Kiteknolojia China iko sawa na nchi za Marekani na Ulaya

"Kusema ukweli, ni kwamba watu ambao hawaendi China mara nyingi hufikiria kuwa wako nyuma, lakini unapoenda huko unavutiwa na wanachofanya katika teknolojia."
–Brad Smith (Raisi wa Microsoft)

Nchi za Magharibi hazipaswi kudhani kuwa China iko nyuma ya Marekani na Ulaya kwenye maendeleo ya teknolojia, raisi na makamu mwenyekiti wa Microsoft alionya.

Mvutano wa Marekani na China katika miaka michache iliyopita ulijikita katika vita kati ya mataifa hayo mawili ya ukuu wa teknolojia, na kupelekea Marekani kudhibiti mauzo ya chips za hali ya juu nchini China ikitaka kudhoofisha taifa hilo la pili duniani kwa uchumi mkubwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Huawei ya China ilishangaza soko la dunia kwa kutolewa kwa simu mahiri yenye kasi ya upakuaji yenye 5G, na hivyo kuonyesha mafanikio dhahiri katika chip licha ya vikwazo vya teknolojia kutoka Marekani.

Akizungumza katika mkutano wa teknolojia ya Wavuti (Web summit tech conference) huko Lisbon, Ureno, Jumanne 12 Nov. Brad Smith wa Microsoft aliiambia CNBC kwamba;

"Kwa njia nyingi, China iko karibu na au hata inapatana na teknolojia ya nchi za Magharibi."

Alitabiri kuwa makampuni ya China na Marekani yatakuwa yakishindana katika teknolojia katika siku za mbeleni na kuzitaka kampuni za Marekani na Ulaya kushirikiana kukuza uchumi na kuleta maendeleo mapya kama vile akili bandia (AI) kwa dunia nzima.

Maneno kama haya sio mara ya kwanza kuyasikia yakisemwa na viongozi wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya
, CEOs wa Ford na Apple waliwahi kunukuliwa wakisema:

"Watengenezaji wa magari wa China wanaenda kwa mwendo wa kasi wa mwanga, kwa kutumia akili ya bandia na teknolojia nyingine za hali ya juu katika magari yao tofauti na teknolojia yoyote iliyopo Marekani. Wanatengeneza magari kwa gharama nafuu ili kupunguza gharama na yaliyo na teknolojia za kisasa na wamepanuka kikamilifu katika masoko ya nje ya China, hili ni tishio lililopo kwetu."
–Jim Farley (Ford CEO)
No supply chain in the world is more critical to us than China. We're not in China for low labor costs. In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
–Tim Cook (Apple CEO)

Kauli za viongozi wa juu wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya ni tofauti sana na wanasiasa wao kama Trump na Biden na sera zao dhidi ya China.

Wanasiasa wa nchi za Magharibi wanaongea kisiasa wakati wakuu wa makampuni makubwa duniani wanazungumzia uhalisia. Kwa sasa hauwezi kuikimbia China katika dunia ya kibiashara na kiteknolojia.

Una wachina hawa hawa wenye vinasaba na hawa machinga wa kichina wa kariakoo?
 
Unaelewa tofauti ya copy and paste na innovation?

Kuna tofauti kubwa kati ya J-35 na F-35. J-35 ni twin engine na F-35 ni single engine

Zina tofauti kubwa sana kwenye mission sets, power production, avionics n.k
Yeye unabishana na mtu akiona Shap ya nje anajua na cockpits nako kunafanana
 
CEOs wa MNCs za nchi za Magharibi kwa kauli zao wenyewe wamekiri kuwa China ilipofikia kiteknolojia ni level nyingine kiteknolojia. Kati ya wewe na hao CEOs nani tumsikilize?

