Kitabu: Maisha ya Malcom X

Kitabu: Maisha ya Malcom X

Mpaka hapa nimesoma na kutambua kuwa Malcom X pia amepitia Maisha ya kujirusha.

Nataka kusoma/kujua ni kwa namna gani amepigania haki na Uhuru wa mtu mweusi..

Ni imani simulizi itaendelea..
 
Malcolm x baadae alikosana na Elijah Mohammed...ngoja tuone kama alilielezea hili...
 
SURA YA 12

MWOKOZI


Wakati wa majira ya kuchipua ya mwaka 1952, niliiandikia familia yangu na Elijah Muhammad barua ya furaha kuwa
bodi ya parole ya jimbo la Massachusetts imepiga kura na kuridhia nitolewe gerezani. Hata hivyo sababu ya taratibu za kiserikali ilichukuwa miezi kadhaa kuachiliwa, hasa kupanga
taratibu za kuwa chini ya uangalizi wa kaka yangu Wilfred
huko Detrioit baada ya kuachiliwa. Wakati huo Wilfred
alikuwa akifanya kazi kwenye duka la samani la Myahudi
fulani. Alifanikiwa kumshawishi bosi wake huyo kunipatia
kazi mara nitakapoachiliwa.
Nilipata taarifa nikiwa gerezani kuwa Shorty naye alikuwa
kwenye mikakati ya kuachiliwa. Lakini kikwazo ilikuwa hana
mdhamini mwenye sifa. (Baadaye nilikuja fahamu kuwa
Shorty alijifunza kuandika muziki alipokuwa gerezani, na
hata alifanikiwa kuandika muziki fulani, naufahamu mmoja
unaitwa “The Bastille Concerto.”)
Kwenda kwangu Detroit badala ya Harlem au Boston
kulitokana na ushawishi wa familia yangu kupitia barua. Hasa
dada yangu, Hilda alikuwa amesisitiza kuwa nina mengi ya
kujifunza japo ninahisi kuwa nayafahamu vyema mafundisho
ya Elijah Muhammad. Hivyo niende na kuwa mshiriki wa
Hekalu la Waislamu.
Ulikuwa ni mwezi wa nane nilipoachiliwa, nilipewa
mawaidha, suti ya Li’l Abner na pesa kidogo. Nilitoka getini na
sikuangalia nyuma.
Sehemu ya kwanza kwenda ni kwenye bafu la kituruki.
Nilioga na kujihisi ugerezani ukinitoka. Nililala kwa Ella siku
moja, naye alikubaliana na suala la mimi kwenda Detroit
kuanza upya. Alisema kuwa polisi wa huko hawatakuwa na
habari nami—si kwamba niende kujumuika na Waislamu
wenzangu ambao Ella hakuwa hata na habari nao. Hilda na
Reginald walijaribu kumshawishi Ella. Lakini Ella na ukichwa
ngumu wake hakukubaliana nao hata kidogo. Alisema kwa
maoni yake kila mtu anaweza kuwa atakavyo yeye, Mlokole,
Msabato, au chochote kile, na kuwa yeye kamwe hawezi kuwa
Muislamu.
Hilda alinipatie pesa asubuhi iliyofuata. Kabla sijaondoka
nilitoka na kwenda kununua vitu vitatu. Nilinunua miwani
mizuri kulinganisha na ile niliyopewa gerezani; pia
nikanunua sanduku la safari na saa.
Nimekuwa nikifikiria kuwa nilikuwa najiandaa na jinsi
maisha yangu yatakavyokuwa bila ya mimi mwenyewe kujua.
Hivyo vitu vitatu ndivyo nilivyovitumia zaidi kuliko vingine
vyote. Miwani ilinisaidia tatizo langu loa macho nililopata
kutokana na kusoma sana kwenye mwanga hafifu kule
gerezani. Ninasafiri sana kiasi kwamba mke wangu huandaa
sanduku lingine la safari likiwa tayari, nikiwa na safari ni
kubeba tu. Na huwezi kutana na mtu anayejali muda zaidi
yangu. Ninaishi kwa muongozo wa saa, na hata
ninapoendesha saa ndiyo inaniongoza na si kipima mwendo.
Kwangu muda ni muhimu kuliko umbali.
Nilipanda basi hadi Detroit. Duka la samani ambalo kaka
yangu Wilfred alifanya kazi lilikuwa katikati ya makazi,
kwenye eneo la maghetto ya watu weusi; naonelea ni vyema
nisilitaje duka hilo kama ninataka kuongelea jinsi walivyo
watapeli watu weusi. Wilfred alinitambulisha kwa Myahudi
aliyemiliki duka lile, na nilianza kazi kama makubaliano.
Nilifanya kazi kama muuzaji.
Matangazo ya “kukopa mali bila kianzio” yaliwaleta watu
weusi dukani pale kama karatasi ya kuwanasa nzi. Ilisikitisha
kwa jinsi walivyolipa mara tatu hadi nne ya bei halisi ya
samani. Zilikuwa ni zile samani mbovumbovu ambazo hata
leo unaweza kuziona kwenye maduka ya samani yaliyopo
maeneo ya magetto ya watu weusi. Niliona mikono
iliyokomaa kwa kazi ikitia saini kwenye mkataba,
kukubaliana na wizi wa mchana kutokana na riba yake kubwa.
Mkataba wenyewe uliandikwa kwa maandishi madogo sana
kiasi kwamba haikuwa rahisi kuusoma.
Nilijionea kihalisi kichekesho kilichoandikwa kwenye
jarida la Jet wakati wa kampeni za urais za mwaka 1964,
kichekesho chenyewe kilikuwa kimezungumzwa mahali
fulani na seneta Barry Goldwater. Kilisema kuwa Myahudi,
Mzungu na mtu Mweusi waliambiwa kila mmoja aombe kitu
kimoja chochote anachotaka. Mzungu aliomba hisa; mtu
mweusi aliomba pesa nyingi; na Myahudi aliomba vito feki na
anuani ya yule mtu mweusi.
Miaka yangu yote mtaani nilikuwa nimeona unyonyaji
lakini hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuuelewa vyema.
Nilijionea watu weusi wakijifunga kwenye mitego ya
kiuchumi ya mzungu ambaye kila jioni alienda nyumbani na
kifurushi cha pesa kutoka maghettoni. Nilishuhudia badala ya
pesa kumsaidia mtu mweusi, zilienda kuwatajirisha
wafanyabiashara wa kizungu ambao waliishi maeneo ya peke
yao, maeneo ambayo mtu mweusi hakutakiwa kupatikana
isipokuwa awe anafanya kazi nyumbani kwa mzungu.
Wilfred alinikaribisha kuishi naye nami nilishukuru sana.
Maisha ya kwenye familia yake yalikuwa ni tiba ya yale ya
kufungiwa gerezani. Nafikiri jambo kama hili linaweza mgusa
sana mfungwa yeyote aliyetoka kuachiliwa. Maisha kwenye
nyumba hii ya Kiislamu yalinifanya mara nyingi nipige
magoti na kumsifu Allah. Barua nilizoandikiwa na familia
yangu nilipokuwa gerezani zilielezea taratibu za maisha ya
Kiislamu nyumbani, lakini ili kuyaelewa vyema maisha hayo
mtu anatakiwa kuyaishi. Kaka yangu alinieleza kwa upole na
subira kila tendo, linavyopaswa kufanywa na umuhimu wake.
Hakukuwa na zile vurugu za asubuhi ambazo huwepo
kwenye nyumba nyingi. Wilfred—baba, mlinzi na mtunza
familia alikuwa ndiye wa kwanza kuamka. “Baba anaandaa
njia kwa ajili ya familia yake,” alisema. Kisha akatawadha
nami nikafuata. Akafuata Ruth mke wake na mwishowe
watoto wao, kulikuwa na utaratibu mzuri kabisa katika
matumizi ya maliwato.
“kwa jina la Allah nafanya udhu”walisema Waislamu
kabla ya kuosha mkono wa kulia, kisha wa kushoto. Meno
yalisuguliwa vizuri na kisha mdomo kusuzwa mara tatu.
Matundu ya pua yalisuzwa pia mara tatu. Kuoga kuliuweka
tayari mwili wote kwa ajili ya sala.
Kila mwanafamilia, hata watoto, walipokutana
walisalimiana “As-Salaam-Alaikum”(salamu ya kiarabu
ikimaanisha amani iwe nawe). “Wa-alaikum Salaam”(amani
iwe nawe pia) alijibu aliyesalimiwa. Muislamu husema
kichwani mwake tena na tena, “Allahu-Akbar, Allahu-Akbar,
(Mungu ni mkuu)
Wilfred alitandika zulia wakati familia yote ikifanya udhu.
Niliambiwa kuwa familia ya Kiislamu huswali kwa kuangalia
jua “Waislamu hawaabudu jua. Tunasali tukitazama
mashariki ili kuwa katika umoja na ndugu na dada zetu
wengine wa Kiislamu 725 milioni duniani kote.
Familia nzima ilijipanga ikitazama mashariki. Kwa pamoja
tulivua ndala na kusimama kwenye zulia la sala.
Kifungua kinywa hakikuwa chakula kigumu, tulipata juisi
au kahawa kisha mimi na Wilfred tulikwenda kazini. Kazini
hapo ilipofika saa sita mchana, na tena saa tisa mchana; bila
kuonekana na wengine pale dukani, tulijisafisha mikono, uso
na mdomo na kisha tukaali kimyakimya. Watoto wa Kiislamu
nao walifanya hivyohivyo huko shuleni. Nao wake na mama
wa Kiislamu waliacha kazi zao na kuungana na Waislamu
wengine milioni 725 katika kuwasiliana na Mungu.
 
