Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya

Kitendo cha Lema na Familia yake kupewa Asylum Canada kinaashiria Taifa limeanza kutengeneza wakimbizi wa kisiasa, jambo ambalo halina afya

Nyie chadema mnatuita sie wa vijijini mafala? [emoji848]

Mimi sio msemaji wa cdm usichanganye maoni yangu na cdm. Nyie ni Mafala kidogo sasa, kama mnalima kwa gharama zenu na kukutana na mateso yote, huku hamna barabara nzuri, maji safi, huduma mbovu za afya nk, na bado mnawashabikia wanaowapangia bei duni za mazao yenu, huku mkibaki masikini wa kutupwa kuna ufala kama huo?
 
Hahahaaaa! Ameenda kula bure no stress!
Maisha ya wakimbizi sio ya kuku kwa mrija. Atapewa vibali vya kuishi vyenye masharti kuwa asirudi tena nchini mwao. Siku akirudi nchini mwao ukimbizi wake unaisha maana ni ishara kuwa huko kwao ni salama. Itabidi atafute kazi afanye. Na uraia wake hapa bongo sijui anakuwa amejivua?
 
Mimi sio msemaji wa cdm usichanganye maoni yangu na cdm. Nyie ni Mafala kidogo sasa, kama mnalima kwa gharama zenu na kukutana na mateso yote, huku hamna barabara nzuri, maji safi, huduma mbovu za afya nk, na bado mnawashabikia wanaowapangia bei duni za mazao yenu, huku mkibaki masikini wa kutupwa kuna ufala kama huo?
Huyo Lissu angefanya vijiji viwe mjini? Una mawazo ya kiboya
 
Huyo Lissu angefanya vijiji viwe mjini? Una mawazo ya kiboya

Angewapa uhuru wa kuuza mazao yao watakalo, na kwa bei inayolingana na dhoruba ya kazi yao.
 
Ni ujinga huo, wala hakuna la maana hapo! Mtu mzima unaamua kujipeleka utumwani wewe pamoja na familia yako! Watoto wake watapoteza mengi hapa duniani, Kizazi cha tatu cha Lema ndicho kitakuja kuinjoi maisha huko kwani ujinga wa Babu yao mzaa Baba au Mama ( ambaye ni Lema wa sasa) wa kukimbia Nchi yake kwa sababu za kutunga zitakuwa zime-fade away!
Umecomment kwa chuki
 
Amecheza karata vizuri, angebaki huku angekula nini? Alishafulia maisha yangekuwa magumu.
Angepewa hata uteuzi.Si unaona Zitto kaufyata.
Ila Watanzania sio raia wa kuwachukulia serious sana.Waangalie familia zao tu.Mi nashauri pale waliposhikilia akina Halima wasipaache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usanii tu, nani amuue? Kwa threat gani aliyonayo kwa taifa? Mbona wapinzani wengine hawajauliwa hadi sasa hivi? Yeye ana nini cha ziada kuliko Mbowe, sugu , mnyika na wengine wengi ambao hawajakimbia nchi?

Ule msemo wake "hakuna kitu kibaya kama uoga " Leo imekuaje? Hana lolote huyo alikuwa anatafuta maisha mteremko ameshayapata atulie huko huko.
Lissu alikuwa na tishio lipi hadi mkamtenda hivo.
 
Na wewe utaendelea kubaki bongo land ukitamani maisha yake na usiyapate. Dah maisha haya
Sitamani maisha yake bali natamani maisha bora. Mimi hapa nilipo nina maisha ya kuridhisha, hivyo sina dhiki ya hivyo.
 
Back
Top Bottom