Kitendo cha kumpa Mbowe privilege kuwa hastahili kushtakiwa kwa ugaidi si sawa kisheria na ni kinyume na dhana ya "Equality before the law"

Kitendo cha kumpa Mbowe privilege kuwa hastahili kushtakiwa kwa ugaidi si sawa kisheria na ni kinyume na dhana ya "Equality before the law"

Kwa elimu yetu ndogo ya uraia tulisomasoma kidogo kuhusu Equality Before the Law (The principle which requires a systematic rule of law that observes due process to provide equal justice, and requires equal protection ensuring that no individual nor group of individuals be privileged over others by the law.). Sitaki kwenda mbali nabaki hapo kwenye Rule of Law na pia kwenye "nor group of individuals be privileged over others"

Si kwamba nami mathibitisha kuwa Mbowe ni gaidi La hasha lakini hizi harakati za vyuoni ambazo mnazileta mpaka ukubwani siyo sawa na mnasumbua Taifa. Ni wazi kuwa hata ninyi hamuheshimu utawala wa Sheria . Utawala gani wa Sheria ambao mnaulilia sasa? Sote tunatambua kuwa "no one is guilty unless proven by the court" . Sasa mnasema yeye siyo Guilty tujiulize je ninyi ni mahakama? . Lakini mnavyokazania kwamba Mbowe si gaidi kwani nani amesema Mbowe ni gaidi ?.

Kitendo ch kumpa Mbowe privilege kuwa hastahili kushtakiwa kwa ugaidi si sawa kisheria na ni kinyume na dhana ya "Equality before the law" lakini pia tujiulize nani anajua Nyendo zote za Mbowe kiasi cha kumtetea namna hii. Ni kweli inafikirisha kuwa ukaribu wa Mbowe (kutokana na nafasi yake) kwa Viongozi mbalimbali na tuhuma zake ni kama haziingii akilini lakini kwani treason cases nyingi zinatokea mbali?, masterminds wa ugaidi na treasons wanatokaga mbali?

Kuchafua Kuta za watu haiwezi kuwa ushaidi wa Makosa ya Mbowe, Mpaka anashutumiwa na kukamatwa manake kuna Dalili za Makosa ya Ugaidi. Mnapaswa kutafuta Ushaidi wakisheria utkaaomtoa kwenye makosa au kusubiri ushahidi wa upande wa mashtake ili mpate kutengeneza hizo reasonable doubts na kumnasua. Lakini si kwa huu utopolo wakuchafua Kuta za Watu na Kuandamana kwenda Mahakamani huku mkichafua mitandao ya kijamii kwa jambo ambalo liko kwenye meza za kisheria.

Mnapaswa kuwa mfano wa vita ya katiba mnayopigania kwa maana ya kuwa "All people are equal under the law" . Kwani Freeman ni mtu wa kwanza kushtakiwa kwa makosa hayo au kwamba watanzania wengine wanaoshtakiwa ni wapumbavu?. Je Mnatufundisha nini mkishika dola. Viongozi wenu wa Chama wataguswa kweli na sheria?. Mbowe akiwa waziri mkuu akifanya kosa ataguswa kweli?. Mnawasema CCM kila siku kuwa hawaheshimu sheria lakini nanyi mnaonesha kuwa ni walewale. What went wrong?, sasa si ni bora hata ya ACT mnaowadharau!

Mnalaumu viongozi kuwa wanaingilia uhuru wa mahakama, Vipi hiki mnachokifanya ninyi siyo kuingilia uhuru wa mahakama?. Mlipaswa kupiga kelele za "JUSICE FOR MBOWE" na si kelele za "MBOWE SIYO GAIDI" na kuchorachora kuta za watu ambapo ni makosa pia kisheria.

Kesi ya Mbowe ni sensitive ndo maana mawakili waki HAWALIPUKI NA KAULI za hovyohovyo bali wanasubiri facts waanza kucounter na wala hakuwaambia mchorechore nyumba za na kuta za watu.

GROW UP CDM
View attachment 1899796

Watanzania sio wajinga wanajua Mbowe toka akiwa mdogo Azania . Wanajua Mbowe kuliko viongozi wote wa CCM ugaidi sio ndoto ya kuamkia siku moja
 
Tonatofautiana katika mstari mwembamba sana.Unakereka na watu kusema "Mbowe sio gaidi".Ungetumia muda kidogo kutafakari kwa nini watu waseme hivyo.Kwanza,huyu ni public figure ana wapenzi na wafuasi na huwezi kuzuia mapenzi yao.Kama unaamini katika kila mtu hasa kosa mpaka itakapothibitishwa basi ungekaa kimya tu.Hiki kitendo cha kuwaona wapenzi wake wana makosa ni tayari umeshachukua upande.All in all nimefurahi kwa uandishi wako!

Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
 
Kina nani hao, unawajua au unasema kwa hisia...

Kesi ya kusingiziwa , unamaanisha mahakama inawahukumu huku wamesingiziwa?

Siyo mahakama ilimuachia huru MDUDE CHADEMA NA KUSEMA ALIKUWA FABRICATED NA JINAI ?

Au leo mnakosa imani na mahakama tena?

..Mahakama pia iliwafunga kwa dhuluma Joseph Mbilinyi, Peter Lijualikali, Halima Mdee, Peter Msigwa, na wengine.

..Sasa hebu tutajie mwana-CCM yupi au wangapi waliwahi kufungwa kimakosa kwa mashtaka ya kisiasa.
 
Watanzania sio wajinga wanajua Mbowe toka akiwa mdogo Azania . Wanajua Mbowe kuliko viongozi wote wa CCM ugaidi sio ndoto ya kuamkia siku moja

WANAOLETA HIZI VURUGU NI WATANZANIA WOTE AU NI KIKUNDI CHA WAFUASI WA MBOWE?
 
..Mahakama pia iliwafunga kwa dhuluma Joseph Mbilinyi, Peter Lijualikali, Halima Mdee, Peter Msigwa, na wengine.

..Sasa hebu tutajie mwana-CCM yupi au wangapi waliwahi kufungwa kimakosa kwa mashtaka ya kisiasa.

Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.
 
Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
Acha kujiosha wewe na chuki zako unafahamika,yaweza kuwa were ndiye mtoa pendekezo la ubambikizi wa ugaidi,na wazo la manyanyaso kwa wenye mawazo mbadala dhidi ya wanakijani.
 
Hata CCM wenyewe huwasikii wakisema Sabaya siyo Jambazi. Why?

Lakini pia Public figure hawezi kuwa gaidi?
Hivi kweli unaweza kuyalinganisha matukio ya Sabaya na Mbowe?Matukio ya sabaya yalikuwa so obvious.Anyway ni nani anayetafsri ugaidi?Mandela alikuwa gaidi katika macho ya makaburu the same Mbowe anaweza kuwa gaidi katika macho ya CCM na serikali yake na si mashabiki na wanachama wa chama chake!!
 
Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.

..Moja ya mashtaka dhidi ya Mbowe, Mdee, Msigwa,etc ilikuwa ni kusababisha kifo cha Aquilina.

..Na walioanza kusema kuna hila ktk kesi ile ni Chadema.

..Mahakama Kuu ilikubaliana na Rufani ya Chadema na kutupilia mbali hukumu ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 
Mahakama iliwafunga kwa dhuluma?

wewe nimekuelewa mkuu kuwa Viongozi wa Chadema wako juu ya sheria.

Nimekuelewa.

..Nionyeshe tukio moja ambapo mkutano wa CCM umepigwa mabomu ya machozi, polisi wametumia mbwa dhidi ya wana-CCM, au wamefyatua risasi za moto dhidi ya kiongozi au mwanachama wa CCM.
 
Acha ujinga mara moja moja tumia akili yako.

Watanzania wanaendelea na mambo yao, hawahangaiki na mambo ya Mbowe wala Sabaya. Ni kikundi tu ndo kinaingilia mambo ya mahakama.
Hata huyo Samia aliongelea siku moja tu na amekaa kimya.

Chadema kila kukicha kuchora nyumba na kuta za watu
 
Hivi kweli unaweza kuyalinganisha matukio ya Sabaya na Mbowe?Matukio ya sabaya yalikuwa so obvious.Anyway ni nani anayetafsri ugaidi?Mandela alikuwa gaidi katika macho ya makaburu the same Mbowe anaweza kuwa gaidi katika macho ya CCM na serikali yake na si mashabiki na wanachama wa chama chake!!

Unamaanisha mahakama yetu ni ya KIKABURU ?

Ila mkishinda kesi mnaisifia na kuitukuza.

So funny
 
..Moja ya mashtaka dhidi ya Mbowe, Mdee, Msigwa,etc ilikuwa ni kusababisha kifo cha Aquilina.

..Na walioanza kusema kuna hila ktk kesi ile ni Chadema.

..Mahakama Kuu ilikubaliana na Rufani ya Chadema na kutupilia mbali hukumu ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Sasa mahakama ilitupa kisheria baada ya kutafsiri sheria au baada ya CHADEMA kuchorachora kwenye ukuta?
 
..Nionyeshe tukio moja ambapo mkutano wa CCM umepigwa mabomu ya machozi, polisi wametumia mbwa dhidi ya wana-CCM, au wamefyatua risasi za moto dhidi ya kiongozi au mwanachama wa CCM.

Hii ndo hoja ya kusema MBOWE SIYO GAIDI .

Mbona umehama na kukimbilia kwenye Mabomu ?
 
Back
Top Bottom