Faiza Huyo Mwarabu Mwenyeji wa Africa Mashariki Unayemzungumzia wewe ni Mwarabu yupi? ( Mwarabu Mweusi? au Mwarabu wa mweupe kama wa Oman) maana kwa tafsiri yako Mwarabu ni mtu yeyote anayezungumza kiarabu, hata akiwa mbantu ie. mzaramo, akijifuza kiarabu au akizaa mtoto uarabuni akajua kiarabu basi huyo moja kwa moja ni mwarabu haijalishi rangi yake or asili yake
Hapana si hivyo, ukiisoma ile post ya Makerere nnayo i refer sana ana ambayo nimeiweka hapo juu kidogo, utaona kuwa wengi wetu wanadhani Uafrika ni kuwa mweusi na kuwa Mbantu, Uafrika ni zaidi ya Ubantu kuna Waafrika wengi sana wasio Wabantu, hali kadhalika Uarabu si weupe au weusi. Mimi nimeuliza sana humu, lakini bado si wewe wala si mwengine aliyekuja na jibu, Jee, Iraqw wa Tanzania ni asili ya wapi? kuna ugumu upi kulijibu hilo? na Kihistoria, Wairaqw ni wa zamani zaidi ya Wabantu katika ardhi hii ya Afrika Mashariki seuse pwani ya Afrika Mashariki.
Mkandara hapo juu, baada ya mwenyewe kujibu kuwa "wafuasi wa Mtume" walikuja karne ya nne au ya tano pwani ya Afrika Mashariki, akashindwa kunijibu jee, kabla ya hapo kulikuwa hakuna misafara ya kwenda na kurudi huko walipotokea "wafuasi wa Mtume"? kabla ya ujio wa hao wafuasi? sidhani kama hilo lina ubishi, na kwa kuondoa tu ubishi nikamuuliza anajuwa historia ya Malikia Bilqis? au wewe nikuulize unaielewa historia ya Malikia bilqis?
Ukichukuwa wasaa kidogo na kujisomea hizo historia, kama tu hauzijuwi, utakuta kuwa Mwarabu hakuja Afrika bali alikwenda huko Mashariki ya Karibu ambako ki jiografia ni bara la Asia.
Ushahidi mwengine wa hivi karibuni ni, toka wanasayansi wavumbuwe kuziona na kuzisoma DNA, wanaweza sasa wakafatilia mtu huyu asili yake wapi, cha kushangaza, na wala si kwa kuwa wanatupenda sana, inaonekana mtu wa kale zaidi ki DNA katokea Tanzania na au Ethiopia na katokea kwa Wairaqw na wa karibu yake, na akatapakaa sehemu zingine za dunia.
Nnauhakika kabisa unajuwa Wairaqw ni akina nani na asili yao ni ipi. Isitoshe, hapo sijagusia kabisa utawala Malikia Bilqis, hapo ndiyo utachoka zaidi, nakuwachuia wewe unipe historia ya Utawala wa Malkia Bilqis.
Hilo nilikuwekea nyekundu, hapana, si kweli kuwa mzaram0 akijifunza Kiarabu basi kishakuwa Mwarabu. Lugha ya kujifunza si ya asili yako, huwezi kuidai hiyo asili kama lugha si mama kwako.
Uarabu na Ubantu si makabila ni lugha, Waarabu wana makabila yao na Wabantu wana makabila yao. Soma ile post ya Makerere utanielewa tu.
Kwanini Waarabu wakaitwa Waarabu?
Maana ya Arabiya ni 'caravan" au msafara, "Arab" au Mwarabu maana yake ni mtu wa msafara na lugha yao ni Kiarabu, kwanini? nakuwachia na wewe unipe jibu. Nnakumbuka nilipokuwa shule ya msingi tukifundishwa kuhusa wahamahamaji, sijuwi unawajuwa ni akina nani hao?
Jee, maana ya Bantu ni nini?