Kitabu cha Munga Tehanani - Uchawi

Kitabu cha Munga Tehanani - Uchawi

Dhana Yako Ni ipi Mkuu?
Ni ujinga Upi tunapeana waafrika.
Ufafanuzi Tafadhari.
Hizo habari za uchawi mnaziamini mpaka zama hizi za uhakiki?

Unaweza kuthibitisha uchawi (si imani ya uchawi, uchawi wenyewe) upo kweli na si hadithi za watu tu, mauzauza ya uongo ya mazingaombwe na hadaa za kisaikolojia kama mchezo wa karata tatu?
 
Uchawi ni Halisi, Hizi si hadithi za wahenga.
Munga Teheran katika Kitabu chake alisema " Uchawi ni Matumizi Mabaya ya Nguvu hizihizi tunazo zitumia kupata Mambo Mazuri.
 
Habari za Uzima WanaJamiiForums.

Kuna kitabu Nimekipoteza ktk mazingira Nisiyoelewa, kinaitwa UCHAWI UNAVYOKUPATA NA KUJIKINGA Cha mwandishi MUNGA TEHENANI wa FAMILIA YA JITAMBUE.

Huyu Bw. Alikuwa anatoa Elimu yenye Ufahamu na Maarifa ya viwango vya Juu Mno ambayo sijaona mwingine Kwa hapa TZ ana Maarifa kama Yeye.

( RIP. MUNGA TEHENANI )
Katika Kitabu hicho alizungumzia Uchawi wa kuruka kwa Ungo.

Anasema, Sio lazima iwe Ungo, Lakini Kuna uwezekano wa watu kuruka kwa kutumia vifaa ambavyo havitumiwi kurukia.

Kama Yupo Mtu ataruka Kwa kutumia Ungo, sio lazima Mtu Huyo awe mchawi.

Kuruka ama kusafiri Kwa Ungo ni suala la uwezo wa kujua Namna ya Kanuni Husika inavyotumika.

Uchawi ni Matumizi Mabaya ya Nguvu hizihizi tunazo zitumia kupata Mambo Mazuri.

Hayo ni sehemu tu ya Yaliyomo Ndani ya kitabu hicho.

TAFADHARI, ikiwa unajua mahali naweza kupata kitabu hiki Nakuomba unijulishe.

Na kama unacho kitabu kama hiki naomba kopi Tafadhari.

Na ikiwa una NONDO nyingine za MUNGA TEHENANI

Naomba tujulishane Jamani.

Ni hayo tu.
Mwenye kitabu hiki anipatie nitamlipa vizuri.
 
MUNGA TEHENANI ktk Kitabu chake alisema hivi " Huko Ulaya, WAZO la wachawi kuruka kwa kutumia FAGIO la Mti, lilishika Mizizi kwenye Karne ya 16 na kuendelea.
Lakini baadae ilibainika kwamba hapakuwa na watu Wenye uwezo huo.
Ilikuwa ni Hali ya kuwatia hofu watu wengine.
Watu wanaoamini ktk Uchawi Hutengeneza visa asili vingi yaani hadithi za Uongo.
*** Kwa hapa kwetu inawezekana wapo watu Wenye Uwezo wa kuruka na Kusafiri Kwa FAGIO LA MTI.
Lakini kwangu Mimi Hawawezi kuwaitwa wachawi.
Kama Ni Lazima niwape jina, NITAWAITA WANASAYANSI WACHOYO.
KUMBUKA: Sio Kila jambo usilolijua na laajabu, ULIITE UCHAWI.
 
Mimi Sijui ila Natafuta Kujua.
1. UCHAWI NI MATUMIZI MABAYA YA NGUVU ZILIZO NDANI YETU.
Kumbe Binadamu tuna NGUVU Ndani mwetu.
Sasa kama nina nguvu ndani yangu, nguvu ya kufikiria na kugundua vitu, nikasoma Chemistry, nikagundua sumu, nikaitumia sumu hiyo kumuua mtu.

Kutumia nguvu ya kufikiri kugundua chemical na kumuua mtu ni uchawi?
 
Mwenye kitabu hiki anipatie nitamlipa vizuri.
Kwakweli Sasa inabidi tutangaze dau ili kukipata.
Ila Mimi Naamini Mshana Jr. Na Watu wa Jamii Yake, , , wanavyo vitabu vya MUNGA TEHENANI.
Naomba Tusaidiane Jamani Kumtafuta Mshana Jr wa hapahapa JF
Naamini tutapata Nondo zakutosha.
 
Sasa kama nina nguvu ndani yangu, nguvu ya kufikiria na kugundua vitu, nikasoma Chemistry, nikagundua sumu, nikaitumia sumu hiyo kumuua mtu.

Kutumia nguvu ya kufikiri kugundua chemical na kumuua mtu ni uchawi?
Nafikiri Elimu ya ST. KAYUMBA haiwezi kukupa matokeo chanya ktk Matumizi ya Nguvu zako za Ndani.
Nguvu zako za Ndani huweza hutenda MAKUBWA ambayo Elimu ya shule na vyuo haiwezi.
 
Aisee! Nilisoma sana magazeti yake Jitambue na lile lingine jina limenitoka, alifundisha sana elimu ya kujitambua, alikuwa na makala moja watu wanatoa visa vyao vya ukweli iliitwa " Jinsi nilivyofedheheka"...
 
Nafikiri Elimu ya ST. KAYUMBA haiwezi kukupa matokeo chanya ktk Matumizi ya Nguvu zako za Ndani.
Nguvu zako za Ndani huweza hutenda MAKUBWA ambayo Elimu ya shule na vyuo haiwezi.
Hujajibu swali langu.

Kimsingi umesema uchawi ni kutumia nguvu ya mtu ya ndani kutimiza nia mbaya.

Nimeuliza hivii.

Sasa kama nina nguvu ndani yangu, nguvu ya kufikiria na kugundua vitu, nikasoma Chemistry, nikagundua sumu, nikaitumia sumu hiyo kumuua mtu.

Kutumia nguvu ya kufikiri kugundua chemical na kumuua mtu ni uchawi?

Kama unajibu kuwa kutumia nguvu yako ya ndani kujua elimu ya Chemistry na kuitumia haiwezi kukupa uchawi, basi definition yako ya uchawiina matatizo inabidi uirekebishe.

Inaonekana umeshindwa hata ku define uchawi ni nini.

Na hili linaonesha kuwa ama wewe ni mjinga hujui kujieleza, ama hata wewe huelewi uchawi ni nini.

Which is which which?

Wewe ni mjinga hujui kujieleza au hata wewe huelewi uchawi ni nini ndiyo maana huwezi hata ku u define?
 
Uchawi ni Halisi, Hizi si hadithi za wahenga.
Munga Teheran katika Kitabu chake alisema " Uchawi ni Matumizi Mabaya ya Nguvu hizihizi tunazo zitumia kupata Mambo Mazuri.
Mzee kwa ushauri achana na kiranga huyo ni atheist huwezi kumuelewesha kikubwa achana nae.

Ni ushauri ukipenda pokea usipo upenda is up to you.
 
Back
Top Bottom