Kitabu cha Erick Kabendera: Ni vema atoe ushahidi wa tuhuma alizochapisha kuhusu Magufuli kuhusika kifo cha Ben Saanane

Kitabu cha Erick Kabendera: Ni vema atoe ushahidi wa tuhuma alizochapisha kuhusu Magufuli kuhusika kifo cha Ben Saanane

Kaandika upuuzi sana. Hivi kweli rais amuite mtu ikulu halafu ampigie Risasi na kumuua hata kama alikua anataka kumuua Rais ana vyombo vingi hizi Tuhuma ni nzito lazima azithibitishe. Nitashangaa sana kama serikali italifumbia macho suala hili
Kwani hao serekali hawajui ukweli? Sana sana wakimuita wataishia kumtishia asiendelee kuusema huo ukweli.
 
Kaandika upuuzi sana. Hivi kweli rais amuite mtu ikulu halafu ampigie Risasi na kumuua hata kama alikua anataka kumuua Rais ana vyombo vingi hizi Tuhuma ni nzito lazima azithibitishe. Nitashangaa sana kama serikali italifumbia macho suala hili
Toa ushahidi kwamba hakuhusika, mwandishi wa kitabu hicho (kwa jinsi alivyo nukuliwa) tayari kamwaga ugali, wewe mwaga mboga zako ili mbivu na mbichi zijulikane, sio hizi habari za kukipiga marufuku kitabu au kuomba taratibu nyingine.
 
Atathibitisha huyo kabendera

..kwanini basi hatuundi Tume ya Uchunguzi, au hatuiti wachunguzi huru toka nje?

..wahusika kutokutekeleza wajibu wao ndio kunasababisha watu kama Kabendera wachukue nafasi ya kuwa wachunguzi.

..tunakosea kumlaumu Kabendera, at least yeye kajiongeza kutafuta ukweli. Kama umeupata, au la, hilo ni suala lingine.
 
Huyu mwandishi amezindua kitabu chake Leo na amechapisha Tuhuma nzito dhidi ya Marehemu Rais Magufuli kuwa yeye Binafsi alimuita Ben Saa nane ikulu na kumpiga Risasi Kisha mwili wake kutupwa katika mto rufiji.

Hizi ni Tuhuma nzito sana ambazo hazina ushahidi wowote dhidi ya aliyekua mkuu wa nchi. Zikiachwa kusambaa bila mwandishi huyu kuthibitisha zitasomwa na itaaminika ni kweli.

Nashauri mambo mawili ya kufanya

1. Kitabu alichozindua leo kizuiwe kusambazwa na kipigwe marufuku ndani na nje ya nchi.

2. Huyu mwandishi aitwe na kuhojiwa na vyombo vya usalama kuhusu Nia yake ya kuchapisha Tuhuma nzito hizi bila ushahidi otherwise Atoe ushahidi kuwa Magufuli alimpiga Risasi Ben Saa nane.View attachment 3190238View attachment 3190239
Hatari sana.

Ila mifumo huwa inafanya kazi kwa njia kadha wa kadha ila zipo njia mbili ambazo ndio huwa zinatumiwa sana ili kuulinda mfumo wenyewe au taarifa za kimfumo.

Mifumo inamalango ya kuingilia na malango haya huwa yanalindwa so wapaswao kuingia ndio pekee wanaoruhusiwa kuingia kwa maana hao ndio hupewa funguo.

Sasa ikitokea ikaonekana funguo zimeanza kuwafikia hata watu ambao hawapaswi kuingia ndani basi kinachofanyika ni kubadili kitasa kisha kugawa tena funguo kwa wahusika na mara hii umakini huwa ni WA hali ya juu huku wale ambao walipata funguo kibahati mbaya wakiachwa na funguo za kale ambazo hazifanyi tena kazi katika mfumo.

Na ikitokea taarifa za siri za ndani ya kimfumo zimevuja na kuanza kuwafikia watu ambao walikua wanafichwa juu ya siri hiyo, huwa kuna mambo mawili yanatokea.

Jambo la kwanza ni kukaa katika hali ya utulivu na ya kujiamini na linapokuja swala la wahusika kuombwa kuthibitisha taarifa hizo au wao wenyewe wakaona kwa level ya hizo taarifa ilipofikia kuna haja ya kutoka mbele na kuweka mambo sawa, huwa kwanza wahapingi na wala hawakubali ila wanabaki hapo katikati kiasi kitakacho kufanya au kuwafanya watu wawe puzzled.

Na baada ya kuwaacheni mko puzzled, hapo hapo njia ya pili inatambulishwa mchezoni ambayo hii ni njia ya propaganda na mlengo wa njia hii huwa mara zote ni kuufukia ukweli kwa uongo ambao ni ngumu kuutilia shaka, mara nyingi propaganda hizi huwa zinaanzia kwenye vyanzo venye nguvu na wahusika watakapoambiwa wajitokeze watoe ushahidi ni either washikwe na kigugumizi kuonesha kwamba hata wao hawajiamini na statements zao zinakua hazikamiliki na wakiwa hawako interested na hayo basi wanaweka kwenye engo ambazo ni ngumu kupata au kuhoji ushahidi ushahidi wa taarifa hiyo.

Na mchezo huu unaweza kuanzia mbele kurudi nyuma au nyuma kurudi mbele au katikati kwenda nyuma kisha mbele au katikati kwenda mbele kisha nyuma ilimradi tu mvurigano uwepo ili mfumo uwe salama.

Kwahiyo usiamini Kila unachokiskia na wala usidharau au kuchukulia poa Kila unachokiskia hata kama kwako wewe haupati connection Kila ukiunganisha dots, au kimekuja kwa udogo kuliko ambavyo ulifikiria kwa maana sometimes kwenye udogo ndio huwa kuna ukweli na kwenye ukubwa huwa hakuna ukweli.

Anyways, wacha tukitafute nasisi tuendelee kutoa tongotongo.

Soooo, bastola cash and... toa code someka
Wapi kilipo kitabu vipi kwa leo kitasomeka?... 😅😅
 
Back
Top Bottom