Kitabu kipya: Tanzania na propaganda za udini na prof. Ibrahim Noor

Vyamavingi,
Hapa tunazungumzia kitabu cha Prof. Ibrahim Noor hatuko kwenye
somo la jihad.

Ikiwa unataka kuzungumzia mada hiyo fungua uzi mpya kwenye
jukwaa husika.

Mzee, nimejibu upotoshaji wa Faiza kuhusu maana za maneno husika.

Vv
 

Asante Mkandara, waliotoa jina Zanzibar/Zenjibar ni hao hao Waarabu, wakamanisha nchi ya watu weusi; vilevile waliotoa jina la Sudan, walimaanisha weusi. Sasa wanaokuja na hoja kuwa Waarabu nao ni wenyeji zaidi Afrika Mashariki kabla ya Wabantu sijui wanajinasibuje kuwa ni Wasomi.

Vv
 
Huu mjadala ungenoga sana kama sio element za majigambo na kebehi.
Umahiri wa wengi una fichika.
Wenzenu hapa tunatafuta kujua.
Hiki kitabu kinapatikana online?
 

Hapana si hivyo, ukiisoma ile post ya Makerere nnayo i refer sana ana ambayo nimeiweka hapo juu kidogo, utaona kuwa wengi wetu wanadhani Uafrika ni kuwa mweusi na kuwa Mbantu, Uafrika ni zaidi ya Ubantu kuna Waafrika wengi sana wasio Wabantu, hali kadhalika Uarabu si weupe au weusi. Mimi nimeuliza sana humu, lakini bado si wewe wala si mwengine aliyekuja na jibu, Jee, Iraqw wa Tanzania ni asili ya wapi? kuna ugumu upi kulijibu hilo? na Kihistoria, Wairaqw ni wa zamani zaidi ya Wabantu katika ardhi hii ya Afrika Mashariki seuse pwani ya Afrika Mashariki.

Mkandara hapo juu, baada ya mwenyewe kujibu kuwa "wafuasi wa Mtume" walikuja karne ya nne au ya tano pwani ya Afrika Mashariki, akashindwa kunijibu jee, kabla ya hapo kulikuwa hakuna misafara ya kwenda na kurudi huko walipotokea "wafuasi wa Mtume"? kabla ya ujio wa hao wafuasi? sidhani kama hilo lina ubishi, na kwa kuondoa tu ubishi nikamuuliza anajuwa historia ya Malikia Bilqis? au wewe nikuulize unaielewa historia ya Malikia bilqis?

Ukichukuwa wasaa kidogo na kujisomea hizo historia, kama tu hauzijuwi, utakuta kuwa Mwarabu hakuja Afrika bali alikwenda huko Mashariki ya Karibu ambako ki jiografia ni bara la Asia.

Ushahidi mwengine wa hivi karibuni ni, toka wanasayansi wavumbuwe kuziona na kuzisoma DNA, wanaweza sasa wakafatilia mtu huyu asili yake wapi, cha kushangaza, na wala si kwa kuwa wanatupenda sana, inaonekana mtu wa kale zaidi ki DNA katokea Tanzania na au Ethiopia na katokea kwa Wairaqw na wa karibu yake, na akatapakaa sehemu zingine za dunia.

Nnauhakika kabisa unajuwa Wairaqw ni akina nani na asili yao ni ipi. Isitoshe, hapo sijagusia kabisa utawala Malikia Bilqis, hapo ndiyo utachoka zaidi, nakuwachuia wewe unipe historia ya Utawala wa Malkia Bilqis.

Hilo nilikuwekea nyekundu, hapana, si kweli kuwa mzaram0 akijifunza Kiarabu basi kishakuwa Mwarabu. Lugha ya kujifunza si ya asili yako, huwezi kuidai hiyo asili kama lugha si mama kwako.

Uarabu na Ubantu si makabila ni lugha, Waarabu wana makabila yao na Wabantu wana makabila yao. Soma ile post ya Makerere utanielewa tu.

Kwanini Waarabu wakaitwa Waarabu?

Maana ya Arabiya ni 'caravan" au msafara, "Arab" au Mwarabu maana yake ni mtu wa msafara na lugha yao ni Kiarabu, kwanini? nakuwachia na wewe unipe jibu. Nnakumbuka nilipokuwa shule ya msingi tukifundishwa kuhusa wahamahamaji, sijuwi unawajuwa ni akina nani hao?

Jee, maana ya Bantu ni nini?
 