Tutajie nchi za West ambazo miaka 60 iliyopita zilikuwa kama China ya leo
Wabongo hawaambii baya kuhusu west yaa west wakianguka kuna wabongo wataokaomboleza kulik wakifiwa na watoto wao .kuanguka kwa west ndo ahueni ya dunia ya tatu
 
Unaifahamu historia ya China kwa udogo tu achana hata na hii inayo wahusu wakomunisti

Wewe unaifahamu historia ya West ambao ndo watabe wa dunia hadi sasa?

In terms of economic output and strength, the gap between America and China's GDP stands at about $10 trillion.

According to the World Bank, the per capita GDP in the US is $76,329 and for China it's $13,600. That's nowhere near each other. the US GDP per capita is 5.6 times higher than for China.

Nenda huko China kalipwe peanuts bila benefits zozote. Narudia, haki anazopata janitor kiwanja ni kubwa kuliko za CEO aliyeko China. Kinachoikwamisha West sasa ni maendeleo yao in terms of rights, wages, living standards zipo juu sana sasa they work against themselves (blessing in disguise).
 
Per capita ya Monaco ni ngapi na ya marekani ni ngapi ?

Per capita ya Macau ni ngapi na ya marekani ni ngapi ?

N.b: Huwa unasoma soma magazeti,machapisho na vitabu vinavyohusu uchumi ?
 
Wewe unaifahamu historia ya West ambao ndo watabe wa dunia hadi sasa?

In terms of economic output and strength, the gap between America and China's GDP stands at about $10 trillion.

According to the World Bank, the per capita GDP in the US is $76,329 and for China it's $13,600. That's nowhere near each other. the US GDP per capita is 5.6 times higher than for China.

Nenda huko China kalipwe peanuts bila benefits zozote. Narudia, haki anazopata janitor kiwanja ni kubwa kuliko za CEO aliyeko China. Kinachoikwamisha West sasa ni maendeleo yao in terms of rights, wages, living standards zipo juu sana sasa they work against themselves (blessing in disguise).
Wazungu wa magharibi walitia mguu pwani ya Afrika mashariki miaka mingi baadae baada ya wachina kutia mguu ooh sorry ni baada ya kuiba teknolojia ya kutengeneza karatasi kutoka kwa wachina ili kuja kuwa sainisha mikataba ya kilaghai wakina chifu mangungo, ni baada ya kuiba teknolojia ya unga wa risasi na kuanza kuuwa watu hovyo hovyo duniani, nilisahau bila priting technology ya wachina wasingeweza chapisha mikataba yao ya kitapeli, nilitaka kusahau tena bila compas ya mchina wasingeweza kusafiri na vimeli vyao, Duuh hata bila hela hawa wazungu wangeweza vipi kununua watumwa kweli wasingeweza ashukuriwe mchina kuwaokoa

Wakati wachina wanafanya maajabu haya hao wamagharibi walikuwa wanakunya vichakani bado hawajitambui
 
Per capita ya Monaco ni ngapi na ya marekani ni ngapi ?

Per capita ya Macau ni ngapi na ya marekani ni ngapi ?

N.b: Huwa unasoma soma magazeti,maharishi na vitabu vinavyohusu uchumi ?

Macao gdp per capita for 2023 was $66,835. US is $76,329. In other words, Macau haifikii average per capita ya US nzima. Au ni sawa na kusema janitor wa kiwanja anahela ndefu kuliko mfanyakazi wa kawaida huko Macau. Hapo sijaongelea per capita ya county kama LA au Manhattan ambazo ni counties tu zenye watu less than 2M.

Sijui Monaco inaingiaje kwenye hii convo.

Wewe ndo ujielimishe kuhusu uchumi na jiulize kwanini wachina wengi bado ndoto yao ni kuishi kiwanja au West wakati kiwanja janitor hana mpango kabisa wa kutembelea China let alone kuishi huko.
 