Asante sana mkuu.

Nahiai kuna mwndelezo wa part hii kwani yaonyesha kama kuna kitu kimepungua.
Vinginevyo ubarikiwe sana.
 
Asante sana mkuu.

Nahiai kuna mwndelezo wa part hii kwani yaonyesha kama kuna kitu kimepungua.
Vinginevyo ubarikiwe sana.
Pia unaweza install hiyo app kutoka playstore na kuendelea kusoma. Unapata free trial ya siku tatu.
Screenshot_20231219-145945.png
 
Sura ya 12 inaendelea.

Siku za Jumatano, Ijumaa na Jumapili zilikuwa siku za mikutano kwenye Hekalu la Detroit lililoitwa Hekalu Namba Moja, lilikuwa ni dogo ukilinganisha na mengine. Karibu na hekalu hilo ambalo kihalisi lilikuwa tu ni fremu ya duka tu, kulikuwa na machinjio tatu za nguruwe. Kelele za nguruwe wakichinjwa zilisikika wakati wa mikutano yetu ya Jumatano na Ijumaa. Naelezea tu jinsi Waislamu tulivyokuwa miaka ya 1950 mwanzoni. Hekalu Namba Moja lilikuwa kwenye nyumba namba 1470 katika mtaa wa Frederick. Nadhani Hekalu la kwanza kuanzishwa, lilianzishwa mwaka 1931 na W. D. Fard huko Detroit, Michigan. Sijawahi ona Wakristo weusi wakijiendesha kama walivyofanya Waislamu, iwe mmoja mmoja au familia nzima. Wanaume walivalia nadhifu.
Wanawake walivaa magauni, bila kupaka vipodozi na walifunika vichwa vyao kwa vitambaa. Watoto walikuwa ni wenye adabu, si kwa watu wazima tu bali hata kwa watoto wenzao. Sikuwhi kuota kuona kitu kama kile kwa watu weusi, watu waliojifunza kujivunia weusi wao, waliojifunza kupenda weusi wengine badala ya kuwaonea wivu na kuwashuku. Niliguswa sana na jinsi wanaume weusi walivyosalimiana kwa mikono huku wakitabasamu, wakifurahi kukutana tena. Wanawake wa Kiislamu, waliiolewa na waseja walipewa heshima ambayo sijawahi ona watu weusi wakiwapa wanawake wao, na hilo lilinistaajabisha sana. Salamu zote zilikuwa za bashasha na zilizojaa heshima: “Ndugu”. . . “Dada”. . . “bibi”. . . “Bwana.” Hata watoto walitumia maneno haya walipoongea na watoto wenzao. Ilipendeza sana. Lemuel Hassan alikuwa ndiye Imam wa Hekalu Namba Moja. “As-Salaikum” alitusalimia. “Wa-Salaikum” tulijibu. Imam Lemuel alisimama karibu na ubao. Juu ya ubao kulikuwa kumechorwa kwa rangi—upande mmoja ilichorwa Bendera ya Marekani na chini yake maneno “Utumwa, Mateso na Kifo,” yakifuatiwa na neno “Ukristo” pamoja na alama ya Msalaba. Pembeni ya Msalaba kulikuwa na picha ya mtu mweusi akiwa amenyongwa mtini. Upande mwingine ilichorwa tuliyofundishwa kuwa ni bendera ya Uislamu, mwezi na nyota na maneno “Uislamu: Uhuru, haki, Usawa,” na chini yake “Nani ataokoka vita ya Armageddon?” Imam Lemuel alifundisha mafundisho ya Elijah Muhammad kwa zaidi ya saa moja. Nilisikiliza kwa makini nikimeza kila neno na ishara za Imam Lemuel. Mara kwa mara alifafanua zaidi kwa kuandika maneno muhimu kwa chaki ubaoni. Niliona ni ajabu kwa hekalu letu dogo kuwa na viti wazi. Nilimwambia kaka yangu Wilfred kuwa hakutakiwi kuwa na viti wazi wakati mitaa imejaa ndugu na dada zetu weusi walichotwa akili, wakinywa, kucheza dansi, kutukana, kupigana na kutumia madawa—mambo ambayo bwana Elijah
Muhammad ametufundisha kuwa yanachangia kuwafanya watu weusi waendelee kuwa chini ya mzungu. Kutokana na nilivyoona, mtazamo juu ya kutafuta waumini wapya hekaluni pale haukuwa chanya kabisa. Ilikuwa kwamba “Allah atatuletea” Waislamu wengine. Binafsi niliwaza kuwa Allah atakuwa na mtazamo kuwasaidia zaidi wale wanaojisaidia. Nimeishi kwenye maeneo ya maghetto kwa miaka mingi; niliwafahamu vyema watu weusi walioishi maeneo hayo. Iwe ni Harlem au Detroit, hawana tofauti. Nilisema kuwa sikubaliani na mtazamo huo, na kwamba tunatakiwa kutoka kwenda mtaani na kuwaleta wengi kwenye Uislamu. Kama unavyojua, maisha yangu yote nilikuwa mwanaharakati, sikuwa mtu wa subira. Kaka yangu Wilfred alinishauri kuwa na subira. Niliweza kuwa na subira kirahisi kwa sababu nilitarajia kuonana na mtu aliyeitwa “Mtume,” Elijah Muhammad mwenyewe.

Leo hii nina miadi mingi ya kukutana na watu maarufu duniani, na baadhi yao ni viongozi wa nchi. Lakini sijawahi kuwa na shauku ya kukutana na mtu kama Jumapili ile ya kuamkia Sikukuu ya wafanyakazi wa Marekani ya mwaka 1952. Waislamu wa Detroit walikuwa na safari, nafikiri yalikuwa kama magari kumi—kwenda Chicago kwenye Hekalu Namba Mbili, kumsikiliza Elijah Muhammad. Toka utoto sijawahi kuwa na shangwe kama tulivyokuwa tukiondoka na gari ya Wilfred kuelekea Chicago. Kwenye makusanyiko makubwa ya Waislamu nilikuja kuona, kusikia na makumi elfu ya watu weusi wakishangilia, lakini mchana
wa Jumapili ile mahekalu yetu mawili madogo yalipokusanyika-labda Waislamu mia mbili hivi, Wachicago wakitusalimu na kutukaribisha wa kutoka Detroit, nilipatwa na hisia ambazo sijawahi kuzipata tena. Akili yangu haikujiandaa kabisa kukutana ana kwa ana na Elijah Muhammad. Alipanda jukwaani akitokea nyuma ya Hekalu. Mtu mwenye umbo dogo, rangi ya kahawia na sura ya upole ambaye nilizoea kumuona kwenye picha alikuwa anatembea kuelekea jukwaani huku akiwa amezungukwa na Fruit of Islam(walinzi wa matunda ya Uislamu.) Ukiwalinganisha nao, Mtume alionekana dhaifu na mduchu.

