Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

hawashauriki na huenda alifanya hivyo
 
Nakubaliana na wewe ila huenda mengine hayaletwi hadharani kwa bahati mbaya. Ni mpango kamili wenye lengo mahususi kwa waliletao, mimi na wewe tunaweza baki kubishana wee kumbe ni lengo haswa. Na huenda sio yeye aliyelileta hadharani japo hawezi kuja kulikana...wasemapo kuna sijui dipu siteti huenda yote haya ni kutoa tahadhari na kusukuma jambo walitakolo.
 
kosa ni;
1. kusambaza barua ya mawasiliano ya kiofisi kwenye vyombo na mitandao.
Hajafanya kosa lolote hapa kwa kufanya hivyo.
Amefanya hivyo kwa nia njema kabisa (endapo kama yeye kweli ndiye aliyesambaza barua hiyo mitandaoni), hii ni ktk kuujulisha umma wote wa Watanzania mahali popote pale walipo duniani kwamba Rais wa nchi amekiuka Katiba ya nchi ambayo aliapa kwa kinywa chake kwamba ataitetea na kuilinda.
 
Serikali ya sasa ni kama ile ya JK. Inawezekana kabisa huyu jaji siye aliyesambaza hiyo barua. Huko ilikotumwa ndiko wameisambaza ili kudhalilisha mamlaka.

Utamlaumu bure huyu jaji ila ujue huu utawala usipojirekebisha utafitinika
Naungana na wewe, huenda kuna kufitiniana huko ndani. Mambo kama haya hupelekea misiba ambayo huleta taharuki mbeleni.
 
Serikali ya sasa ni kama ile ya JK. Inawezekana kabisa huyu jaji siye aliyesambaza hiyo barua. Huko ilikotumwa ndiko wameisambaza ili kudhalilisha mamlaka.

Utamlaumu bure huyu jaji ila ujue huu utawala usipojirekebisha utafitinika
Huyo Jaji atoke hadharani kama sio yeye aliye isambaza barua, kwa sasa sisi wananchi tunajua kuwa yeye kama mwandishi ndiyo source ya barua kusambaa.
yeye asinge andika barua kweli tungesema hajahusika na usmabazaji ila kwakuwa anakiri kuwa yeye ndiye mwandishi wa barua hiyo basi kwa sasa yy ndiye aliyeisambaza.
 
Huyo Jaji atoke hadharani kama sio yeye aliye isambaza barua, kwa sasa sisi wananchi tunajua kuwa yeye kama mwandishi ndiyo source ya barua kusambaa.
Hahahaa... kwanini unasema 'sisi wananchi?' sema 'sisi wengine' maana wengine (kama mimi) sioni unavyoona. Kama mkataba wa DPW umevujishwa, sembuse barua ya jaji? Kama Aziz kasema kuna watu kisutu wanapigiwa simu ya namna ya kuhukumu, bado huoni lolote nchi hii linawezekana!?
 
wacha kutetea makosa, kuwa mkweli, sema kuwa Jaji Mugasha kakosea kwa kusambaza barua ya mawasiliano ya kiofisi kwenye mitandao.

tunataka tabia hii ikomeshwe kwa viongozi.
 
Kukosoa Kitendo cha Rais kumuongezea Jaji Mkuu muda wa kuendelea kuwepo kwenye kiti ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu kwa mamlaka zilizo juu yake.
Sasa km amekiuka KATIBA asiseme watu wengine Bwana, yeye ni msimamizi wa sheria ulitaka akasemee wapi uvunguni kwako ?

Mahakama ni mhimiri unaojitegemea wenyewe hauingiliwi na mihimili mingine km Bunge na Serikali na uwepo wa Mahakama ni kusimamia, kukosoa, kusahihisha na kuangalia utendaji kazi wa sheria zilizopo je zinafuatwa km zilivyowekwa au zinakiukwa ?
 
Huyo jaji ana akili nyingi sana,katiba inabakwa na watawala kwa interest zao,lakini mtu wa kawaida akivunja katiba anafungwa jela maisha.
Hongera kwa jaji mwenye akili zilizokamilika kwa kuweka mambo public.

Sidhani kama ni akili kwa mazingira yetu haya nacho ona anacheza na mazingira ya sasa kwamba Rais ni Mwanamke afu Mzanzibar na tena Muislam ni kama kuna ka wivu hivi

Pia issue ya Bandari watu wameanza ku test kina cha Rais na kwa hasa hoja kama hizo tatu juu, lkn hana sijui akili au nini ni kuona tu atafanywaje? Maana sidhani kama kipindi cha Jiwe kama angethubutu kuonyesha huo ujuaji kwa kutoa kwa changamoto kwa kiti cha Urais

Ndo unaona wana nyanyuka hata kina Tibaijuka kusema wee wakati aliisha kuwa na madudu ya kila aina toka UN mpaka wizarani hapa achia mbali mambo ya Escrow Acc
 
wacha kutetea makosa, kuwa mkweli, sema kuwa Jaji Mugasha kakosea kwa kusambaza barua ya mawasiliano ya kiofisi kwenye mitandao.

tunataka tabia hii ikomeshwe kwa viongozi.
Kukosea wapi we ulitaka afanyeje aje akwambie wewe peke yako ?
 
umesema ukweli bila unafiki.
huo ndio ukweli.
Kitendo hicho cha Jaji ni kutaka kumpanda kichwani Amiri Jeshi Mkuu.
kwakweli hii tafasiri yake ni dharau.
 
wacha kutetea makosa, kuwa mkweli, sema kuwa Jaji Mugasha kakosea kwa kusambaza barua ya mawasiliano ya kiofisi kwenye mitandao.

tunataka tabia hii ikomeshwe kwa viongozi.
Kwani aliyeandikiwa huoni hata yeye anaweza kuivujisha!? Akija sema sio yeye aliyevujisha, itabadilisha kitu gani? Hizi habari kuja humu kwangu naona ni mikakati fulani hivi, suala la nani anakosea nani anapatia nyakati hizi sioni kama zina mantiki. Tujue tu hazijaja kwa bahati mbaya..huku kuna DPW (wapo wasemao Rais kadanganywa), ghafla linakuja hili la kikatiba tena(wapo wasemao Rais anazidi kudanganywa). Huoni ni kama mkakati MAALUMU dhidi ya kiti?
 
Mkuu usijifiche kwenye kazi za watu. Hayo mambo na mkulima anaye pambana kutafuta mbolea wapi na wapi. Je unajuaje kama alisha shauri hapo Mwanzo. Huo ndio uhuru wa kutoa mawazo, huoni sasa mimi na wewe tumehabarishwa?
 
Hoja dhaifu sana. Kwani kuna kosa gani amefanya kuandika hiyo barua?
 
umesema ukweli bila unafiki.
huo ndio ukweli.
Kitendo hicho cha Jaji ni kutaka kumpanda kichwani Amiri Jeshi Mkuu.
kwakweli hii tafasiri yake ni dharau.
Mahakama ni Mhimiri unaojitegemea unaweza kukosoa pale sheria inapokiukwa haijarishi ni publicly au privately Ila UJUMBE umefika
 
Akimsifu hadharani ni sawa lakini akimkosoa ni tatizo?Jaribu kufikiri zaidi ya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…