Wazungu wa magharibi walitia mguu pwani ya Afrika mashariki miaka mingi baadae baada ya wachina kutia mguu ooh sorry ni baada ya kuiba teknolojia ya kutengeneza karatasi kutoka kwa wachina ili kuja kuwa sainisha mikataba ya kilaghai wakina chifu mangungo, ni baada ya kuiba teknolojia ya unga wa risasi na kuanza kuuwa watu hovyo hovyo duniani, nilisahau bila priting technology ya wachina wasingeweza chapisha mikataba yao ya kitapeli, nilitaka kusahau tena bila compas ya mchina wasingeweza kusafiri na vimeli vyao, Duuh hata bila hela hawa wazungu wangeweza vipi kumunua watumwa kweli wasingeweza ashukuriwe mchina kuwaokoa

Wakati wachina wanafanya maajabu haya hao wamagharibi walikuwa wanakunya vichakani bado hawajitambui

Wachina walipofika waliwaachia nini nyie cha maana hata kwa bahati mbaya tu?

Bila hao wazungu na ukoloni, ambao I don't support, ungekua bushman hadi leo. Shule, hospital, barabara ngapi walijenga? Taja kimoja tu cha mchina?

Kipindi wakoloni wanakuja Africa China ilikua kama Ileje tu hawana mbele wala nyuma. Haya maendeleo yao wameyapata in the last 50yrs. Ndo maana nasema wachina walipo sasa West ilikua huko miaka 100 iliyopita. Wachina wakifikia maendeleo ya West kwa kila nyanga yani rights, wages, living standards West itakua mbali zaidi. It's as clear as the day light.
 
Wachina walipofika waliwaachini nini nyie cha maana hata kwa bahati mbaya tu?

Bila hao wazungu na ukoloni, ambao I don't support, ungekua bushman hadi leo. Shule, hospital, barabara ngapi walijenga? Taja kimoja tu cha mchina?

Kipindi wakoloni wanakuja Africa China ilikua kama Ileje tu hawana mbele wala nyuma. Haya maendeleo yao wameyapata in the last 50yrs. Ndo maana nasema wachina walipo sasa West ilikua huko miaka 100 iliyopita. Wachina wakifikia maendeleo ya West kwa kila nyanga yani rights, wages, living standards West itakua mbali zaidi. It's as clear as the day light.
Kwa nini tuachiwe ? Ulitaka nao wachina wasombe babu zetu kama mbuzi au watandike viboko ucgi wazee wetu mbele ya wanao hiyo ndio alama uliyotaka watuachie ?

Unaifahamu historia ya China duniani bwana mdogo au upeo hapa ndipo ulipoishia ?
 
Macao gdp per capita for 2023 was $66,835. US is $76,329. In other words, Macau haifikii average per capita ya US nzima. Au ni sawa na kusema janitor wa kiwanja anahela ndefu kuliko mfanyakazi wa kawaida huko Macau. Hapo sijaongelea per capita ya county kama LA au Manhattan ambazo ni counties tu zenye watu less than 2M.

Sijui Monaco inaingiaje kwenye hii convo.

Wewe ndo ujielimishe kuhusu uchumi na jiulize kwanini wachina wengi bado ndoto yao ni kuishi kiwanja au West wakati kiwanja janitor hana mpango kabisa wa kutembelea China let alone kuishi huko.
Umewahi fika China ? Una uhakika hakuna wamarekani hawapo China bwana mdogo ?
 
Kwa nini tuachiwe ? Ulitaka nao wachina wasombe babu zetu kama mbuzi au watandike viboko ucgi wazee wetu mbele ya wanao hiyo ndio alama uliyotaka watuachie ?

Unaifahamu historia ya China duniani bwana mdogo au upeo hapa ndipo ulipoishia ?

The term "human right" doesn't exist kwa wachina. Uliza mambo wanayowafanyia wamatumbi wenzenu kila siku au google ujionee.

Wachina in the 60s tu hapo walikua sawa na Ileje. Haya maendeleo yao ni hivi recent tu kama unaijua historia nyingine sema wewe.
 
Umewahi fika China ? Una uhakika hakuna wamarekani hawapo China bwana mdogo ?