Wote, yeye na walinzi walivaa suti nyeusi, mashati meupe na tai za kipepeo. Mtume alikuwa amevaa baraghashia iliyopambwa kwa dhahabu. Nilimkodolea macho mtu yule mkuu aliyetumia muda wake kuniandikia barua nilipokuwa mfungwa ambaye hakumfahamu hata kidogo. Mtu ambaye niliambiwa kuwa ametumia miaka yake akitaabika na kujitolea kutuongoza watu weusi kwa sababu anatupenda sana. Niliposikia sauti yake nilikaa kwa kuinamia mbele na kusikiliza kwa makini(Najaribu kukumbuka alichosema Elijah Muhammad kutokana na nilivyokuja kumsikia akiongea zaidi ya mara mia) “Kwa miaka ishirini na moja iliyopita sijaacha hata siku moja kusimama na kuwahubiria, nilipokuwa huru na hata nilipokuwa kifungoni. Nilikuwa kifungoni kwa miaka mitatu na nusu na pia zaidi ya mwaka mmoja kwenye jela ya jiji kwa
sababu ya kuhubiri kweli hii. Pia nilinyimwa nafasi ya kuonyesha upendo wa baba kwa miaka saba sababu ya kuwakimbia maadui wa neno hili na ufunuo wa Mungu uwapao uhai na kuwafanya kuwa sawa na mataifa yote huru, yaliyostaarabika na watu wa dunia hii kwa ujumla . . . . “ Elijah Muhammad aliongea jinsi ambavyo kwa karne nyingi kwenye nyika hizi za Amerika ya Kaskazini, “Shetani mwenye macho ya bluu-mzungu” alivyomchota akili mtu anayeitwa “Negro.” Alituambia jinsi ambavyo mtu mweusi wa Marekani amekufa “kimaadili, kiakili na kiroho.” Sababu ya kuchotwa huko akili. Alizungumza jinsi ambavyo mtu mweusi ndiye mtu wa asili aliyenyakuliwa kutoka nyumbani kwake na kuvuliwa lugha yake, utamaduni wake, muundo wake wa familia, jina lake la ukoo mpaka mtu mweusi wa Marekani aliposhindwa kujitambua yeye ni nani.

Alituambia na kuonyesha jinsi ambavyo mafundisho yake juu ya ukweli wa mtu mweusi yanamuinua mtu mweusi kutoka daraja la chini kabisa la kijamii katika jamii ya mzungu na kumuweka alipokuwa mwanzo, juu ya ustaarabu wote. Mwisho wa hotuba alipumzika kidogo kuvuta pumzi, kisha akaniita kwa jina langu. Nilikuwa kama nimepigwa na umeme. Aliniomba nisimame. Aliuambia mkusanyiko ule kuwa nilikuwa nimetoka gerezani karibuni tu. alizungumza jinsi nilivyokuwa “Imara” wakati nipo gerezani. Alisema, “kila siku kwa miaka kadhaa,
ndugu Malcom amekuwa akiniandikia barua kutoka gerezani. Nami nilimuandikia barua mara nyingi kadri nilivyoweza.” Nilisimama pale huku nikihisi macho ya Waislamu mia mbili yakinitazama. Nikasikia akinitolea mfano. Mungu alipojisifu juu ya uaminifu wa Ayubu, alisema Elijah Muhammad, Shetani alimjibu kuwa wigo wa ulinzi wake kumzunguka Ayubu ndiyo unamfanya awe muaminifu. “Ondoa ulinzi huo,” Shetani alimwambia Mungu, “nami nitamfanya Ayubu akutukane waziwazi.” Shetani anaweza kudai kuwa nilipokuwa nimezungukwa na wigo gerezani nilijidai tu kuwa Muislamu, alisema Elijah Muhammad, kisha akaendelea kuwa sasa nipo uraiani Shetani anadai kuwa nitarudia maisha yangu ya kunywa pombe, kuvuta sigara, kutumia madawa ya kulevya na uhalifu. “Basi sasa wigo uliomzunguka ndugu yetu Malcom umeondolewa, tutajionea wenyewe atakavyoenenda.” Alisema bwana Elijah Muhammad. “nina imani ataendelea kuwa muaminifu.” Na Allah alinibariki kuendelea kuwa imara na muaminifu katika imani yangu ya Kiislamu pamoja na majaribu mengi niliyokutana nayo. Na hata ulipotokea mgogoro kati yangu na Elijah Muhammad, nilimwambia bila unafiki wowote kuwa bado nina imani naye kuliko hata yeye mwenyewe anavyojiamini. Leo siko pamoja na bwana Muhammad sababu tu ya husda na wivu.Nilikuwa na imani na Elijah Muhammad kuliko ninavyoweza kuwa na imani na mtu yeyote duniani hapa.

Utakuwa unakumbuka nilisema kuwa nilipokuwa gerezani bwana Muhammad alifikia nyumbani kwa kaka yangu Wilfred alipotembelea Hekalu Namba Moja huko Detroit. Waislamu wengi wanasema huwezi kumtendea Elijah Muhammad zaidi ya anavyoweza kukutendea, basi Jumapili hiyo alitulika familia nzima pamoja na Imam Lemuel Hassan kupata chakula cha jioni kwenye nyumba yake mpya. Bwana Muhammad alisema kuwa watoto na wafuasi wake walikuwa wamemsisitiza ahamie kwenye nyumba hii kubwa. Ilikuwa nyumba nzuri na kubwa ya vyumba kumi na nane. Ilikuwa namba 4847 katika barabara ya Woodlawn huko Chicago. Nadhani ni juma lilelile ndiyo walikuwa wamehamia. Tulipofika bwana Muhammad alituonyesha eneo alilokuwa anaendelea kupaka rangi. Ilinibidi kujizuia, vingenevyo ningekimbia kuleta kiti ili Mtume wa Allah aketi, lakini kumbe naye pia alikuwa anatuwazia sisi. Tulitegemea kusikia busara zake wakati wa chakula lakini badala yake alitusisitiza tuongee. Nilikaa pale nikitafakari jinsi ambavyo hekalu letu la Detroit limekaa tu likisubiri Allah kuwaleta waumini, na zaidi-juu ya mamilioni ya watu Weusi kote Marekani, watu ambao hawajawahi kusikia mafundisho yanayoweza kumuamsha na kumchochea mtu mweusi . . . basi pale kwenye meza ya bwana Muhammad nikapata ujasiri wa kuongea. Siku zote nimekuwa mtu wa kuongea kwa uwazi. Kulipokuwa na ukimya nilimuuliza bwana Muhammad kuwa Hekalu letu Namba Moja kule Detroit lilitakiwa kuwa na Waislamu wangapi. Alinijibu “Maelfu.” Nilimjibu ndiyo, Kisha nikamuuliza “Unafikiri ni njia gani nzuri ya kupata hao maelfu?” “Wafuate vijana,” alisema. “Baada ya kuwapata, wazee watajiunga kwa kuona aibu.” Nikadhamiria akilini mwangu kuwa tutafuata ushauri huo. Tuliporudi Detroit niliongea na kaka yangu Wilfred. Nilijitolea kumsaidia kazi Imam Lemuel Hassan. Naye aliunga mkono wazo langu kuwa tutumie njia ya bwana Muhammad katika kupata waumini wapya. Kuanzia siku hiyo, kila siku jioni baada ya kutoka kazini nilienda kufanya kile ambacho Waislamu wakati huo tuliita “Uvuvi.” Nilijua lugha na mawazo ya watu walioishi maeneo ya maghetto: “My man, let me pull your coat to something-” Nilikuwa nimeshatuma maombi yangu na nikapokea “X” yangu kutoka Chicago. “X” ya Waislamu inawakilisha jina lake halisi la ukoo wake wa Kiafrika ambalo hatakuja kulijua. Kwangu “X” ilikuwa mbadala wa jina la Little ambalo mmiliki watumwa aliwapachika babu zangu. Kupata kwangu “X” kulimaanisha maisha yangu yote kwenye Taifa la Kiislamu nitajulikana kama Malcom X. Bwana Muhammad alifundisha kwamba tutatumia hizo “X” mpaka Mungu mwenyewe atakaporudi na kutupatia majina matakatifu kwa mdomo wake mwenyewe. Nilienda kutafuta waumini kwenye vibanda vya kuchezea pool, baa na vichochoro vya maeneo ya maghetto ya Detroit. Huko niliwapata ndugu zangu weusi wakiwa masikini, wajinga, waliochotwa akili, viziwi, vipofu na mbumbumbu wa kiakili, kiroho na kimaadili kiasi kwamba hawakuweza kuitikia. Ilinichukiza kuona ni mara chache sana watu walionyesha udadisi hata ule kidogo tu juu mafundisho yenye lengo la kumuamsha mtu mweusi. Wachache walioonyesha udadisi niliwabembeleza sana wahudhurie mikutano kwenye Hekalu Namba Moja, lakini kati ya wale waliokubali kuja— waliokuja hawakufika hata nusu. Polepole watu wakaanza kupendezwa. Kila mwezi magari kadhaa yaliongezeka kwenye msafara wetu wa kuelekea kwenye Hekalu Namba Mbili huko Chicago. Lakini hata baada ya kumsikia na kumuona Elijah Muhammad, ni wachache tu waliandika barua kwa Elijah Muhammad kuomba kuwa wanachama wa Taifa la Kiislamu. Lakini baada ya miezi michache ya kupambana Hekalu letu likawa na washirika mara tatu ya idadi ya mwanzo. Jambo hilo lilimfurahisha sana bwana Elijah Muhammad hadi akafanya ziara ya heshima kuja kututembelea. Bwana Muhammad alinisifa sana baada ya Imam Lemuel Hassan kumueleza jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Uislamu. Sasa msafara wetu ukawa umekuwa mkubwa. Nakumbuka kuwa tulienda Chicago ndani ya magari ishirini na matano. Na kila tulipoenda tuliheshimishwa kwa chakula katika nyumba ya Elijah Muhammad. Alipendezwa sana na uwezo wangu, niliweza kuona hilo kwa jinsi alivyoongea. Nami ni kama nilimuabudu.

