Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

"Kunyoa kiduku sio uhuni ila kuna wahuni wananyoa viduku" whatch out
 
Sio sahihi. Kuna mstari wa maandiko umekataza unyoaji wa hivyo. Nikiukumbuka nitauleta hapa.
 
HIVI ANAYEAMUA KUWA MTINDO SAHIHI WA KUNYOA NYWELE NI NANI.HAYO MAWIGI YA MAITI. MARASTA, VIPARA(AU VINAITWA KWA KINYOZI TAKO).MTINDO WA JOTI WAMASAI WAMEKUWA NAO MUDA MREFU KWA HIYO NI WAHUNI
View attachment 619281
Satanical appearances.. Kuna jamii ambazo kwa jinsi zinavyoharibu miili yao ni kielelezo tosha cha uwepo wa shetani. Huwezi kutoboa toboa mwili au kuweka mitindo ya nywele ya kishetani ukabaki kuwa kielelezo cha mfano wa Mungu
 
Satanical appearances.. Kuna jamii ambazo kwa jinsi zinavyoharibu miili yao ni kielelezo tosha cha uwepo wa shetani. Huwezi kutoboa toboa mwili au kuweka mitindo ya nywele ya kishetani ukabaki kuwa kielelezo cha mfano wa Mungu
kwahiyo wamasai wote ni mashetani!!! huu ni ukoloni mamboleo kuhusudu vitu vya waarabu na wazungu tu
 
Hiko kiduku ni sehemu ya ajira yake... Biblia imekataza kiduku?
 
Tuondokane na fikra za kikoloni za kukataa mitindo yetu ya asili ya mavazi na urembo. Mzungu akienda ofisi ya serikali na nywele ndefu za kiume ni ruksa ila mbongo akienda na Afro ni mhuni...tubadilike
 
Inategemea aina ya dhehebu, kuna yatoayo mafnzo kabla ya ndoa kuna yayojali micjnango ya kifedha ya mhusika,ila kamwe hakuna kanisa linaloruhusu hayo ya Jot.
 
Mambo ya Walawi 19:27

Law 19:27
Screenshot_20171028-211139.jpg
 
Mambo ya walawi yalikuwa yanawahusu wana wa Israel na si watu wa mataifa, ndio maana alikuja Masihi kuukomboa ulimwengu wote wakiwemo watu wa mataifa, hizo sheria zote zilihusu watu wa Israel na si wewe
Unataka kutuambia amri alizopewa Musa kule mlimani nowadays hazituhusu! Yaani hakuna haja ya kuwaheshimu wazazi! Ni kutamani kwa kwenda mbele, kuua sio kosa?

Wala hatutakiwi kumuabudu Mungu siku ya Sabato si ndio?

Una maana kulitaja jina la bwana Mungu wetu ni ruksa si eti?

Wewe ni wakuogopa sana.
 
Back
Top Bottom