Kitabu cha Munga Tehanani - Uchawi

Kitabu cha Munga Tehanani - Uchawi

Mzee Munga ni moja ya watu wa kwanza kabisa kufundisha elimu hii ya kujitambua. Walikuwa na society inaitwa Life Wave na ilibadilika jina na kuwa The Path Society ambapo wapo Kigamboni kwa sasa.
Huyu Mr Munga niliwahi kumtizama TVT enzi hizo kwa sasa ni TBC. Kwakweli niliona mara moja kipindi chake kilikuwa kinaitwa Jitambue, nakiri niligundua jamaa ana uelewa wa mambo..

Baadae nilikuja kusikia amefariki dunia RIP Mr Munga Tehani
 
Si mtata hivyo mkuu, haya ni maswali ya msingi tu, maswali ya definition tu. Tujue mtu anaposema "uchawi" anamaanisha nini, kabla hatujaanza kubishana kama uchawi upo au haupo.

Nipo kwenye definition tu, hata sijaingia kwenye argument.

Sasa hapo kuna utata gani?
Hiki kitabu ninachokiulizia hapa kinayo majibu.
Tutafute Kitabu kwanza
 
Huyu Mr Munga niliwahi kumtizama TVT enzi hizo kwa sasa ni TBC. Kwakweli niliona mara moja kipindi chake kilikuwa kinaitwa Jitambue, nakiri niligundua jamaa ana uelewa wa mambo..

Baadae nilikuja kusikia amefariki dunia RIP Mr Munga Tehani
Hakika, Hata Mimi nilimuona kwenye TVT 2008.
Na baada ya Pale nikaanza kumfuatilia kwenye gazeti la JITAMBUE
 
Define uchawi nini halafu nieleze ni vipi unaujua huu ni uchawi, si kitu kingine chochote unachokijua au usichokijua.
Hivi kuna uchunguzi uliyowahi kufanyika ukaja na majibu kuelezea hicho kinachodhaniwa ni uchawi kwamba si uchawi ni kitu tu chengine na ni kitu gani hasa?
 
UCHAWI
UNAVYOKUPATA NA KUJIKINGA

ILIANDIKWA NA MUNGA TEHENAN 2007.

FAMILIA YA JITAMBUE

Habari Wanajamii Forum.
Naomba Kwa idhini yenu Nishushe KIPANDE CHA NONDO kinachohisu Uchawi Kwa kadiri ya NOTES nilizochukua kutoka Kwa Mwandishi MUNGA TEHENAN.

1. UCHAWI NI NINI?

Mwandishi anasema, Hilo ni swali gumu sana kuliko unavyofikiria.
Watu husema Kuna Uchawi na wengine husema Hakuna Uchawi.

Lakini Mtu anapoiliza Huo Uchawi ni Kitu Gani, Ndipo tunagundua Kwamba tunazungumzia jambo Tusilolijua.

Munga anasema,
Je, Uchawi ni kuwa na vifaa ambavyo Mtu anaweza kuvitumia kutengeneza Nguvu yenye kuweza kusafiri ma kwenda kumdhuru amtakaye?

Je, Uchawi ni uwezo wa kuweka sumu kwenye chakula au Maji watu wakatumia na kufa polepole au ghafla?

Je, Uchawi ni mbinu ambazo Mtu anaweza kuzifanya na kusababisha mwingine afukuzwe kazi bila sababu ya msingi?

Je Uchawi ni uwezo wa kumghilibi Mume au Mke wa Mwingine hata akatoka nje ya Ndoa yake halali?
Je, UCHAWI NI NINI BASI?

Mwandishi MUNGA TEHENAN anasema, , , , ,Nauliza maswali hayo kwasababu Uchawi Huwa unatajwa kwenye Matukio mengi sana.
Kwamfano;
Mtu kufukuzwa kazi
Kuugua
Kufa
Kuachwa na Mpenzi/ Mume/Mke
Kufirisika / kutajirika
Na mengine ya aina hiyo.

Tunasema Ni Uchawi kwasababu tumeupima Kwa Matokeo na Matukio.
Lakini nje ya Matokeo na Matukio HAKUNA UCHAWI.