Kwa kuangalia comments na aina ya watu wanaokipigia debe hiki kitabu, inatosha kusema ni cha kupuuzia kama stori za kariakoo Gerezani za mzee mmoja humu
 

Hapana, Zenjbar haimaanishi mtu mweusi Kiarabu. Pata darsa dogo:

"Zenj" linatokana na neno "Zinj" na Bar ni neno tulijualo kwa Kiswahili kama "bara".

Zanzibar ya visiwa vya Unguja na Pemba si pahala ambapo awali paliitwa Zinjibar na Waarabu, hawawezi kufanya kosa hilo, "bar" ni bara na Zanzibar ya sasa ni kisiwa. Upo hapo ulipo?

Jee, sasa unajuwa maana ya bar? jee hii "Zinj" maana yake nini? na hilo bara la Zinj lilikuwa wapi?

Majibu niliwahi kuyatowa zamani humuhumu JF wanaokumbuka watakusaidia.

Ukiniambia Sudan linatokana na neno "mtu mweusi" nnaweza kukubalia na sababu zipo, lakini sitaki kuingia huko kwa sasa, nnakupa kidokezo tu.
 

Hiyo nchi iliyoitwa na Waarabu "nchi ya weusi" ni ipi hiyo?

Kabla hujajibu soma post namba 204, kuna mtu kadokezea hilo pia lakini nimempa darsa dogo, sijuwi kama na wewe umemaanisha hilohilo au jingine?
 
Mzee, nimejibu upotoshaji wa Faiza kuhusu maana za maneno husika.

Vv

Yamo humu kwenye huu uzi hayo maneno? ni post yangu ipi uliyoijibu yenye huo "upotoshaji"? naomba niwekee au niambie tu ni post namba ngapi, tafadhali. Tusiandikie mate na wino upo.
 
Unazungumzia propaganda za udini wakati wewe ndie KINARA.
 

Umechanganya mambo mengi sana mpaka nnashindwa ku "concentrate", sasa kama hautaki kujuwa North na South na wanahistoria walioboobea wanatumia "terminology" hiyo itakuwa wewe huna haja ya kujuwa asili za watu bali unataka ubishi wa kijinga.

Hilo la Makabila ya kibantu kufika 1,000 si muhali hata yakifika 2,000 lakini Wabantu watabaki kuwa Wabantu na Watabaki kuwa Walikuja Afrika ya Mashariki.

Unajuwa maana ya Bantu?

Nnakuwekea hizo "proofs" usome mwenyewe ili usije ukauliza "source". Hakuna aliyezaliwa anajuwa kila kitu, tunasoma, tunajifunza, tunajuwa, unless uwe ni mjinga wa kuzaliwa ndiyo utakataa kusoma waanazuoni waliobobea fani zao na proofs zao, unaweza kuwapinga walichoandika ukaja na chako chenye mashiko zaidi lakini huwezi kuwacha kuwasoma waliyoyaandika watu wengine. Sidhani kama wewe uko huko.

Nnankushangaa sana unapoona kuwa ni kituko mimi kuweka links za maandiko ya wanahistoria ujisomee mwenyewe ili yakuingie.

Unajaribu kufanya "character assassination" ya kijinga. Hunipati huko.
 

Duh, maajabu hayatakoma humu JF! Yaani hizo adabu unazaodai kufundishwa Madras mnafundishwa kuwaheshimu watu wa dini yenu tu?

Kama mwafundishwa adab kwa ajili ya wote basi huyo Faiza unayemsifia kuwa na adab humfahamu na umepotoka sana, Faiza anakuwa na adab anapomjibu Muislam mwenzake, hilo nimegundua leo alipokuwa anajibizana na Mkangara; ukitaka kujua hilo fuatilia majibu ya Faiza kwa wengine ambao sio Waislamu wenzake. Pole Mzee kwa kutomfahamu Faiza.

Vv
 
Hivi wewe hauamini katika jihad? Jihad ni kufanya jitihada katika chochote ukifanyacho.

Hivi huna jitihada yoyote uifanyao katika maisha yako? au umeaminishwa kuwa jihad ni nini?








Vyamavingi,
Hapa tunazungumzia kitabu cha Prof. Ibrahim Noor hatuko kwenye
somo la jihad.

Ikiwa unataka kuzungumzia mada hiyo fungua uzi mpya kwenye
jukwaa husika.




Mzee, nimejibu upotoshaji wa Faiza kuhusu maana za maneno husika.

