Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
"Kusema ukweli, ni kwamba watu ambao hawaendi China mara nyingi hufikiria kuwa wako nyuma, lakini unapoenda huko unavutiwa na wanachofanya katika teknolojia."
–Brad Smith (Raisi wa Microsoft)
–Brad Smith (Raisi wa Microsoft)
Nchi za Magharibi hazipaswi kudhani kuwa China iko nyuma ya Marekani na Ulaya kwenye maendeleo ya teknolojia, raisi na makamu mwenyekiti wa Microsoft alionya.
Mvutano wa Marekani na China katika miaka michache iliyopita ulijikita katika vita kati ya mataifa hayo mawili ya ukuu wa teknolojia, na kupelekea Marekani kudhibiti mauzo ya chips za hali ya juu nchini China ikitaka kudhoofisha taifa hilo la pili duniani kwa uchumi mkubwa.
Mwishoni mwa mwaka jana, Huawei ya China ilishangaza soko la dunia kwa kutolewa kwa simu mahiri yenye kasi ya upakuaji yenye 5G, na hivyo kuonyesha mafanikio dhahiri katika chip licha ya vikwazo vya teknolojia kutoka Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa teknolojia ya Wavuti (Web summit tech conference) huko Lisbon, Ureno, Jumanne 12 Nov. Brad Smith wa Microsoft aliiambia CNBC kwamba;

"Kwa njia nyingi, China iko karibu na au hata inapatana na teknolojia ya nchi za Magharibi."
Alitabiri kuwa makampuni ya China na Marekani yatakuwa yakishindana katika teknolojia katika siku za mbeleni na kuzitaka kampuni za Marekani na Ulaya kushirikiana kukuza uchumi na kuleta maendeleo mapya kama vile akili bandia (AI) kwa dunia nzima.
Maneno kama haya sio mara ya kwanza kuyasikia yakisemwa na viongozi wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya, CEOs wa Ford na Apple waliwahi kunukuliwa wakisema:
"Watengenezaji wa magari wa China wanaenda kwa mwendo wa kasi wa mwanga, kwa kutumia akili ya bandia na teknolojia nyingine za hali ya juu katika magari yao tofauti na teknolojia yoyote iliyopo Marekani. Wanatengeneza magari kwa gharama nafuu ili kupunguza gharama na yaliyo na teknolojia za kisasa na wamepanuka kikamilifu katika masoko ya nje ya China, hili ni tishio lililopo kwetu."
–Jim Farley (Ford CEO)
–Jim Farley (Ford CEO)
”No supply chain in the world is more critical to us than China. We're not in China for low labor costs. In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
–Tim Cook (Apple CEO)
–Tim Cook (Apple CEO)
Kauli za viongozi wa juu wa makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya ni tofauti sana na wanasiasa wao kama Trump na Biden na sera zao dhidi ya China.
Wanasiasa wa nchi za Magharibi wanaongea kisiasa wakati wakuu wa makampuni makubwa duniani wanazungumzia uhalisia. Kwa sasa hauwezi kuikimbia China katika dunia ya kibiashara na kiteknolojia.