Kitendo cha kumpa Mbowe privilege kuwa hastahili kushtakiwa kwa ugaidi si sawa kisheria na ni kinyume na dhana ya "Equality before the law"

Tonatofautiana katika mstari mwembamba sana.Unakereka na watu kusema "Mbowe sio gaidi".Ungetumia muda kidogo kutafakari kwa nini watu waseme hivyo.Kwanza,huyu ni public figure ana wapenzi na wafuasi na huwezi kuzuia mapenzi yao.Kama unaamini katika kila mtu hasa kosa mpaka itakapothibitishwa basi ungekaa kimya tu.Hiki kitendo cha kuwaona wapenzi wake wana makosa ni tayari umeshachukua upande.All in all nimefurahi kwa uandishi wako!
 
Shujaa mwendazako embu tutolee chuki zako hapa kwani ni mmoja wa timu bambikizi na kila mara unakuja kuhubiri chuki zako dhidi ya wale mnaowanyanyasa.
 
Hapo Moshi mjini kwenye kuta za hospitali ya Mawezi kuna maandishi makubwa mekundu "Mbowe Sio Gadi" na umbali mchache tu kutoka makao makuu ya polisi mkoa, hakuna anayesumbukliwa kuhusu maandishi yale, yamedharauliwa na watu wake wa damu kabisa huku wakiendelea na shughuli za kiuchumi pembeni mwa barabara kama kawaida.

Kitendo cha kuweka maandishi hayo hadharani huku wahusika wakijua kesi ya msingi iko mahakamani ni kuingilia na kuielekeza mahakama cha kufanya kinyume na sheria.
 
Sasa ndugu intel justice,mbona hakuna uwiano wa uyaaminiyo ,mawazo yako na uhalisia wa jina na matendo yenu.
 
Bro ila hata Equality Before the Law definition yake lazima unakili Wikipedia?
 
Kama wote ni sawa mbele ya sheria sasa kwa nini tumemuacha Magufuli amekufa bila kupelekwa mahakamani akajibu tuhuma za mauaji, dhuluma na utekaji?

Kuna watu hadi leo hakuna ajuaye waliko, mara inasemekana aliamuru wauwawe kisha wakatupwa baharini. Ila yake tunamuachia Mungu atamalizana naye.
 
Kesi ya Kijinga mahakama wanaijuaje. Kwani kesi ngapi CHADEMA wameshinda?

Jaji/Hakimu anareject vip kesi iliyoletwa kwake?

Kwa nini wareject kesi ya mbowe na si ya babu seya?
Rais aliwaambia polisi wafute kesi za kubambika na wamefuta.

Huu ni udhaifu mkubwa kisheria mpaka walinda haki za watu ndio wanakuwa wa kwanza kuzivunja.

Tafakari kama kuna maboresho yoyote , zaidi ya kauli za kisiasa
 
..Na kitendo cha kuwashtaki Chadema, huku Polisi wakiwavumilia CCM kwa makosa hayohayo, ni kinyume na dhana ya " equality before the law. "
CCM kuna aliyetuhumiwa kwa ugaidi mkuu ?

Usitoke nje ya Mada, mfano huwezi kuhalalisha jinai kwa hoja yako
 
Equality before the law? jee wewe na Majaliwa, Ndugai au Tulia unadhani mko equal?
Ukilipatia jibu sahihi swali hilo utagundua kuwa mada yako imepotea mazima

Waambie wafanye jinai wagundulike waone.
 

Unataka wakusanyike kuelezea kuwa Mbowe siyo Gaidi au unamaanisha nini?

Usije ukawa unatoka nje ya Hoja
 
CCM kuna aliyetuhumiwa kwa ugaidi mkuu ?

Usitoke nje ya Mada, mfano huwezi kuhalalisha jinai kwa hoja yako

..wanaokamatwa ni wapinzani peke yao, CCM huwa hawakamatwi.

..Na wewe usihalalishe dhuluma na double standards kwa hoja yako.
 
Hiyo ni kwa Mbowe je kuna watanzania wangapi wako mahabusu aua jela kwa kesi za kusingiziwa, kukamatwa kwao hakukufuata sheria na taratibu

Kina nani hao, unawajua au unasema kwa hisia...

Kesi ya kusingiziwa , unamaanisha mahakama inawahukumu huku wamesingiziwa?

Siyo mahakama ilimuachia huru MDUDE CHADEMA NA KUSEMA ALIKUWA FABRICATED NA JINAI ?

Au leo mnakosa imani na mahakama tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…