Kitendo cha kumpa Mbowe privilege kuwa hastahili kushtakiwa kwa ugaidi si sawa kisheria na ni kinyume na dhana ya "Equality before the law"

Watanzania sio wajinga wanajua Mbowe toka akiwa mdogo Azania . Wanajua Mbowe kuliko viongozi wote wa CCM ugaidi sio ndoto ya kuamkia siku moja
 
Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
 
Kina nani hao, unawajua au unasema kwa hisia...

Kesi ya kusingiziwa , unamaanisha mahakama inawahukumu huku wamesingiziwa?

Siyo mahakama ilimuachia huru MDUDE CHADEMA NA KUSEMA ALIKUWA FABRICATED NA JINAI ?

Au leo mnakosa imani na mahakama tena?

..Mahakama pia iliwafunga kwa dhuluma Joseph Mbilinyi, Peter Lijualikali, Halima Mdee, Peter Msigwa, na wengine.

..Sasa hebu tutajie mwana-CCM yupi au wangapi waliwahi kufungwa kimakosa kwa mashtaka ya kisiasa.
 
Watanzania sio wajinga wanajua Mbowe toka akiwa mdogo Azania . Wanajua Mbowe kuliko viongozi wote wa CCM ugaidi sio ndoto ya kuamkia siku moja

WANAOLETA HIZI VURUGU NI WATANZANIA WOTE AU NI KIKUNDI CHA WAFUASI WA MBOWE?
 
..Mahakama pia iliwafunga kwa dhuluma Joseph Mbilinyi, Peter Lijualikali, Halima Mdee, Peter Msigwa, na wengine.

..Sasa hebu tutajie mwana-CCM yupi au wangapi waliwahi kufungwa kimakosa kwa mashtaka ya kisiasa.

Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.
 
Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
Acha kujiosha wewe na chuki zako unafahamika,yaweza kuwa were ndiye mtoa pendekezo la ubambikizi wa ugaidi,na wazo la manyanyaso kwa wenye mawazo mbadala dhidi ya wanakijani.
 
Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
Hivi kweli unaweza kuyalinganisha matukio ya Sabaya na Mbowe?Matukio ya sabaya yalikuwa so obvious.Anyway ni nani anayetafsri ugaidi?Mandela alikuwa gaidi katika macho ya makaburu the same Mbowe anaweza kuwa gaidi katika macho ya CCM na serikali yake na si mashabiki na wanachama wa chama chake!!
 
Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.

..Moja ya mashtaka dhidi ya Mbowe, Mdee, Msigwa,etc ilikuwa ni kusababisha kifo cha Aquilina.

..Na walioanza kusema kuna hila ktk kesi ile ni Chadema.

..Mahakama Kuu ilikubaliana na Rufani ya Chadema na kutupilia mbali hukumu ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
..Na kitendo cha kuwashtaki Chadema, huku Polisi wakiwavumilia CCM kwa makosa hayohayo, ni kinyume na dhana ya " equality before the law. "
Ha ha aaaaa sisiemu bwana pasua kichwa ,,
 
Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.

..Nionyeshe tukio moja ambapo mkutano wa CCM umepigwa mabomu ya machozi, polisi wametumia mbwa dhidi ya wana-CCM, au wamefyatua risasi za moto dhidi ya kiongozi au mwanachama wa CCM.
 
Acha kujiosha wewe na chuki zako unafahamika,yaweza kuwa were ndiye mtoa pendekezo la ubambikizi wa ugaidi,na wazo la manyanyaso kwa wenye mawazo mbadala dhidi ya wanakijani.

Mhemko huo
 
Acha ujinga mara moja moja tumia akili yako.

Watanzania wanaendelea na mambo yao, hawahangaiki na mambo ya Mbowe wala Sabaya. Ni kikundi tu ndo kinaingilia mambo ya mahakama.
Hata huyo Samia aliongelea siku moja tu na amekaa kimya.

Chadema kila kukicha kuchora nyumba na kuta za watu
 
Unamaanisha mahakama yetu ni ya KIKABURU ?

Ila mkishinda kesi mnaisifia na kuitukuza.

So funny
 
Sasa mahakama ilitupa kisheria baada ya kutafsiri sheria au baada ya CHADEMA kuchorachora kwenye ukuta?
 
..Nionyeshe tukio moja ambapo mkutano wa CCM umepigwa mabomu ya machozi, polisi wametumia mbwa dhidi ya wana-CCM, au wamefyatua risasi za moto dhidi ya kiongozi au mwanachama wa CCM.

Hii ndo hoja ya kusema MBOWE SIYO GAIDI .

Mbona umehama na kukimbilia kwenye Mabomu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…