Kwa asilia mwanamke anatakiwa ahudumiwe na mme wake, ikitokea mme wake hahudumii kisa mke wake anakipato au biashara lazima atahongwa na kuanzisha mahusiano yakupatiwa fetha nje ya ndoa
Kwa akili hizi, wewe lazima utakuwa either ni Polisi au CCM.
Ni wapi huko ambapo asili ya Mwanamke ni kuhudumiwa?
Maana the last time I checked, sikuwahi kuona free life and lunch kwa wanawake kwenye jamii nitokayo. Wanawake wamekuwa sehemu muhimu katika ujenzi wa familia na jamii. Ukiacha malezi, wanaume ndiyo walimiliki ardhi lakini wanawake ndiyo waliokuwa wakilima katika ardhi hizo.
Katika jamii niliyotoka, wanawake walilipiwa mahari sababu muoaji alikuwa akipunguza nguvukazi kwenye familia/ukoo hivyo mahari ilikuwa ni replacement ya nguvukazi hiyo inayoenda kuolewa na kwenda kuongeza nguvukazi kwingine. Kama ilitokea Mwanamke ni mvivu basi wazee hawakuwa tayari kupokea mahali au muoaji angetakiwa kutoa hata bata kama mahari.
Hivyo nataka kukumbusha tu kwamba, kiasili mwanamke ni mtafutaji sambamba kabisa na mwanaume. Si wa kuhudumiwa kama unavyoiweka, ingawa unaweza ukawa upo sahihi kwa jamii utokayo.