Mwaka 1953 niliacha kazi kwenye duka la samani. Nilipata kazi yenye mshahara mzuri kidogo kwenye kiwanda cha Gar Wood huko huko Detroit. Kiwanda hicho kilitengeneza mabodi ya magari ya taka. Kazi yangu ilikuwa kusafisha baada ya wachomeleaji kumaliza kazi yao. Wakati wa chakula bwana Muhammad alikuwa anasema mahitaji yake makubwa ni kupata vijana wengi zaidi, vijana walio tayari kufanya kazi kwa bidii wawezavyo ili kuchukua majukumu ya maimam wake. Alisema kuwa mafundisho yanatakiwa kupelekwa mbali kuliko yalipofika, na kunahitajika kufungua mahekalu kwenye majiji mengine. Sikuwahi kufikiria kabisa kuwa nitakuwa mhubiri. Sikuwa hisi hata kidogo kuwa nina vigezo vya kumuwakilisha bwana Muhammad. Kama kuna mtu angeniambia niwe mhubiri ningestaajabu sana na kumwambia kuwa nina furaha kumtumikia bwana Muhammad katika nafasi ya chini kabisa. Sijui kama lilikuwa ni pendekezo la bwana Muhammad au ni mhubiri wa Hekalu namba moja, Lemuel Hassan ndiye alieamua niwahubirie ndugu na dada hekaluni mwetu. Nakumbuka nilitoa ushahidi jinsi mafundisho ya Elijah Muhammad yalivyonitendea: “Kama nikiwaambia maisha maisha niliyoishi hamtaniamini. . . . ninapomuongelea mzungu simuongelei mtu nisiyemjua. . . .” Muda mfupi baada ya hapo, Imam Lemuel Hassan akanitaka kuwahutubia ndugu na dada kwa hotuba ya bila kujiandaa. Nilisita na sikuwa najiamini, lakini nilijipa moyo kuwa nimewahi shiriki kwenye mijadala kule gerezani hivyo nikajitahidi kadri nilivyoweza. (Sikumbuki nilichosema lakini nakumbuka kuwa mwanzoni mada yangu kuu ilikuwa juu ya Ukristo na madhira ya utumwa, mada ambazo nilihisi ninazielewa vya kutosha kutokana na kujisomea gerezani) “Ndugu na dada zangu, dini ya mzungu aliyetufanya watumwa, yaani Ukristo, inafundisha watu weusi wa huku Amerika Kaskazini kuwa tukifa tutaota mabawa na kupaa mawinguni ambako Mungu ametuandalia makao yaitwayo Mbinguni. Huu ndiyo Ukristo wa mzungu unaotumika kutuchota akili sisi watu weusi. Tumeukubali! Tumeupenda! Tumeuamini! Na tumeuishi, lakini tukiwa tunaendelea kufanya hivyo, kwa maslahi yake; huyu shetani mwenye macho ya bluu ameugeuza ukristo huo ili aweze kutukandamiza . . . kufanya macho yetu yaendelee kuangalia keki kutoka angani na mbingu inayokuja . . . wakati yeye akifurahia mbingu yake hapa hapa duniani . . . kwenye maisha haya haya. Leo hii nahutubia mbele ya maelfu ya Waislamu, na nawafikia mamilioni wengine kupitia redio na luninga, lakini kwa hakika sipati hisia kama zile nilizopata kwa kuhutubia Waislamu wale sabini na tano au mia moja hivi pamoja na baadhi ya wageni wachache, wakiwa wamekaa pale hekaluni huku vilio vya nguruwe kutoka machinjioni vikisikika. Wakati wa majira ya joto ya mwaka 1953 niliwekwa kuwa Imam msaidizi wa Hekalu Namba Moja la Detroit—sifa zote zimuendee Allah.
Kila siku baada ya kazi nilienda kwenye maeneo ya maghetto ya watu weusi kufanya uvuvi. Niliwaona ndugu na dada zangu ambao shetani wa kizungu alikuwa amewachota akili. Nywele zao zilikuwa kama zangu zilivyokuwa kwa miaka mingi, zimelainika kwa kuwekwa dawa—zimenyooka kama za mzungu. Mara kwa mara mafundisho ya bwana Muhammad yalipingwa na hata kudhihakiwa . . . “Hebu niondokee, umewehuka!” Wakati mwingine kichwa changu kiliwaka kwa hasira na masikitiko kwa ajili ya ndugu zangu weusi waliokuwa vipofu. Nilisubiria kwa hamu sana kupewa nafasi nyingine ya kuongea kutoka kwa Imam Lemuel Hassan. “Ndugu na dada zangu, hatukushusha nanga kwenye jiwe la Plymouth—jiwe la Plymouth ndilo lililotushukia!”. . . ‘Fanya kila uwezalo kusaidia kazi ya Mtume Elijah Muhammad kwa watu weusi . . . siku zote mzungu ametutawala kwa kutufanya tumkimbile kumuomba, ‘tafadhali bwana, tafadhali mzungu, bosi utanidondoshea makombo mengine kutoka meza yako iliyojaa utajiri. . . .’ ‘Ndugu zangu na dada zangu weusi! Tunaposema weusi tunamaanisha wote wasio wazungu. Ndugu na dada hebu angalieni ngozi zenu! Sote ni weusi mbele ya mzungu lakini tuna rangi tofautitofauti elfu kidogo. Geuka na mtazame mwenzako! Una aina gani ya weusi wa Kiafrika uliochafuliwa na mzungu? mnaniona mimi, mtaani walizoea kuniita Detroit Red. Ndiyo! Ndiyo, shetani mbakaji mwenye nywele nyekundu ndiye alikuwa babu yangu! Wala si zamani, Baba wa mama yangu. Mama yangu hakupenda kuongelea hilo na huwezi mlaumu. Alisema hajawahi kumuona baba yake na alikuwa akishukuru kwa hilo, nami namuunga mkono. Iwapo ningeweza kutoa damu ya babu yangu huyo inayochafua mwili wangu na rangi yangu ningefanya hivyo! Sababu nachukia kila tone la damu ya mbakaji yule iliyomo ndani yangu! ‘Na hili si kwangu tu, limetokea kwetu sote! Tafakari kuhusu wakati wa utumwa, haikuwa rahisi kwa bibi na nyanya zetu kuepuka wabakaji wa kizungu waliowamiliki.