Vv




Yamo humu kwenye huu uzi hayo maneno? ni post yangu ipi uliyoijibu yenye huo "upotoshaji"? naomba niwekee au niambie tu ni post namba ngapi, tafadhali. Tusiandikie mate na wino upo.

Faiza, nimekundikia mtiririko mzima ili kukurahisishia; nikiandika nambari za post itakupotezea muda wa kutafuta. Hebu kanusha, au kuna mtu ametumia ID yako?

Vv
 
Kwa kuangalia comments na aina ya watu wanaokipigia debe hiki kitabu, inatosha kusema ni cha kupuuzia kama stori za kariakoo Gerezani za mzee mmoja humu

Kapwila...
Haikuwa rahisi kukipuuza kitabu changu.
Kimeingia katika Cambridge Journal of African History.

Ikiwa unaijua Cambridge University utaelewa.

Kinasomeshwa Northwestern University, Chicago Illinois, mabingwa
wa African History.

Na mwandishi akaalikwa Northwestern kufanya mhadhara.
Vipo vitabu vya kupuuza na viko vitabu havipuuziki.

Kitabu nakala ya Kiswahili tunakwenda toleo la nne na la Kiingereza
toleo la tatu.

Kapwila...
Vipo vitabu vya kupuuza na viko vitabu havipuuziki.
Kitabu hiki kimenifikisha mbali sana.

Angalia hapa Majlis jinsi kinavyochangamsha jamvi.

Stori za Gerezani na Kariakoo wakati wa kudai uhuru ungezisikia
wapi kama si kitabu hiki?

Ungelimjuaje Dossa "The Bank" aliyetoa gari yake kuipa TANU?

Ungelimjuaje Abdul "The Sweet" aliyemleta Earl Seaton, Japhet
Kirilo, Sheikh Hassan
bin Amir na Julius Nyerere New Street?

Unajua michango ya hawa watu walipofika New Street nini walifanya
kwa Tanganyika?

Vipo vitabu vya kupuuza na viko vitabu havipuuziki.
 

Vyamavingi,
Maalim Faiza anakusoma...
 
Huu mjadala ungenoga sana kama sio element za majigambo na kebehi.
Umahiri wa wengi una fichika.
Wenzenu hapa tunatafuta kujua.
Hiki kitabu kinapatikana online?

Haika,
Hiki kitabu hakipatikani "online."

Kinauzwa duka la vitabu la Ibn Hazm Media Centre Mtoro na Manyema na
Tanzania Publishing House (TPH), Samora Avenue.

Bei yake ni shs: 5000.00.
 


Nitafanyia utafiti madai yako juu ya waIraqw
 

Jee, una habari za Ufalme wa Kushi?
 

Kwanza kabisa, napenda kukurekebisha, huyo ni Mkandara na si "Mkangara", kwetu huku pwani, "kangara" ni jina la pombe ya kienyeji.

Pili, napenda ufahamu, tena ufahamu sana, kuwa Mkandara ni Muislam, tena ni Muislam kweli kweli na anaujuwa Uislam kuliko unavyofikiria. Namheshimu sana kwa hilo.

Tatu, napenda ufahamu, Mkandara ananijuwa sana, si leo, si jana, si kupitia JF tu. Anapajuwa kwetu.

Nne, napenda ufahamu, kaka yake Mkandara ndiye alimfundisha Mbowe disko ni nini, mpaka leo unamuona MBOWE ana Bilicanas ni sama na kaka'ke Mkandara.

Tano, napenda ufahamu, Waarabu wa Pemba wajuana kwa vilemba.

Sita, ntasubiri majibu yako mpaka kesho saa sita.

Do not judge the book by its cover.
 
Last edited by a moderator:

Kapwila...
Kuna kitu nimekiona nimeona nikurudie nikuonyeshe ili upate yakini
kuwa kitabu changu kilikuja na taarifa muhimu sana katika historia
ya uhuru wa Tanganyika.

Soma hapo chini:

Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu kuhusu:

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,
'' Minerva Press, London 1998.​

[TABLE="width: 615"]
[TR]
[TD]

''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary;
Alexander M. Tobias and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kapwila,
Huyu Alexander M. Tobias alifukuzwa chama kwa usaliti katika mkutano
wa kuunda TANU July 1954 kwa sababu alichukua majalada ya TAA
akawapa Special Branch.

Habari hizi alinipa marehemu Mzee Germano Pacha mmoja wa wale
waasisi 17 wa TANU.

Kapwila,
Bado unaamini kitabu hiki ni cha kupuuzwa?​


[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…