Mkimaliza kutifuana kuhusu Ubora kati ya Beberu marekani na Tapeli Janjaruko China, mje sasa tujadili kuhusu our third world developing country Tanzania, nchi ambayo kwa zaidi ya miaka na miaka tumebaki ktk siasa za ugomvi, maendeleo ya kibaguzi, miaka nenda rudi wenzetu wanagundua na kuvumbua mambo sisi bado tupo kujenga matundu ya vyoo vya shule zenye wanafunzi zaidi ya 400, walimu 10, mazingira mabovu ya kujifunzia, uhaba wa walimu, uhaba wa nyumba za walimu, mishahara mibovo, siasa mbovu, viongozi wanafiki walafi, washenzi na wavivu.
Anyway kuhusu USA na washirika wake hao zama zao zishakwisha hao kiufupi muda wao wa kuanguka ndio huu, watasumbuana sana baadhi ya mataifa yanayowazidi maendeleo&ushawishi kwa muda tu lkn haitisaidia kitu, kuanguka kupo pale pale.
Kuanguka kwao kuna sababu ambazo walizisababisha wao wenyewe na wanaendelea kuzisababisha.
Mfano issue ya maendeleo ya China kwa ukubwa wao wamechangia kwa sehemu kubwa, yaani nyoka unayemfuga leo, kesho anakugeuka kukushambulia.
Pili hao USA na baadhi ya washirika wao ktk masuala ya kuijenga future yao na race yao wameshafeli pakubwa mpaka sasa, wamebaki kupitisha masheria ya ajabu ajabu ya kuharibu uzao wao wenyewe na nguvu kazi ya taifa kwa kuruhusu baadhi ya sheria pinzani kwa Asili ya uzazi kama vile homosexual, malezi mabovu kwa watoto, utoaji mimba&uzazi wa mpango uliopitiliza, Uhuru uliopitiliza, kwa aina hii ya taratibu mbovu, imekuwa ikikimaliza kizazi chao taratibu, japo wengi hawaoni, lkn mtoto wa leo ndie kijana wa kesho, na mzee wa leo ndie kijana wa jana na mtoto wa juzi, hivyo Kuharibu Uzao ni kuiharibu Future ya wazao, kuharibu kizazi cha leo ni kuiharibu kesho ya hao wazao.
Pia aina ya siasa za hao wamarekani na nduguzo zimeshawachosha wengi dunian, yaani zile siasa za kupangiana na kutishana kuhusu mambo ya nchi yako mwenyewe zimeshafika mwisho, sikuhizi si maajabu mpaka baadhi ya nchi hoehae za huku Afrika zinavimbiana sauti na hao wamagharibi, mfano Niger, Burkina Faso, mpaka Uganda hapo nao wanampandishia sauti Beberu na washirika wake, kiufupi ushawishi na hilo taifa umeshajifia.
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea hilo taifa la USA kufeli duniani kiitikadi&kisiasa, kimaendeleo&kitechnolojia mpaka kijamii wanazidi kufeli pakubwa sana dhidi ya China na baadhi ya nchi za Asia.
Baadae sana kama China nae atazubaa basi tutegemee Super power mkubwa kuliko yeyote aliyewai kuwepo kama Afrika itaamka na kujifunza ujinga ilioufanya na kuchukua hatua basi kuna uwezekano Kukatokea Taifa jipya kutoka Afrika ama Muungano wa nchi za Afrika kuleta Taifa moja powerfull.
Suala la muda tu siasa za dunia zishaonesha