Mbakaji huyo aliyemtoa uanaume mwanaume mweusi kwa vitisho . . . na kumjaza hofu kiasi kwamba mpaka leo hii mwanaume mweusi anaishi akimuogopa mzungu siku zote. Na hata leo anaishi chini ya ukandamizaji wake. ‘Fikiria—fikiria juu ya mwanaume mweusi akiwa amejawa na uoga na hofu , akisikiliza kilio cha mke wake, mama yake , binti yake akibakwa zizini, jikoni na vichakani. Fikirini hilo ndugu na dada zangu! Fikiria kusikia mke, mama na binti yako akibakwa! Nawe ukiwa umejazwa hofu na mbakaji huyo kiasi kwamba huwezi kufanya chochote. Kisha watoto waliozaliwa akawaita majina mabaya kama mulatto, quadroon, octoroon na majina mengine mabaya anayotuita pale asipotuita Nigger “Geuka na muangalie mwenzako, na fikiria kuhusu jambo hili. Sote rangi zetu zimechafuliwa lakini shetani huyu bado anategemea wahanga wake tumpende!
Nilikuwa nikikabwa na jazba kiasi kwamba nyakati nyingine nilitembea mitaani hadi usiku sana. Wakati mwingine nilikuwa siongei na mtu yoyote kwa saa kadhaa, nakaa kimya nikitafakari mambo ambayo mzungu amewafanyia watu wetu hapa Marekani.

****​
 
Sura ya 12 inaendelea

Siku moja msimamizi wa kiwanda cha Gar Wood nilikofanya kazi alinifuata huku akiwa na wasiwasi sana. Alisema kuwa kuna mtu yupo ofisini amekuja kuniona. Mzungu niliyemkuta pale alisema, “Nimetoka F.B.I” Alifungua kitambulisho chake—vile wanavyofunguaga ili kukutisha. Aliniambia nimfuate. Hakusema kwa nini. Nilimfuata hadi ofisini kwao. Walitaka kujua kwa nini sijajiandikisha jeshini kwa ajili ya vita ya Korea? “Nimetoka gerezani karibuni,” nilisema. “Sikujua kama mnachukua wenye historia ya kufungwa.” Kweli waliamini kuwa ninafikiri kiukweli kuwa waliowahi kufungwa hawapaswi kujiandikisha. Waliuliza maswali mengi. Nilishukuru hawakuniuliza iwapo nilikuwa na nia ya kuvaa sare za mzungu, sikuwa na nia hiyo. Walidhania tu kuwa ningependa kuzivaa. Waliniambia kuwa hawatanifunga kwa kushindwa kujiandikisha, na kuwa watanipa muda lakini ninapaswa kujiandikisha haraka iwezekanavyo. Basi nilitoka hapo na kwenda moja kwa moja wanakoandikisha. Waliponipatia fomu za kujaza, panapohusika dini nilijaza kuwa mimi ni Muislamu na kwamba dhamira yangu hainiruhusu kushiriki vita.

Nilirudisha fomu ile. Shetani yule mwenye umri wa makamo alinikata jicho kisha akainuka na kuelekea ofisi nyingine, bila shaka kuongea na mkuu wake. Baada ya muda kidogo alirudi na kuniashiria niingie ofisi ile. Nakumbuka kulikuwa na shetani watatu wazee. Wote walikuwa na muonekano uliosema “Mnigger msumbufu” nami nikawaangalia kwa uso wa “Shetani wa kizungu” bila kupepesa macho. Waliniuliza natumia vigezo gani kudai kuwa Uislamu ndiyo dini yangu. Niliwaambia kuwa Elijah Muhammad ni mtume wa Allah, na wote wanaomfuata bwana Muhammad katika Marekani ni Waislamu. Nilifahamu vyema kuwa walishasikia hili kutoka kwa ndugu wengine wa Hekalu Namba Moja waliofika kabla yangu. Waliniuliza iwapo nafahamu “Kukataa utumishi jeshini sababu ya dhamira” kunamaanisha nini. Niliwaambia kuwa mzungu anaponiambia niende mahali fulani kupigana na hata kufa ili kulinda namna ambavyo mzungu anamtendea mtu mweusi hapa marekani, basi dhamira yangu inakataa. Waliniambia kuwa suala langu litasubiri uamuzi. Lakini bado nilifanyiwa vipimo vya mwili na kupewa kadi iliyoonyesha daraja nililowekwa. Hiyo ilikuwa mwaka 1953, sikusikia tena kutoka kwao kwa miaka saba iliyofuatia, hapo ndipo nilipopokea kadi nyingine kwa njia ya posta. Huwa natembea nayo, hii hapa kadi namba 20 219 25 1377, ilitolewa tarehe 21/11/1960. Inasema “daraja 5-A,” sijui inamaanisha nini. Nyuma ya kadi iliandikwa “Michigan Local Board No. 19, Wayne County, 3604 South Wayne Road, Wayne, Michigan.”

***
Kila mara nilipoongea Hekaluni pale sauti yangu ilikwaruza sababu ya hotuba iliyopita. Koo langu lilichukua muda mrefu sana kuzoea hali ile. ‘Unafahamu kwa nini mzungu anakuchukia? Ni kwa sababu kila anapoona sura yako, anakuwa kama anatazama uhalifu wake kwenye kioo— na dhamira yake inamsuta kiasi kwamba hawezi kuvumilia! Kila mzungu wa Marekani anapokutana na mtu mweusi anatakiwa kupiga magoti na kusema “samahani, samahani sana kwa watu wa jamii yangu kuwatendea wa jamii yako uovu mbaya sana katika historia; utanipa nafasi ya kutubu? Lakini nyinyi ndugu na dada mnatarajia mzungu atafanya hivyo? Hapana, mnamfahamu vyema! Na kwa nini hatafanya hivyo? Kwa sababu hawezi. Mzungu amemtengeneza shetani ili kuleta machafuko duniani . . . .” Wakati huo huo niliacha kazi kiwanda cha Gar Wood na kwenda kufanya kazi kiwanda cha kampuni ya Ford Motors, tulikuwa kwenye kitengo kilichohusika na uundaji wa Lincoln-Mercury. Nikiwa kama mhubiri kijana, niliweza kwenda Chicago kumuona Elijah Muhammad wakati wowote ambao sikwenda kazini. Naye alinisisitiza kumtembelea kadri niwezavyo. Nilichukuliwa kama mmoja wa watoto wao-yeye na mkewe, dada Clara Muhammad. Niliwaona watoto wao mara chache sana. wengi wao miaka hiyo walikuwa wakifanya kazi mbalimbali jijini Chicago. Udereva taxi, kazi za mikono na nyinginezo kama hizo. Pia nyumbani pale waliishi na mama yake Elijah Muhammad, bi Marie. Nilitumia muda mwingi na Bi Marie kama tu niliotumia na bwana Muhammad. Nilipenda kusikia simulizi zake juu ya maisha ya utotoni ya mwanae walipokuwa wakiishi huko Sandersville Georgia, Elijah Muhammad alizaliwa huko mwaka 1897. Bwana Muhammad alizungumza nami kwa saa na saa. Baada ya kula mlo mzuri wa Kiislamu tulikaa mezani na kuzungumza, au nilienda naye kuzunguka na gari alipokuwa anatembelea maduka machache yaliyomilikiwa na Waislamu pale Chicago. Maduka yalikuwa ni mfano wa kuwaonyesha watu weusi jinsi wanavyoweza kufanya mambo yao wenyewe-kwa kuajiri watu weusi wenzao, na kufanya biashara na weusi wenzao na hivyo kuacha kunyonywa na mzungu. Kwenye duka mchanganyiko la dawa na vitu vya nyumbani lililokuwa kwenye makutano ya mtaa wa Wentworth na mtaa wa 31, bwana Muhammad alifanya kazi ndogondogo kama kufagia nk. Alifanya hivyo kuwaonyesha wafuasi wake aliowafundisha kuwa uvivu na uzembe ni moja ya dhambi kubwa sana ambazo mtu mweusi anajitendea. Nilikuwa natamani kumnyang’anya ufagio sababu nilihisi bwana Muhammad ni wa thamani sana hivyo hakustahili kufagia. Lakini hakuniruhusu kufanya chochote zaidi ya kuambatana naye huku akinishauri juu ya njia bora ya kutangaza ujumbe wake.