Mwandishi anasema, Hauwezi kuukuta Uchawi ukiwa umewekwa mahali, Bali Unaweza Kuuona Ukiwa Unafanya Kazi.

Kama Ukikuta Tunguli, Hirizi na Pembe zenye manyoya Mahali, Huwezi Kusema Huo ni Uchawi.
Kwa maana wote tunajia kwamba, hivyo ni vifaa ambavyo hutumika Kwa shughuli mbalimbali.
Vinaweza kutumika Kwa Uchawi Lakini vyenyewe si Uchawi.
. . . . . . . . itaendelea
 
Tatizo la kiranga nimjuzi wa kutengeneza maswali ya Malumbano.
Kwamba wewe ukimjibu Kisha Yeye akanushe na jibu asitoe.
Fuatilia koments zake . . . Utaniamini Mimi.
Huajibi maswali.

Uchawi ni nini? Unajuaje huu ni uchawi, na hiki ni kitu kingine tu tofauti na uchawi labda hujakielewa tu?
 
Hivi kuna uchunguzi uliyowahi kufanyika ukaja na majibu kuelezea hicho kinachodhaniwa ni uchawi kwamba si uchawi ni kitu tu chengine na ni kitu gani hasa?
Watu wengi sana wanaumwa, wakienda kwa waganga wa kienyeji kuaguliwa wanaambiwa huo ni uchawi wamerogwa na ndugu zao. Wakati si kweli, ni ugonjwa wa kawaida tu.

Sasa ukiumwa utajuaje huu ni ugonjwa wa kawaida tu na huu ni ugonjwa wa kurogwa uchawi?
 
Tukiangalia kwa kina upande mmoja upo sahihi kwa ulichoeleza ni kweli hilo hutokea, ila pia kwa upande mwengine hutokea pia watu wanaenda kwa waganga baada ya kushindikana kupata tiba hospitali na hupona kwa matibabu ya waganga na hayo maradhi uhusishwa na uchawi.

Mbali na maradhi kuna matatizo mengine pia tunaona huwafanya watu kwenda kwa waganga kupata ufumbuzi.
 
Bado hujajibu maswali yangu.

Uchawi ni nini?

Utahakikishaje huu ni uchawi na hiki ni kitu kingine tu ambacho labda sijakielewa tu, lakini si uchawi?
 
Bado hujajibu maswali yangu.

Uchawi ni nini?

Utahakikishaje huu ni uchawi na hiki ni kitu kingine tu ambacho labda sijakielewa tu, lakini si uchawi?
Ndio maana mwanzo nilikuuliza swali kuwa je kuna uchunguzi uliyowahi kufanyika ukaja na majibu kwamba hicho kinachodhaniwa ni uchawi si uchawi bali ni kitu chengine na ni kitu gani hiko?

Naweza nisijue ni nini maana ya uchawi ila tunakutana na hayo yenye kuitwa kuwa ni uchawi, nimetoa mfano hapo watu kukosa tiba hospitali ila wakaambiwa na waganga kuwa kinachowasumbua ni uchawi na wakatibiwa kwa tiba za kiganga na wakapona, ndio maana nasema muhimu hapa kama ungefanyika uchunguzi ndio ungetoa majibu.

Kuwa tunaweza tukasema hicho kinachoitwa uchawi kuwa si uchawi ila linakuja swali je ni nini hicho?
 
Unafanya vipi uchunguzi kuhusu kitu ambacho hata hakijawa defined?

Uchawi ni nini?

Hilo ndilo swali la kwanza.
 
Unafanya vipi uchunguzi kuhusu kitu ambacho hata hakijawa defined?

Uchawi ni nini?

Hilo ndilo swali la kwanza.
Sasa mbona kuna watu wanapinga kuwa hakuna uchawi ikiwa haijulikani uchawi ni nini?

Wewe unasema kuwa hayo yenye kudaiwa kuwa ni uchawi yaweza kuwa si uchawi bali ni mambo mengine tu tusiyoyajua, hapo ndipo umuhimu wa uchunguzi unapohitajika maana kama kuna mambo ambayo hatuyajui na kweli yapo na yanahusu hadi maradhi na tiba basi huoni kuwa tunahitaji kuyafanyia uchunguzi kuliko kuacha kufanya uchunguzi kisa definition?
 
Back
Top Bottom