Kitabu cha "ushahidi kuwa Mungu hayupo na uchawi haupo" kiko njiani

Huwezi kumlazimisha ngombe kunywa maji, ngombe anayeonyeshwa bwawa la maji na bado akawa hataki kunywa maji basi huyo ni kumtakia kila la kheri.

Hivyo hivyo kila binadamu anao uhuru wa kuchagua
Mgonjwa wa ukimwi hawezi kudai eti anatibu ukimwi wakati yeye mwenyewe halitete. Endelea kunywa maji machafu mimi ng'ombe ninayejitambua nimeliona bwawa lenye maji safi vipi unilazimishe ninywe maji taka?
 
Mgonjwa wa ukimwi hawezi kudai eti anatibu ukimwi wakati yeye mwenyewe halitete. Endelea kunywa maji machafu mimi ng'ombe ninayejitambua nimeliona bwawa lenye maji safi vipi unilazimishe ninywe maji taka?
endelea kujitambua
 
Unabishana na umma
 
Unabishana na umma
Uma unachokiamini kimetoka wapi? Ni mambo yaliyotoka kale na jamii zimekuja zikirithishana na ni kawaida katika jamii yoyote kwa jamii kuwa na mapokeo ambayo siku moja anaibuka mtu na kusema jamani hiki tulichokifuata siku zote hakiko hivyo kiko hivi.

Jamii za watu wenye elimu bora, mijadala kama hii ni jambo la kawaida kabisa na kila anayekuja na hoja mpya wanamsikiliza.

Hoja wakiisikiliza wanaipima na wakiona yanayozungumzwa yana tija wanafuata, wakiona hayana tija wanaachana nayo.

Lakini katika nchi zenye elimu mbovu, watu wanakalili tu na kile alichokikalili atakibishia mpaka basi na hili ndilo tatizo letu.

Hoja kama hizi ndizo zitatupa heshima mbele ya jamii kwa kuonekana mtu mweusi na mweupe ni sawa. Si kukaa kukalili tu wanayoyaleta na hamtaki kusikia lolote kutoka kwa ndugu zenu ila wakaileta wao mnasikiliza na kufuata.

Huo ni utumwa wa ki fikra
 
Napita mimi.
 
Hebu rudia
Sijakuelewa
 
Mimi naaminikitu ninachokijua na wala sobahatishi,SisiWaislamu marammnyingi huwa tunasoma kwa kufahamu si kukariri tuu.Tunaposema kuna MUngu tuna maana Mwenye kumiliki Dunia nia Vilivyomo ndani yake ,Anga na Mbingu na Sayari na vile tusivyowez kuvidiriki.
Hakuna yeyote aliyedai kumiliki vitu hivyoisipokuwa Yeye Mmoja tuu Mungu
 
Kuamini ni kuchagua lakini ukitaka kuwa na uhakika na kile unachokiamini msikilize anayejaribu kukuchalenji na upime anatoa sababu zipi.

akikueleza ya kipuuzi mpuuze lakini akikwambia yenye mantiki msikilize
 
We kitoe tu hicho kitabu mbona ni cha kawaida tu na kidogo tu kulingana na vitabu vingine, vilivyobeba mazito.
 
Kwa mujibu wa Biblia QURAN na elimu za uchawi majibu kuhusu hizo sauti za mababu ni michezo ya shetani kuwahadaa watu.
Mtu akishakufa hana tena connection na walio hai. Japo wapo wanaokufa na wanarejea tena duniani lakini sio kwa kifo cha Mungu. Maana zipo aina mbili za vifo.
 


Mimi nadhani hujatumia akili yako vyema kutafuta je Mungu yupo au hayupo??!!.

Matokeo ya mambo au vitu kuwepo kwavyo na kutenda nidhamu ni ishara ya kuwepo kwa A Supreme conscious being, hii ni upembuzi wa akili ya kawaida tu bila kutumia vitabu au imani za kidini.

Hebu leo chunguza Kompyuta au programmed Robot, Vifaa hivyo vinafanya kazi kwa nidhamu iliyokusudiwa, nidhamu hiyo kaitengeneza mtu/Engineer aliyesanifu vyombo hivyo, katika utendaji kazi wa vifaa hivyo haiwezekani leo mtu azuke tu na adai kwamba kompyuta au Robot kwa utendaji kazi wake zimezuka zenyewe au zimejiunda zenyewe!!!.

Chukua mfano huo huo wa utendaji kazi wa Kompyuta na Robot na geuza huo mfano kwa ajili yako wewe mwenyewe na Mwili wako, Katika mwili wako kuna jinsia, je hiyo jinsia uliiomba wewe, yaani uliomba uzaliwe na jinsia hiyo??, au wazazi wako walitaka wewe uwe na jinsia hiyo??-- je ni nani alipanga uwe na jinsia hiyo??!!, Je, ni nani alipanga wazazi wako wawe ni hao ulionao??!!, kabila lako, race yako nk, ni nani alipanga??!!, katika mwili wako kuna mifumo ifuatayo 1-- mfumo wa upumuaji, 2-- mfumo wa umeng'enyaji, 3-- mfumo wa damu, 4--- mfumo wa fahamu, 5--mfumo kusikia, 6--- mfumo wa uzazi nk, mifumo yote hii inafanya kazi katika nidhamu kusudiwa, je ni nani aliyeweka hii nidhamu kusudiwa katika huo mwili wako na ili iweje??!! au hiyo mifumo ulijiwekea wewe mwenyewe na ukaipatia hizo nidhamu za utendaji kazi??!!--- kama Kompyuta, Robot na Magari na mitambo mbalimbali zimeundwa na Wataalamu na zina mifumo inayofanya kazi katika nidhamu kusudiwa sasa iweje upinge kwamba wewe hujaundwa na ndio maana mwilini mwako kuna mifumo inayofanya kazi kwa nidhamu tena nidhamu kusudiwa na huyo aliyekuunda??!!--- sio katika mwili wako tu bali hata katika viumbe hai wengine unaweza kujifunza kwani na wao wanavyo vitu ambavyokwavyo mtu anaweza kujifunza kwamba na wao wametengenezwa katika nidhamu ili kukidhi haja kusudiwa, haja iliyowekwa na mtengenezaji wao kwani hakuna kiumbe kilichojitengeneza chenyewe.

Kuzaliwa na kuzaana kwa viumbe hai nayo ni nidhamu iliyowekwa na huyo aliyekusudia nidhamu hiyo itende kazi kwa jinsi hiyo.

Pi Kuna mifano mingi hai kutoka katika vitu visivyokuwa hai kuhusu nidhamu ya utendaji kazi wao kiasi kwamba kwa akili ya kawaida tu mtu unajua kwamba vitu hivyo lazima vitakuwa vimetengenezwa na A supreme conscious being kwani haiingii akilini kudhani kwamba kuna kitu kinaweza kuibuka chenyewe na kutenda nidhamu fulani bila ya kuwepo na muanzilishi wa hiyo nidhamu.

Basi huyo Muanzilishi wa hizo nidhamu katika mwili wako ndiye Mwenyezi Mungu mtukufu.
 
ndugu yangu, unachojaribu kufanya ni kutumia "logic"

swala la hili linaweza kuwa tofauti na logic unazojaribu kutumia hivyo jiandae kusikiliza mawazo mapya unaweza kubadiri mtizamo
 
Utakumbana na upinzani mzito lakini nimesoma bandiko lako nikaona UNA HOJA. Kitabu kikikamilika tuuzie hata softcopy tupate maarifa mapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…