Kitendo cha Kanisa kufungisha ndoa ya Joti huku akiwa amenyoa mtindo wa kihuni ni sahihi?

Nimeipenda hii mada..,ila.imenikuta bize ningependa nimuelimishe mwenye uzi,kwa sasa naiweka kiporo.
 
Kama benki ya mkombozi ya kanisa katoliki ilitakatisha pesa za escrow unategemea nini?
 
Nani kakwambia huu mtindo wa kihuniii tuanze hapoooo
 
....hata kumning'iniza Yesu na nepi msalabani ule pia ni uhuni !
 
Mavazi, muonekano sio ishu ya kuwazuia kugunga ndoa hasa ukizingatia joti ni msanii, mbona maofisa wa jeshi huwa wanafunga ndoa huku wakiwa wamevaa sare za kijeshi (OG) mbona hamsemi. Acheni watu wajipatie neema na baraka za Mungu
 
Binafsi siwezi kusema amekosea au hajakosea ila nimachoweza kusema ni kwamba kila kitu na mahapa pake, kiduku kanisa la kikiristo si sahihi hata kidogo, haya makanisa teletewa wazungu na baadhi ya watu tukayakubali, kama tumeyakubali basi tujaribu kutembelea kwenye misingi yake, tukiwa kwenye masuala mengine na kwenyewe tuzingatie matakwa, mfn, Mambo ya Walawi 9:28 imekataza kujichora miili (tatoo) lakini mila za kiafrika hazikatazi japo kwa sasa tunajichora zile za kizungu na si za kiafrika tena, hakika kizazi cha sasa hivi tumechangaya mambo sana, hatueleweki tena kama tunawaiga wazungu au tuko kwa wafrika, sifa , tamaa, njaa za pesa , uzinzi, ulozi, ulafi, nk vimetutawala, viongozi wa dini hawaoni wala hawasikii tena, mila na desturi nazo tumezipiga teke tumebaki tunaelea tu hatuna pa kushika ila penye matakwa binafsi ndo tunashika.
 
weka andiko kiBiblia kuthibitisha huo mtindo wa kihuni! Hayo ni mapokeo tu ndugu. Kwa USA na jamaica unaweza kukutana na pastor amesuka dread lakini kwa Tanzania ni ishara ya uhuni, sasa mfano kama huu una uhusiano wowote na andiko la biblia?
Sio dread tu Mkuu wengine wamechora matatooo na kutoboa miili yao na kuweka vipini kibao. Hakuna mnyoo wa kihumi pale wabongo tu, tumezoea kujadili upuuzi.
 
Mtoa mada sijui unajua kuwa Mr Blue alifungishwa ndoa na sheikh huku akiwa amevaa hereni
 
Kwa ninavyojua mavazi mitindo ya nywele ni masula ya utamaduni wa mahali.
Hatuwezi leo kuvaa makanzu yale walokua wanavaa mashariki ya kati na kufuga midevu eti kuwaiga wao kwa kuwa biblia iliandikwa katika mazingira yao.
Ukienda Asia wakristo wa kule wanamavazi yao na mitindo yao ya nywele.
Ukija Afrika tuna mitindo yetu kulingana na jamii zetu.
Mavazi anayovaa mkristo pale London akiyavaa mswahili huko Mpitimbi ataonekana amekosea si kwasababu Mungu hataki ila itamaduni na jamii haitaki.
Tutofautishe masula ya Mungu na masuala ya utamaduni wa eneo husika.
Kuna mambo kwenye Biblia kama vyakula, vinywaji na hata mavazi yalielezwa kulingana na mazingira na utamaduni wa eneo husika, unapaswa kujua upi ni utamaduni wa eneo husika yapi ni Mambo ya Mungu.
Using'ang'ane kula mikate isiyotiwa chachu huku kwetu hatuwezi wala kunywa divai si utamaduni wetu sie wetu ulanzi ugali na komoni.
Hata kunyoa kuna mitindo imepita mingi sana, mavazi suruali au sketi unayovaa leo sio iliyovaliwa miaka kadhaa iliyopita. Ukifunga ndoa suti utakayovaa leo sio ambayo ungevaa miaka ya 60 mtindo umepita huo.
Kuna kasumba tu mambo yafanywayo na vijana nyakati zote kuaonekana ni mabaya, utasikia vijana wa siku hizi hata wa miaka hiyo waliambiwa hivyo pia. Vijana wawe vijana na wazee wawe wazee
Mungu atusaidie tusikalili na kukalilishwa maandiko tuyaelewe vyema na kuyaishi.
Hata wanaoonekana wakosefu Yesu ataingia kwao, kama alivyoingia kwa kahaba na waliojihisi ni wema sana walimshangaa.
Huenda huyu aliyenyoa kiduku akaiona Mbingu kwa maana walio na njaa anawalisha, walio uchi anawavisha n.k na hayo ndio maswali yanayohitaji majibu ili kuingia Mbinguni
Tusitupe lulu zetu kwa Nguruwe
 
Biblia ingekuwa ngumu ivo, hata mtu mmoja asingeenda mbinguni, unasemea ilo denge, ukienda nchi nyingine na tamaduni nyingine Hilo ni traditional yao wala sio denge.
Mungu atuongoze tusiwe watumwa wa dini Bali neno la Mungu Liwe kioo, kibao cha kutuongoza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…