Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kitanzi cha CCM Kawe: Watia nia 176 wa ubunge dhidi ya Halima Mdee CHADEMA

.
 
Dah...kibongobongo...kazi ya ubunge ndiyo kazi rahisi kukiko zote ....inahitaji sifa mbili tu ..kujua kusoma na kuandika...wakati Konda wa daladala lazima ajue na kuhesabu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hii kali nimecheka kwa nguvu
 
======
UPDATE: Waliochukua fomu hadi leo, Julai 17, wamefikia 176
======

Hili linaweza kuwa ajabu lingine la dunia ama linaweza kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia World Guinness Book of Records, ama linaweza kuvunja rekodi ya nchi na dunia kwa jimbo moja la ubunge kuwa na watia nia wengi kuwahi kutokea na karibia asilimia mia moja wa chama kimoja.

Pamoja na kwamba kibubu cha tume ya uchaguzi ya CCM kitatuna kwa mapato na pengine kuwa jimbo lililoingiza mapato mengi zaidi kwa kuuza form nyingi zaidi lakini madhara yake ni makubwa kuliko hayo mapato.

1. Katika watia nia wote hao 80 nina hakika hawapungui walau 20 wenye nguvu ya pesa, ushawishi ndani ya chama na wale wa mbeleko na vimemo. Kwa kuzingatia hili pekee tayari yatatokea makundi yasiyopungua 10 hivi. Makundi yenye nguvu na misuli ya kila aina. Hapa badala ya kupambana na adui yataanza kupambana yenyewe kwa yenyewe.

Jimbo la Kawe lililomegwa kutoka Kinondoni limekuwa na umaarufu mkubwa kuliko hata Kinondoni yenyewe na hii pengine ni kutokana na jiografia yake na aina ya mtu anayelishikilia.

3. CCM wanalitaka hilo Jimbo kwa hali na mali. Na wamewekeza muda mrefu sana tena kwa gharama kubwa mno. Hivyo kitendo cha kulikosa kitakuwa aibu kubwa, fedheha na hasara kubwa kisiasa.

4. Kitendo cha wanaume na uwekezaji wao wote kuja kushindwa na mwanamke mmoja ni ndoto ya kutisha sana na jinamizi wasilolipenda CCM

5. Kuonesha umwamba na ubabe kuwa wakitaka kitu hawashindwi kwakuwa wana kila kitu kila nyenzo ya kupata ushindi

Ni kwa muktadha huo wa kukamia kulikopitiliza hilo jimbo.. Wamejikuta wanatoa boko. Kwakuwa watatumia muda mwingi sana kwenye:
Mchujo
Kupata tano bora
Kwenye kupata mgombea mmoja
Kwenye kuunganisha makundi
Kwenye kuponya majeraha kabla ya uchaguzi

Kumbuka kila hatua kati ya hizo zote itaacha maumivu kwa kundi fulani
Ni wakati wakihangaika na yote haya Halima Mdee atakuwa busy kuimarisha himaya yake.

Matokeo yake ni nini? Muda utasema

Yupo mtu huko anaitwa poti 0713942322 yeye kapita kwa watia nia wote kawachukulia pesa kawambia yupo nao bega kwa bega ebu fikiria watu 176 achukue milion moja moja tu tayari katengeneza pesa, wamejitokeza wengi lakini madalali wa siasa huko nao wanawapiga kwa kwenda mbele wanapigwa vibaya mpaka mchujo kufika top 3 watakuwa wameliwa pesa nyingi sana
 
Unaweza kuwa sahihi maana halima 2010 aliupata baada ya Katibu wa Mkoa wa CCM kuingiza jina la Kizigha kinyemela wanaCCM wakanuna na kumpa mdee.
Sasa watia nia wengi wanaibiwa na kundi la wajanja wachache waliojipenyeza humo usiku na mchana
 
Halima itabaki stori aliwahi kuwa mbunge machachari wa Kawe!! hawezi kushinda by any means and she should start to prepare to face that reality and get used to it!!
And you are the dispenser of that reality?
Which makes you an ignominious.
 
And you are the dispenser of that reality?
Which makes you an ignominious.

Mkuu mimi kuamini Mdee is no more as mbunge wa Kawe hakunijengei aibu yoyote kwenye jamii!! kwani kosa langu ni lipi na kura zitapigwa kujua ni Mdee au Paskal Mayalla?

Mkuu siku zote kuna stages za kuukubali ukweli naelewa ni ngumu kumeza na ni lazima chadema mzipitie stages zote, stage namba moja ni Information!! namba mbili ni DENIAL , mkijikwamua toka hapo DENIAL mlipokwamia miaka yote hii huko mbele kwenye CONSCIOUSNESS and Reality ni mteremko!

Halima, DJ , Sugu , Prof J ,wote kwishney nawashauri watunze vizuri kiinua mgongo chao bunge lijalo hawana siti tena za kwenda kuzipasha joto!!

mimi ni sisiem najua what we kijani think and do kwa watu dizaini ya Mdee! sisiem hatupendi kulea wanaotukera na kukwamisha juhudi, Magufuli the Black White man aka Bulldozer aka Mubashara hahitaji kina Halima na kelele zao wanatuchelewesha kufikia uchumi wa juu, bao la mkono ni halali yake Halima kama akisumbua kwenye kura!!!
 
Unaweza kuwa sahihi maana halima 2010 aliupata baada ya Katibu wa Mkoa wa CCM kuingiza jina la Kizigha kinyemela wanaCCM wakanuna na kumpa mdee.
Sasa safari hii Angela kizigha yuko moto anapambana na Yusuph Mwenda .. Muda huu wajumbe wapiga kura baadhi wanakutana sehemu kupanga yao

Uchaguzi ni Leo ukumbi wa mbezi beach huko
 
Sasa safari hii Angela kizigha yuko moto anapambana na Yusuph Mwenda .. Muda huu wajumbe wapiga kura baadhi wanakutana sehemu kupanga yao

Uchaguzi ni Leo ukumbi wa mbezi beach huko
Mie Naona halima keshapita maana huku si kujichanganya, maskini CCM Kawe
 
Mie Naona halima keshapita maana huku si kujichanganya, maskini CCM Kawe
2010-2015 Ccm wakawe walijichanganya kumleta Angela kazigha ,wakasalitiana

2015-2020 Ccm walirudia kosa lile lile kwa kumleta Kipi Warioba ,na ule upepo wa EL ,wakasalitiana zaidi ( kiasi viongozi wengi wa Ccm mkoa na wilaya walipoteza nafasi zao

2020-2025 , wakibugi tena imekula kwao
 
Hata Kigamboni kama wataforce kuliingiza lishenzi Bashite jua upinzani utachukua. Inabidi intelligensia ya chama ifanyekazi haswa kujua nani Kawe anapendwa maana halima has to go kwa kweli
 
Hata Kigamboni kama wataforce kuliingiza lishenzi Bashite jua upinzani utachukua. Inabidi intelligensia ya chama ifanyekazi haswa kujua nani Kawe anapendwa maana halima has to go kwa kweli
Kama kawe watapita Hawa halima kutusua ni ngumu

1.Angela kazigha , safari hii ccm kawe wake nae
2.Yusuph Mwenda yule meya wa kino zamani
3.Kuna jamaa anaitwa bulldozer

Gwajima huyu anafaa kupiga debe nchi nzima ,muhimu waumini wake wapewe maelekezo
 
Back
Top Bottom