Kitendo cha Jaji Mugasha kukosoa mamlaka hadharani ni utovu wa nidhamu, sio ushujaa

Usichokijua ni kuwa MAJAJI wana viapo vya kuilinda na kuitetea katiba ya nchi.....

Mh.Jaji Mugasha yuko sahihi.....

Hii inatoa picha kuwa Rais tuliyenaye ni mwanademokrasia haswa.....

Majaji wanalijua hilo....

Jaji Mugasha analijua hilo.....

#SiempreJMT[emoji120]
#SiempreSSH[emoji2956]
 
Kitendo alichofanya Jaji ni cha kijasiri na kizuri mno bravo, tunahitaji vichwa kama hiki kututoa tulikokwama, hbr ya nani kasambaza hiyo wanajua wao katoa dukuduku lake na msg sent clear n loud
 
Akimsifu hadharani ni sawa lakini akimkosoa ni tatizo?Jaribu kufikiri zaidi ya hapo.
Rais wetu ni mtu muungwana sana, na yeye mwenye alisha tamka kuwa yuko tayari kukosolewa kwa njia ya staha.
lakini kwenye jambo hili tatizo sio kukosoa au kutoa kushauri bali njia iliyo tumika kutoa ushauri ndio tatizo.
 
Nchi inaongozwa kidemokrasia....

Rais SSH ni mwanademokrasia haswa[emoji2956]

Majaji wanalijua hilo....

Kinyume na hicho ,Jaji Mugasha asingeweza kutupa msimamo wake wa kitaaluma[emoji120]

#SiempreJMT[emoji120]
 
Hata jiwe alikuwa anasemwa hasa na wapinzani wake wa kisiasa.
Mliomuogopa jiwe poleni sana sasa zungumzeni hayupo tena.
 
angeanza kusema na kiongozi wake wa Mhimili sio kusambaza mabarua kila kona!!!
Mkuu unajuaje kama hakushauri? Ndio maana alipo ona ushauri wake umepuuzwa ndipo akaamya kuweka ushauri wake katika maandishi kama kumbukumbu! Sasa Wewe Mkulima mwenzangu unajua mambo ya kumbukumbu katika Ofisi za Serikali
 
Mkuu huyu mtu ni wa ajabu sana; anasema yeye ni Mkulima lakini hapa anashupaza shingo kujifanya anajua kazi za mihimili ya dola. Aidha anajua mambo ya siri sana, siri na ya kawaida ya mawasiliano ya Serikali. Ndugu Mkulima weka hapa nakala ya hiyo barua tuione ili tuielewe vizuri
 
Hakuna utovu wa nidhamu kusema makosa ya mtawala hadharani...

Wewe ulitaka asemee makosa haya gizani mafichoni? Huo ndo ungekuwa utovu wa nidhamu Kwa 100% bila shaka..!!

By the way, utovu mkubwa wa nidhamu ni ule wa Rais Samia Suluhu Hassan na Wazanzibari wenzake kuamua kuuza bandari za bahari na maziwa makuu ya Tanganyika kwa waarabu wa DP World - Dubai hadharani mchana kweupe!

Huu ndo utovu nidhamu na kutudharau Watanganyika...
 
Muondoeni kwenye nafasi yake kama mmechukia.
 
Mimi Mkulima nipo ipalamwa, nimeiona barua Ya Jaji Mugasha ikionyeshwa kwenye kipindi cha 360 clouds tv tarehe 28/6/2023 saa mbili asubuhi leo.
hakuna siri barua hiyo iko kwenye vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii.

barua hiyo imesambazwa kila kona, hakuna siri.
 
Je kufanya hivyo ni kosa kisheria?
 
Honestly jaji mugasha kazingua kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe wake siyo ile aliyoitumia ambayo imelenga kudhalilisha muhimili na kudhalilisha mamlaka ya uteuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…