Wapo. Jiulize wangapi wanaenda kuishi huko permanently au kutembea tu. Hata kutembea tu wanaoenda ni wachache sana. Wakati wachina wanaingia kiwanja hadi kwa kuzamia kabisa yani wanakimbia maendeleo ya nchi yao wenyewe ili wazamie kiwanja 🤣

Bwana mdogo Bufa rudi kijijini kwenu ileje ukatambikwe maana inaonekana una ushamba wa states na ujinga wa asili.

Nashindwa hata nijadiliane na wewe nini maana unaandika utumbo au upo high muda wote bwana mdogo maana sikuelewi
 
Njoo kiwanja ule mema ya dunia, braza. Huko China ni Ileje iliyochangamka tu. Maza mwenyewe kacheza DV green card lottery 🤣

I rest my case.
 
Umemuelewa Tim Cook alichosema hapa?

No supply chain in the world is more critical to us than China.
We're not in China for low labor costs....In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple
football fields."

China itaipita Marekani. Halafu China nayo itapitwa na India.
 
"Kusema ukweli, ni kwamba watu ambao hawaendi China mara nyingi hufikiria kuwa wako nyuma, lakini unapoenda huko unavutiwa na wanachofanya katika teknolojia."
–Brad Smith (Raisi wa Microsoft)

Nchi za Magharibi hazipaswi kudhani kuwa China iko nyuma ya Marekani na Ulaya kwenye maendeleo ya teknolojia, raisi na makamu mwenyekiti wa Microsoft alionya.

Mvutano wa Marekani na China katika miaka michache iliyopita ulijikita katika vita kati ya mataifa hayo mawili ya ukuu wa teknolojia, na kupelekea Marekani kudhibiti mauzo ya chips za hali ya juu nchini China ikitaka kudhoofisha taifa hilo la pili duniani kwa uchumi mkubwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Huawei ya China ilishangaza soko la dunia kwa kutolewa kwa simu mahiri yenye kasi ya upakuaji yenye 5G, na hivyo kuonyesha mafanikio dhahiri katika chip licha ya vikwazo vya teknolojia kutoka Marekani.

Akizungumza katika mkutano wa teknolojia ya Wavuti (Web summit tech conference) huko Lisbon, Ureno, Jumanne 12 Nov. Brad Smith wa Microsoft aliiambia CNBC kwamba;

"Kwa njia nyingi, China iko karibu na au hata inapatana na teknolojia ya nchi za Magharibi."

Alitabiri kuwa makampuni ya China na Marekani yatakuwa yakishindana katika teknolojia katika siku za mbeleni na kuzitaka kampuni za Marekani na Ulaya kushirikiana kukuza uchumi na kuleta maendeleo mapya kama vile akili bandia (AI) kwa dunia nzima.

Maneno kama haya sio mara ya kwanza kuyasikia yakisemwa na viongozi wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya
, CEOs wa Ford na Apple waliwahi kunukuliwa wakisema:

"Watengenezaji wa magari wa China wanaenda kwa mwendo wa kasi wa mwanga, kwa kutumia akili ya bandia na teknolojia nyingine za hali ya juu katika magari yao tofauti na teknolojia yoyote iliyopo Marekani. Wanatengeneza magari kwa gharama nafuu ili kupunguza gharama na yaliyo na teknolojia za kisasa na wamepanuka kikamilifu katika masoko ya nje ya China, hili ni tishio lililopo kwetu."
–Jim Farley (Ford CEO)
No supply chain in the world is more critical to us than China. We're not in China for low labor costs. In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
–Tim Cook (Apple CEO)

Kauli za viongozi wa juu wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya ni tofauti sana na wanasiasa wao kama Trump na Biden na sera zao dhidi ya China.

Wanasiasa wa nchi za Magharibi wanaongea kisiasa wakati wakuu wa makampuni makubwa duniani wanazungumzia uhalisia. Kwa sasa hauwezi kuikimbia China katika dunia ya kibiashara na kiteknolojia.
China yenyewe si sawa na China.
 
Back
Top Bottom