia.
 
Pamoja na kwamba simkubali JPM lakini siamini kama anaweza kumpiga risasi mtu isipokuwa kutuma polisi wale wavuta bangi wafanye hilo tukio
 
Tofautisha kati ya "kutembea nayo" na "kuwa nayo" kwa muda tajwa mwagito.
 
Mimi sijakisoma, umekisoma chote? Wakati mwingine watu wanaweza kuchukua mstari mmoja na kuufanya kuwa kitabu chote. Lakini pia kama ana justification ya claim yake, shida Iko wapi? Kama mwandishi wa habari za kiuchunguzi (investigative journalist), na ambaye most probably ame'consult' watu kadhaa, including lawyers, na wakampa go ahead ya maudhui ya kitabu. Let's give him the benefit of the doubt. Kuna kanuni moja nimejifunza katika moral philosophy kwamba "when in doubt/uncertain about something suspend judgement". Sisi tuna tendency ya kutoa hukumu hata kama hatujui undani wa jambo fulani, maana tunafikiri tukisubiri mpaka tujue ukweli wake tutakuwa tumechelewa. Hivyo, tuna huu utamaduni wa kuwahukumu watu unfairly bila kujua undani wa jambo wanalolizungumzia, na hili ni tatizo kubwa kwetu.
 
Ni kweli amepotea, ushahidi kuwa ameuwawa anao huyo mwandishi sidhani kama Kuna mtu mwingine anajua Ben alipo zaidi ya Kabendera. Kwa sababu kuuwa mtu ni kosa basi nadhani Kabendera Atoe ushahidi kuwa Magufuli alimuua saa nane kwa kumpiga Risasi ya kichwa ikulu ili Haki iweze kutendeka. Familia ya Ben inasuburi mpaka Leo kujua kijana wao Yuko wapi hukumu itatolewa hata kama muuaji ameshakufa atahukumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…