Jinsi tulivyokuwa ilinifanya kufikiri kuhusu Socrates kwenye ngazi za soko la Athens akisambaza hekima yake kwa wanafunzi wake. Au jinsi ambavyo mmoja wa wanafunzi wake, Aristotle, naye alivyokuwa akifuatwa na wanafunzi wake alipokuwa akitembea kwenye shule ya Lyceum. Nakumbuka siku moja kulikuwa na glasi chafu ya maji mezani na bwana Muhammad akaweka glasi safi pembeni yake na kusema, “unataka kujua jinsi ya kusambaza mafundisho yangu?” kisha akaniekezeakwenye glasi za maji. “Usimshutumu mtu ukimuoana ana glasi ya maji iliyo chafu. Waonyeshe tu glasi safi uliyonayo. Watakapoichunguza hautakuwa na haja ya kuwaonyesha kuwa yako ni bora zaidi.” Katika vitu vyote ambavyo bwana Muhammad alinifunza sijui kwa nini hilo bado limenikaa akilini japo sijalitumia mara zote. Napenda sana mapambano. Nina muelekeo wa kumuambia mtu kuwa glasi yake ya maji ni chafu. Mwanawe alipokuwa na shughuli nyingi, mama Marie alinisimulia juu ya utoto na ukuaji wake huko Georgia. Alianza kunisimulia tokea yeye mwenyewe akiwa na miaka saba. Aliniambia kuwa wakati huo alipata maono kuwa atakuja kuwa mama wa mtu mkubwa sana. Aliolewa na mhubiri wa kanisa la Kipabtisti, Mcungaji Poole ambaye pia alifanya kazi kwenye mashamba na viwanda vya mbao vilivyokuwepo kule Sandersville. Aliendelea kusema kuwa Elijah alikuwa tofauti sana kati ya watoto wake kumi na tatu. Alisema alianza kuona utofauti wake mara tu alipoanza kutembea.
Mara zote alitatua mizozo ya kaka na dada zake, alisema mama Marie. Pamoja na udogo wake walimchukulia kama kiongozi wao. Na alipofikia umri wa kuanza shule tayari alikuwa ameanza kuonyesha utambuzi mkubwa juu ya suala la rangi za watu katika Marekani. Ilimlazimu kuacha shule baada ya darasa la nne na kwenda kufanya kazi sababu familia ilikuwa masikini. Dada yake mkubwa ndiye alimfundisha nyakati za usiku. Mama Marie alisema kuwa Elijah alikuwa akitumia saa nyingi akisoma biblia huku machozi yakimlengalenga (Bwana Muhammad aliwahi kuniambia kuwa alipokuwa mdogo alihisi kuwa maneno ya Biblia yalikuwa kama mlango uliofungwa, na yanaweza kufunguliwa, anapaswa tu kujua jinsi ya kufungua. Na alikuwa akilia kwa sababu ya kushindwa kupata uelewa kamili) Elijah aliendelea kukua vilevile kidhaifu na kuwa mvulana aliyependa sana jamii yake. Mama Marie alisema kuwa badala ya Elijah kushutumu matendo yaliyokuwa yanafanywa na watu weusi, mara zote alipata sababu ya kutetea kasoro zao. Mama Marie ameishafariki. Naamini alipata moja ya mazishi makubwa sana katika Chicago. Si Waislamu tu, watu wengine pia walijua uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya Elijah na mama yake. “Sioni aibu kusema jinsi elimu yangu ilivyo ndogo,” aliniambia bwana Muhammad. “Kusoma kwangu hadi darasa la nne tu ni ushahidi kuwa sifahamu chochote zaidi ya kile nilichofundishwa na Allah. Allah amenifundisha hesabu.

Alinikuta na ulimi mzito naye akanifundisha kutamka maneno.” Bwana Muhammad alisema kuwa hakuweza kuwavumilia jinsi wazungu wa Sandersville—wakulima, wasimamizi wa viwanda vya mbao na waajiri wengine wa kizungu, watu ambao walizoea kuwatukana wafanyakazi weusi. Alisema kuwa alikuwa akimuomba kistaarabu yeyote aliyemuajiri kuwa kamwe asimtukane. “Niliwaambia kuwa kama hawapendezwi na kazi yangu basi wanifukuze na si kunitukana.” (Bwana Muhammad aliongea kwenye maongezi ya kawaida kama vile alivyokuwa anatoa hotuba. Hakuwa muongeaji mzuri, lakini kila alichoongea kilinigusa sana, hata muongeaji aliyefundishwa hangeweza kunigusa vile. ) Alisema kuwa alifanya kazi alizoajiriwa kwa uaminifu sana kiasi kwamba mara nyingi aliwekwa kuwa msimamizi wa watu weusi wengine. Baadaye, baada ya kuwa amemuoa dada Clara na wana watoto watatu, mwanzoni mwa mwaka 1923 kuna muajiri mmoja wa kizungu alimtukana bwana Elijah Muhammad, wakati huo akitumia jina la Elijah Poole. Ili kuepuka matatizo, Elijah akahama na familia yake kwenda Detroit. Wakati huo alikuwa na miaka ishirini na tano. Watoto wake wengine watano walizaliwa Detroit na wa mwisho alizaliwa Chicago.

Mwaka 1931 bwana Elijah Muhammad alikutana na bwana W. D. Fard huko Detroit. Bwana Muhammad alinisimulia kuwa madhara ya mdororo wa uchumi uliotokea miaka hiyo yaliathiri kila sehemu, lakini kwenye maeneo ya Maghetto ya watu weusi hali ilikuwa mbaya zaidi. Kulikuwa na mnegro mmoja mweupe hivi na mwenye umbo dogo aliyekuwa akienda nyumba kwa nyumba katika maeneo ya watu weusi masikini. Alikuwa akiuza bidhaa za Hariri na bidhaa zingine. Alijitambulisha kama, “Ndugu kutoka Mashariki.” Mtu huyu alianza kuwasimulia watu weusi jinsi walivyotoka kwenye maeneo ya mbali-nchi ya mababu zao. Aliwaonya juu ya kula “Nguruwe wachafu” na vyakula vingine “Visivyofaa” ambavyo watu weusi walikuwa na kawaida ya kuvila. Alianza kufanya mikutano nyumbani kwa watu weusi waliomsikiliza. Alifundisha Biblia na Quran, na moja ya wanafunzi wake alikuwa ni Elijah Poole. Mtu huyu alisema jina lake ni W. D. Fard. Alisema kuwa ni mzaliwa wa kabila la Koreish, kabila la Muhammad ibn Abdullah, Mtume Mwenyewe. Machinga huyu wa hariri na bidhaa zingine aliijua Biblia vizuri kuliko watu weusi waliozaliwa katika Ukristo. Bwana W. D. Fard alifundisha kuwa jina la kweli la Mungu ni Allah, na dini yake ya kweli ni Uislamu, na jina la kweli la waumini wa dini hiyo ni Waislamu.

