Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Sioni uhuni wowote hapo,huo mnyoo Ndio unaofanya aishi hapa mjini kwa kipato halali,Ndio muonekano wake yeye kama msanii. Kama ni kosa basi hata wale wanajeshi wanaovaa mavazi ya kijeshi kanisani siku ya ndoa wanafanya makosa.
 
mimi mwenyewe rc na sijatoa zaka muda sasa,kwanini niwe na tatizo na Joti ambaye hiyo staili yake ya nywele inamfanya alipe 1/10 kila mwezi?
Acha hoja nyepesi

Kama yuko sahihi asihukumiwe

Kama ni kosa halimfanyi Mungu kupokea rushwa eti ili aendelee kutoa zaka

Sijafundishwa hivyo na katekista wangu
 
nmekusoma mkuu,lkn yapi maoni yako hapo?
Me simuhukumu

Huenda kwa alivyofanya itawavuta wengine kuja kanisani kumjua Mungu ila huenda akabaki kuwa kibao cha kuelekeza njia wakati sehemu yenyewe haijui wala hatafika kamwe

Tumwache atajihukumu mwenyewe akitoka hanemuni
 
Acha ufarisayo
Joti yupo sawa.
Huna exposure, Hujui kitu
 
The first thing to ask what is the church, if we can understand then we can answer the question. Not all congregation mentioning God and Jesus is the church!
 
joti kazi yake ni mchekeshaji.. hicho kiduku kinakufanya ucheke tu kabla hajaanza vituko...

sasa akikinyoa atakula nini.. wakati baada ya harusi anarudi kazini...
 
Kama kuna makanisa yanafungisha ndoa mashoga kwanini isiwe Kiduku ???
 
Sio tu kunyoa kihuni ht vle anavyojifanyaga mwanamke tena shangingi lilliloshndkana ni sawa?
 
Soma kitabu cha Wakorintho, waraka za Mtume Paulo kuhusu mavazi, kusuka na muonekano kwa ujumla mbele za Mungu.
Kuhusu kunyoa vibaya kama mtindo wa denge umekatazwa soma , Mambo ya Walawi 19:27.
Ndoa ni jambo Takatifu mbele za Mungu halipaswi kuchukuliwa kwa mizaha, ingalikuwa inaruhusiwa kukaa vyovyote mbele ya Kanisa basi hakukuwa na haja hiyo ndoa iingie Kanisani ili ifungwe wangeweza kufungia hata majumbani kwao.
Kuna code of ethics zinazotawala ktk mambo ya dini.
Mambo ya walawi yalikuwa yanawahusu wana wa Israel na si watu wa mataifa, ndio maana alikuja Masihi kuukomboa ulimwengu wote wakiwemo watu wa mataifa, hizo sheria zote zilihusu watu wa Israel na si wewe
 
Back
Top Bottom