Kitanda na rangi za chumba nilichoandaliwa ukweni kimenisononesha sana

Kitanda na rangi za chumba nilichoandaliwa ukweni kimenisononesha sana

Uchumi wako umeongezeka vipi wakati unalala kwa wakwe?acha kuchafua wakwe zako kwa imani zako za kishirikina zilizojaa kichwani
Mimi ukweni tena kilimanjaro tu hapo ndani ndani ukienda hakuna hata guest moja inakubidi tu ulale kwa wakwe.

Tanzania kubwa sana sio kila sehemu zina nyumba za kulala wageni.
 
Labla hicho chumba wakwe hua wanakodisha Kama guest house 😂
 
Unalalaje ukweni bro chukua chumba gest ulale nyumbani unaenda kusalimia na kupiga msosi labda kama uchumi hauko sawa unapaswa ulale nyumbani kwenu tu hata kama pakoje,mwanaume unalale ukweni.
Kikao tumemaliza saa nane usiku huko migombani, chumba ningechukia wapi?
 
View attachment 3399917

Nimeoa kwenye mkoa mmoja wa Kanda ya Kaskazini ambako huko kunatajwa na kuogopwa sana na watu wasio wa ukanda huo, kwani kunasifika kwa kuua mume akiwa na mafanikio.

Hii sio mara ya kwanza kuwatembelea wakwe zangu, na mara zote huwa naandaliwa chumba kizuri chenye kitanda kikubwa, rangi za kuta nyeupe na matandiko huwa ya rangi nzuri zilizotulia.

Sasa uchumi wangu umeongezeka sana, na Nina mafanikio sana kwenye uwekezaji wangu.

Wakwe wameniandalia chumba cha rangi ya zambarau, ambayo ni rangi ya msibani.

Mashuka na matandiko yenye rangi nyekundu, ambayo ni rangi inayoonyesha kumwagika kwa damu.

Pia kitanda nilichoandaliwa ni kidogo sana cha futi sita kwa mbili na nusu, utadhani kitanda cha kuoshea maiti.

Kwa kweli mapokezi haya yamenifikirisha sana, kuanzia Leo usiku nitaenda kulala Arusha, hawa wakwe nadhani wameona sasa wayatamatishe maisha yangu.

Wamenikosa
Mwenzako alilazea kwenye chumba kina rangi nyeusi tiiii, hakuna dirisha, balbu inatoa mwanga wa mwekundu
 
Nyumba nimeijenga mwenyewe, nimewakabidhi nyumba ikiwa fully furnished, ndio maana nashangaa. Rangi za vyumba vyote vilikuwa ni nyeupe, vitanda vyote vilikuwa ni queen size, hiki kimetoka wapi?
Tupatie picha na hati ya makabidhiano ya nyumba tutakuamini vipi ??
 
Back
Top Bottom