Bwana W. D. Fard alifundisha kuwa watu weusi wa Marekani ni vitukuu vya Waislamu. Kuwa Watu weusi wa Marekani ni kondoo waliopotea. Wamepotea kwa miaka mia nne kutoka Taifa la Kiislamu, na kwamba yeye, bwana Fard amekuja kuwaokoa na kuwarudisha watu weusi kwenye dini yao ya kweli. Bwana Fard alifundisha kuwa hakuna mbingu iliyo angani wala kuzimu iliyopo ardhini. Mbingu na kuzimu ni hali ambazo watu waliishi hapahapa duniani. Alisema kwa miaka mia nne mtu mweusi wa Marekani ameishi kuzimu, naye amekuja kuwarudisha mbinguni, nyumbani kwao, miongoni mwa watu wa jamii yao. Bwana Fard alifundisha kuwa, kama ambavyo kuzimu ipo duniani basi na shetani yupo duniani, yaani mtu mweupe aliyezaliwa kutoka kwa mtu mweusi miaka elfu sita iliyopita. Lengo hasa la kuzaliwa kwake lilikuwa ni kutengeneza kuzima duniani kwa miaka elfu sita iliyofuatia. Na kuwa watu weusi, watoto wa Mungu walikuwa Miungu pia, alisema. Alifundisha pia kuwa miongoni mwa watu weusi, kulikuwa na mtu ambaye alikuwa Mungu wa Miungu; mkuu wa wakuu, muweza yote, mkuu kwa hekima na nguvu—jina lake rasmi ni Allah. Aliwafundisha waumini wake wa mwanzo kuwa kila dini inasema kuwa karibu na siku za mwisho Mungu atakuja kuwafufua kondoo waliopotea, kuwatenganisha na adui zao na kuwarejesha kwa watu wa jamii yao. Alisema kuwa unabii unamzungumzia mwokozi huyo wa kondoo waliopotea kama Mwana wa Binadamu, Mungu katika mwili, Mwokozi au Mesia atakayetokea kama vile radi itokavyo mashariki kwenda magharibi.
Yeye ndiye ambaye Wayahudi humuita Mesia, Wakristo wakimwita Kristo na Waislamu wakimwita Mahdi.

****
 
Sura ya kumi na mbili inaendelea
Nilikaa na kusikiliza kile ambacho niliamini ni historia ya kweli ya dini yetu, dini ya kweli ya mtu mweusi kutoka kwa bwana Muhammad mwenyewe. Bwana Muhammad akisema kuwa usiku mmoja alipata ufunuo kuwa bwana W. D. Fard ndiye utimizo wa unabii huo. “Nilimuuliza,” alisema bwana Muhammad, “Wewe ni nani na jina lako nani?” Naye alijibu, ‘Mimi ndiye ambaye dunia imekuwa ikimsubiria kwa miaka elfu mbili iliyopita.’ “Nilimuuliza kwa mara nyingine,” alisema, “’Jina lako halisi ni nani?’ Naye alijibu, ‘Jina langu ni Mahdi. Nimekuja kuwaongoza kwenye njia ya kweli.’” Bwana Muhammad alisema kuwa alikaa akisikiliza kwa akili na moyo mkunjufu-kama tu mimi nilivyomsikiliza yeye. Na kuwa hajawahi tilia shaka hata kidogo yale aliyofundishwa na “Mwokozi.”

Polepole W. D. Fard akaanza kufundisha wahubiri wa kwenda kusambaza mafundisho yake kwa watu weusi wa Marekani. Wakati wa kuwapa majina wahubiri wake hawa wa mwanzo, bwana fard alimpa Eiljah Poole jina la “Elijah Karriem.” Kisha mwaka huo wa 1931 bwana Fard akaanzisha Chuo Kikuu cha Uislamu huko Detroit. Kilikuwa na darasa la watu wazima ambalo lilifundisha mambo mbalimbali kutia ndani, hesabu ili kuwasaidia watu weusi kuepuka kutapeliwa na “Shetani wa kizungu mwenye macho ya bluu.” Kuanzisha shule bila kitu kulimaanisha haikuwa na waalimu wenye sifa, lakini iliwalazimu kuanza kwa vyovyote vile. Bwana Elijah Karriem aliwatoa watoto wake kwenye shule za umma za Detroit na kuwapelekea kwenye Chuo Kikuu cha Uislamu kama wanafunzi wa mwanzomwanzo. Bwana Muhammad aliniambia kuwa kitendo cha watoto wake wakubwa kukosa elimu rasmi ni ishara ya kujitoa kwao katika kuanzisha vyuo vikuu vya Kiislamu huko Detroit na Chicago ambavyo leo vina waalimu wazuri zaidi.

Bwana W.D. Fard alimchagua Elijah Karriem kuwa Imam Mkuu juu ya wengine wote. Na hilo lilisababishwa kutokea kwa wivu mkali kutoka kwa wale wengine. Wote walikuwa na elimu nzuri kumshinda Elijah Karriem, na pia walikuwa walikuwa wazungumzaji wazuri kumzidi. Walionyesha hasira zao hata mbele ya Elijah, “Kwa nini tuwe chini ya mtu ambaye hana sifa za kutosha?” Ni wakati huo ndipo Elijah Karriem alibadilishwa jina na kuitwa “Elijah Muhammad,” na akiwa Imam Mkuu alianza kupokea mafundisho binafsi kutoka kwa W. D. Fard kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Elijah Muhammad anasema wakati huo alisikia mambo ambayo hayakufundishwa kwa wengine. Pia ni wakati huo ambao Elijah Muhammad na W. D. Fard walikwenda Chicago na kufungua Hekalu Namba Mbili. Pia waliandaa matayarisho ya Hekalu Namba Tatu huko Milwaukee.

Mwaka 1934, W. D. Fard alipotea ghafla bila kujulikana alikokwenda. Elijah Muhammad alidai kuwa Maimam wengine walijaribu kumuua sababu wivu wao ulikuwa umekuwa mkali sana. Anasema “Wanafiki” hawa walisababisha akimbilie Chicago na Hekalu Namba Mbili likawa makao yake makuu. “Wanafiki” wale walimfuata na huko hivyo akalazimika kukimbilia Washington, D. C na kuanzisha Hekalu Namba Nne. Pia alipokuwa Washington alihudhuria maktaba ya bunge na kusoma vitabu ambavyo W. D. Fard alikuwa amemuambia kuwa vilikuwa na kweli kadhaa ambazo shetani wa kizungu alikuwa ameziandika lakini hazikuwa ndani ya vitabu vinavyopatikana kwa watu wote. Alisema kwa sababu ya kufuatiliwa na “wanafiki” alikuwa akihama miji mara kwa mara, na hakukaa sehemu moja kwa muda mrefu. Alipoweza alikuwa akirudi nyumbani kumtembelea mke na watoto wake nane ambao walitunzwa na Waislamu wengine. Alipokuwa akiitembelea familia yake hata wafuasi wake wa mwanzo pale Chicago hawakujua kama amerudi nyumbani. Maana kwa madai yake ni kuwa “wanafiki” walidhamiria hasa kumuua. Mwaka 1942 bwana Muhammad alikamatwa na polisi. Alisema kuwa kuna watu weusi vibaraka walikuwa wamemchongea kwa shetani mweupe kuhusu mafundisho yake, alishtakiwa kwa kukimbia kujiandikisha jeshini japokuwa umri wake ulikuwa umepita ule wa kutumikia jeshini. Alihukumiwa miaka mitano gerezani na kufungwa huko gereza la Milan, Michigan.

Alitumikia kifungo kwa miaka mitatu na kisha kuachiwa kwa parole. Mnamo mwaka 1946 aliendelea na kazi yake ya kuwatoa watu weusi wa Marekani tongotongo. Mtu huyu mwenye umbo dogo na mpole, Mtukufu Elijah Muhammad ambaye hata sasa hivi anafundisha ndugu na dada zetu huko Chicago! Mtume wa Allah-jambo linalomfanya kuwa mtu mweusi mwenye nguvu zaidi ndani ya Marekani. Alipoteza miaka saba akikimbia wanafiki, akapoteza mingine mitatu na nusu gerezani alikowekwa na shetani mweupe kwa ajili yako na mimi. Shetani huyo hataki Mtukufu Elijah Muhammad atuamshe mimi na wewe, wala kuwaamsha ndugu zetu wengine wajinga na walioshikwa akili hapa Amerika ya Kaskazini-kwenye mbingu ya mzungu na kuzimu ya mtu mweusi.

