Kitabu cha kabendera ni hadithi za kufikirika na sio Facts, Serikali ipeleke Shitaka Mahakamani

Hizi ni claim ndani ya kitabu, tuna ziverify vipi ?

Nikitoka na kusema Mbowe ndio anahusika na kumuua Ben , taarifa hizi ni za ndani ya wstu wa chadema ila sitotaja majina kwa sababu za kiusalama, je Utaniamini maneno yangu ?

Be rational
 
Kila mara Chadema na wapenda haki wanasema wanataka haki kwa Ben S, ila sijawahi sikia wakisema kwamba Rais wa nchi alifanya kama Kabendera alivyoelezea
 
Peleka wewe kama raia.
Serikali makini haiwezi ikajibu shutuma hizi.
 
Mmmh !
 
First things first, serikali unayotamani ifungue mashtaka haina jeuri ya kufanya hivyo na wala haitafungua mashtaka. Mengi(if not all) ya ulichokiita biased allegations ni ukweli mtupu na Kabendera si mtu wa kwanza kuyamwaga peupe lakini amekuwa wa kwanza kuyaanika 'rasmi' tofauti na ilivyokuwa awali ambapo yalisambaa kama 'rumors'.
Being a scientist umepinga with zero facts, unadai ame-mislead pasina kuainisha ukweli(with your solid facts ili tulinganishe kati yako na Kabendera nani mkweli na nani ni muongo).
Bandiko lako ni manipulation 100%, unajifanya spin master kupotosha watu. Ikulu hawaishi malaika, ni watu kama wewe with their good, bad and ugly characters hivyo mtu kuuawa au kutokea jaribio la ubakaji ni kitu kinachowezekana kabisa. Unadai Kabendera can't prove anayodai yalitokea ikulu je upande wako can you prove kwamba hayakutokea?
Maelezo yako yameendeshwa na hisia(too bad) ila kwa zile tabia za Jiwe(namjua we used to be neighbors akiwa waziri) yote yaliandikwa kwenye kitabu hakuna cha kushangaza labda kwa wasiomfamu ndiyo watashangaa.
 
Faida ni kujua yaliyojiri, mama Janet amepitia madhila mengi ambayo hata Kabendera hayafahamu ndiyo maana hayamo kwenye kitabu.
 
Sasa mleta mada unasema kilichoandikwa na Kabendera kwenye kitabu chake ni hadithi za kufikirika, sasa unakwenda mahakamani kushtaki nini?
Unashtaki hadithi za kufirika za mwandishi ili iweje?
Yaani wewe unaumia nini na hadithi za kufikirika za Mwandishi?
 

..mbona ni rahisi zaidi kwa serikali kuchunguza na kumkamata aliyemuua Ben Saanane?
 
Sisi ndio tunapenda hizo hadithi.
Na ntanunua hata vitabu 3 ili nimuunhishe.
Vingine ntavipeleka "Machame VS Ikungi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…