- Thread starter
- #61
Dah nasikitika Sana ,pale ukifika kijijini watakupokea kwa bashasha hasa Kama ulikuwa una utaratibu wa kutuma hela za hapa na pale ,bad enough wao uwa wanaamini ukifika chuo umetoboa ,ni hapo nakuona ukiwa very stressed .
Aisee Kaka rudi nyumbani ila kapige jembe haswa bila kutizama watanionaje .
Ningenunua vitu vyako ili nikuongezee hela ya kwenda kujianza ila Kaka yako niko juu ya mawe ,hela ya vikoba niliyokopa imenitokea puani silali usiku na mchana nimekuwa Kama digidigi ,nenda kapambane mdogo wangu nikiaaliwa kulimaliza hili la mikopo ya vikoba salama bila kufa Wala kukimbia nchi basi nitakutafuta walau tupige hata story .
Kwaheri ,nenda mdogo wangu
maneno matamu sana haya