Kitanda na rangi za chumba nilichoandaliwa ukweni kimenisononesha sana

View attachment 3399917

Nimeoa kwenye mkoa mmoja wa Kanda ya Kaskazini ambako huko kunatajwa na kuogopwa sana na watu wasio wa ukanda huo, kwani kunasifika kwa kuua mume akiwa na mafanikio.

Hii sio mara ya kwanza kuwatembelea wakwe zangu, na mara zote huwa naandaliwa chumba kizuri chenye kitanda kikubwa, rangi za kuta nyeupe na matandiko huwa ya rangi nzuri zilizotulia.

Sasa uchumi wangu umeongezeka sana, na Nina mafanikio sana kwenye uwekezaji wangu.

Wakwe wameniandalia chumba cha rangi ya zambarau, ambayo ni rangi ya msibani.

Mashuka na matandiko yenye rangi nyekundu, ambayo ni rangi inayoonyesha kumwagika kwa damu.

Pia kitanda nilichoandaliwa ni kidogo sana cha futi sita kwa mbili na nusu, utadhani kitanda cha kuoshea maiti.

Kwa kweli mapokezi haya yamenifikirisha sana, kuanzia Leo usiku nitaenda kulala Arusha, hawa wakwe nadhani wameona sasa wayatamatishe maisha yangu.

Wamenikosa
Wewe hufai kukaribishwa, siku nyingine beba kitanda chako na chakula chako na sahani zako. Pumbaffff.
 
Kwa hiyo chumba kilipakwa rangi ya zambarau kwa ajili yako tu? Hayo mashuka yamenunuliwa kwa ajili yako tu? Na hicho kitanda ni maalum kwa ajili yako tu kukilalia?

Nikisema una changamoto ya afya ya akili nitakuwa nimekukosea?
Nyumba nimeijenga mwenyewe, nimewakabidhi nyumba ikiwa fully furnished, ndio maana nashangaa. Rangi za vyumba vyote vilikuwa ni nyeupe, vitanda vyote vilikuwa ni queen size, hiki kimetoka wapi?
 
View attachment 3399917

Nimeoa kwenye mkoa mmoja wa Kanda ya Kaskazini ambako huko kunatajwa na kuogopwa sana na watu wasio wa ukanda huo, kwani kunasifika kwa kuua mume akiwa na mafanikio.

Hii sio mara ya kwanza kuwatembelea wakwe zangu, na mara zote huwa naandaliwa chumba kizuri chenye kitanda kikubwa, rangi za kuta nyeupe na matandiko huwa ya rangi nzuri zilizotulia.

Sasa uchumi wangu umeongezeka sana, na Nina mafanikio sana kwenye uwekezaji wangu.

Wakwe wameniandalia chumba cha rangi ya zambarau, ambayo ni rangi ya msibani.

Mashuka na matandiko yenye rangi nyekundu, ambayo ni rangi inayoonyesha kumwagika kwa damu.

Pia kitanda nilichoandaliwa ni kidogo sana cha futi sita kwa mbili na nusu, utadhani kitanda cha kuoshea maiti.

Kwa kweli mapokezi haya yamenifikirisha sana, kuanzia Leo usiku nitaenda kulala Arusha, hawa wakwe nadhani wameona sasa wayatamatishe maisha yangu.

Wamenikosa
CHAPA LAPA
 
Wamekudharau coz wewe ni masikini choka mbaya,ndio maana umejiwahi kwa kujidai kua eti uchumi wako umeongezeka na una mafanikio,hiyo kauli umeitumia tu kama defensive mechanism coz unajua kua wachangiaji watakuchana kua tafuta hela ili uache kulalamika kwenye vitu vidogo,

Mtu mwenye uchumi imara hawezi kuanzisha uzi kama huu
 
Back
Top Bottom