“Nilikaa chini ya miguu ya mtume wetu na kusikia kweli kutoka katika kinywa chake! Nimeahidi kwa Allah nikiwa nimepiga magoti kuwa nitamwambia mzungu kuhusu uovu wake na mtu mweusi nitamwambia mafundisho ya kweli ya Mtukufu Elijah Muhammad. Sijali iwapo hilo litanigharimu maisha yangu . . . .” Huo ndiyo ulikuwa msimamo wangu. Hayo ndiyo yalikuwa maneno yangu yasiyobadilika, niliyasema popote bila woga wala kusita. Nilikuwa mtumishi wake muaminifu zaidi, na hata leo najua kuwa nilimuamini kuliko hata alivyojiamini. Miaka iliyofuata ilinibidi kukabiliana na mgogoro wa kisaikolojia na wa kiroho.

Mwisho wa sura ya 12.
 
Sura ya kumi na mbili inaendelea
Nilikaa na kusikiliza kile ambacho niliamini ni historia ya kweli ya dini yetu, dini ya kweli ya mtu mweusi kutoka kwa bwana Muhammad mwenyewe. Bwana Muhammad akisema kuwa usiku mmoja alipata ufunuo kuwa bwana W. D. Fard ndiye utimizo wa unabii huo. “Nilimuuliza,” alisema bwana Muhammad, “Wewe ni nani na jina lako nani?” Naye alijibu, ‘Mimi ndiye ambaye dunia imekuwa ikimsubiria kwa miaka elfu mbili iliyopita.’ “Nilimuuliza kwa mara nyingine,” alisema, “’Jina lako halisi ni nani?’ Naye alijibu, ‘Jina langu ni Mahdi. Nimekuja kuwaongoza kwenye njia ya kweli.’” Bwana Muhammad alisema kuwa alikaa akisikiliza kwa akili na moyo mkunjufu-kama tu mimi nilivyomsikiliza yeye. Na kuwa hajawahi tilia shaka hata kidogo yale aliyofundishwa na “Mwokozi.”

Polepole W. D. Fard akaanza kufundisha wahubiri wa kwenda kusambaza mafundisho yake kwa watu weusi wa Marekani. Wakati wa kuwapa majina wahubiri wake hawa wa mwanzo, bwana fard alimpa Eiljah Poole jina la “Elijah Karriem.” Kisha mwaka huo wa 1931 bwana Fard akaanzisha Chuo Kikuu cha Uislamu huko Detroit. Kilikuwa na darasa la watu wazima ambalo lilifundisha mambo mbalimbali kutia ndani, hesabu ili kuwasaidia watu weusi kuepuka kutapeliwa na “Shetani wa kizungu mwenye macho ya bluu.” Kuanzisha shule bila kitu kulimaanisha haikuwa na waalimu wenye sifa, lakini iliwalazimu kuanza kwa vyovyote vile. Bwana Elijah Karriem aliwatoa watoto wake kwenye shule za umma za Detroit na kuwapelekea kwenye Chuo Kikuu cha Uislamu kama wanafunzi wa mwanzomwanzo. Bwana Muhammad aliniambia kuwa kitendo cha watoto wake wakubwa kukosa elimu rasmi ni ishara ya kujitoa kwao katika kuanzisha vyuo vikuu vya Kiislamu huko Detroit na Chicago ambavyo leo vina waalimu wazuri zaidi.

Bwana W.D. Fard alimchagua Elijah Karriem kuwa Imam Mkuu juu ya wengine wote. Na hilo lilisababishwa kutokea kwa wivu mkali kutoka kwa wale wengine. Wote walikuwa na elimu nzuri kumshinda Elijah Karriem, na pia walikuwa walikuwa wazungumzaji wazuri kumzidi. Walionyesha hasira zao hata mbele ya Elijah, “Kwa nini tuwe chini ya mtu ambaye hana sifa za kutosha?” Ni wakati huo ndipo Elijah Karriem alibadilishwa jina na kuitwa “Elijah Muhammad,” na akiwa Imam Mkuu alianza kupokea mafundisho binafsi kutoka kwa W. D. Fard kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Elijah Muhammad anasema wakati huo alisikia mambo ambayo hayakufundishwa kwa wengine. Pia ni wakati huo ambao Elijah Muhammad na W. D. Fard walikwenda Chicago na kufungua Hekalu Namba Mbili. Pia waliandaa matayarisho ya Hekalu Namba Tatu huko Milwaukee.

Mwaka 1934, W. D. Fard alipotea ghafla bila kujulikana alikokwenda. Elijah Muhammad alidai kuwa Maimam wengine walijaribu kumuua sababu wivu wao ulikuwa umekuwa mkali sana. Anasema “Wanafiki” hawa walisababisha akimbilie Chicago na Hekalu Namba Mbili likawa makao yake makuu. “Wanafiki” wale walimfuata na huko hivyo akalazimika kukimbilia Washington, D. C na kuanzisha Hekalu Namba Nne. Pia alipokuwa Washington alihudhuria maktaba ya bunge na kusoma vitabu ambavyo W. D. Fard alikuwa amemuambia kuwa vilikuwa na kweli kadhaa ambazo shetani wa kizungu alikuwa ameziandika lakini hazikuwa ndani ya vitabu vinavyopatikana kwa watu wote. Alisema kwa sababu ya kufuatiliwa na “wanafiki” alikuwa akihama miji mara kwa mara, na hakukaa sehemu moja kwa muda mrefu. Alipoweza alikuwa akirudi nyumbani kumtembelea mke na watoto wake nane ambao walitunzwa na Waislamu wengine. Alipokuwa akiitembelea familia yake hata wafuasi wake wa mwanzo pale Chicago hawakujua kama amerudi nyumbani. Maana kwa madai yake ni kuwa “wanafiki” walidhamiria hasa kumuua. Mwaka 1942 bwana Muhammad alikamatwa na polisi. Alisema kuwa kuna watu weusi vibaraka walikuwa wamemchongea kwa shetani mweupe kuhusu mafundisho yake, alishtakiwa kwa kukimbia kujiandikisha jeshini japokuwa umri wake ulikuwa umepita ule wa kutumikia jeshini. Alihukumiwa miaka mitano gerezani na kufungwa huko gereza la Milan, Michigan.

Alitumikia kifungo kwa miaka mitatu na kisha kuachiwa kwa parole. Mnamo mwaka 1946 aliendelea na kazi yake ya kuwatoa watu weusi wa Marekani tongotongo. Mtu huyu mwenye umbo dogo na mpole, Mtukufu Elijah Muhammad ambaye hata sasa hivi anafundisha ndugu na dada zetu huko Chicago! Mtume wa Allah-jambo linalomfanya kuwa mtu mweusi mwenye nguvu zaidi ndani ya Marekani. Alipoteza miaka saba akikimbia wanafiki, akapoteza mingine mitatu na nusu gerezani alikowekwa na shetani mweupe kwa ajili yako na mimi. Shetani huyo hataki Mtukufu Elijah Muhammad atuamshe mimi na wewe, wala kuwaamsha ndugu zetu wengine wajinga na walioshikwa akili hapa Amerika ya Kaskazini-kwenye mbingu ya mzungu na kuzimu ya mtu mweusi.

“Nilikaa chini ya miguu ya mtume wetu na kusikia kweli kutoka katika kinywa chake! Nimeahidi kwa Allah nikiwa nimepiga magoti kuwa nitamwambia mzungu kuhusu uovu wake na mtu mweusi nitamwambia mafundisho ya kweli ya Mtukufu Elijah Muhammad. Sijali iwapo hilo litanigharimu maisha yangu . . . .” Huo ndiyo ulikuwa msimamo wangu. Hayo ndiyo yalikuwa maneno yangu yasiyobadilika, niliyasema popote bila woga wala kusita. Nilikuwa mtumishi wake muaminifu zaidi, na hata leo najua kuwa nilimuamini kuliko hata alivyojiamini. Miaka iliyofuata ilinibidi kukabiliana na mgogoro wa kisaikolojia na wa kiroho.

Mwisho wa sura ya 12.
Mkuu tunasubiri muendelezo ...shusha vitu tafadhali!
 
Back
Top Bottom