Kitendo cha Maaskofu wa TEC kuomba NOVENA na Rais kukimbilia kikao cha Maimam ni kuligawa Taifa kidini

Kwenye swala la kuungwa mkono na waislam fanya tafiti tofauttisha uislam iman na viongozi wake uislam ni dini inayozungumza haki
Hao viongozi wake na waumini wa mlengo wa hovyo ndio wanaoipaka matope hiyo dini; ndiyo maana mara nyingi inakuwa vigumu kutenganisha mchanganyiko huo.

Kama ilivyo, katika mambo mengine yote ya kimakundi, kama ukabila na sifa nyingine nyingi; siku zote silaumu kila mtu katika makundi hayo kijumlajumla. Katika kila kundi kuna watu wasiokubaliana na ubaguzi wa watu wengine kwa misingi ya kikabila, kidini, nakadhalika.

Kwa hiyo nisome vizuri, sijahukumu uislam kijumla, ila hivyo vikundi vinavyoipaka matope dini hiyo.
 
Hili jambo niliwaza hivyo hivyo Jana ila nilikuwa sijapata namna nzuri ya kuwasilisha hapa JF
 
Mnaoandika nyuzi humu mitandaoni kuhusu criticism juu ya awamu hii sijui kwanini mnapenda kuingia banda la udini au uanamke.

Kwani Samia ni malaika na hawezi kukosea, why mnaguilt wash na kumfanya aonekane ni malaika yupo perfect 100%?

Swali jingine, why mna assume kuwa criticism inatoka kwa maaskofu wa makanisa tu ili mpate uhalali wa kusema ni udini unatumika kumjadili matendo yake?

Hao maaskofu wapo wangapi ukilinganisha na idadi ya wanainchi wa kawaida, wanachama wa upinzani, wamasai wa ngorongoro ambao wengi wao wanamtupia madongo kila kukikucha?

Akiongea askofu mara moja inageuka kuwa ni udini, aliyewaambia askofu anaongoza ibada hapo ni nani?

Ni wajibu wa kila taasisi kukemea utomvu wa nidhamu kwa uongozi usiofuata sheria za inchi na kuzipindisha huku katiba ikikanyagwa mchana kweupe.

Nani kuwaambia haya ni majadiliano ya kidini,kuna sehemu wamesema kuwa samia amekosea mistari ya Bible? Si wanakemea uharibifu wa sheria ambazo sote zinatuongoza?

Hebu acheni hizi habari za kupotisha na kupindisha ukweli.

Anaetetea uhalifu kwasababu anayetuhumiwa ni mtu wako wa karibu,ndugu yako au ni anakulipa kutetea, au unafanana nae dini au imani yako basi na wewe unakuwa ni mshenzi wa kabisa na hauna faida yoyote kuzungumza.
 
Hiyo Novena mngefunga kipindi cha gaidi mwenzenu wa kikatoliki magufuli alivyokua anateka na kuua watu, huyo lissu mnaemtetea huko Gerezani alitaka kuuliwa na huyo Gaidi mwenzenu wa kikatoliki ila hamkufunga Novena leo mnaleta unafiki
 
Yeye ndiye aliyefadhili na kuandaa kikao Cha maimam kumpigia Kampeni zake alizoanza kabla ya Ratiba ya Tume aliyoiunda mwenyewe.Haambiliki.
 
You can say that again 🙄 !
Lakini je muda wake kama umeisha then what’s next ??!
Watu wakusanyike tena Idodomya na wale wanaoitwa majina mengi ya kila aina including the King makers si watakuwepo ndani ya Nyumba ??!
Then what’s next 😳! 😳 ???!

Najaribu tu kufikiri nje ya box 😅🤷🏿‍♂️ !!
 
Rtd aombe msamaha kwa kosa Gani kama yeye alifuata matakwa ya katiba yetu!? Na Je huyo ambae angempendekeza kinyume na katiba angeharibu, Rtd tungemwambiaje?

Let us be honesty to our hearts and mind! He did what was supposed to be done! Unless otherwise he could violate the Constitution.
 

Your browser is not able to display this video.
 


Samia atapita kama mwenzake Magufuli . Magufuli naye alikuwa anawasema mapadre kuhusu Corona ! Yakawaje? Mama naye kiburi chake itakuwa hivyo
 
Kanisa kusali Novena katoliki sio suala la siasa kusali Novena ni jambo la kawaida sana kipindi cha Magu wamesali pia
 
💯 truth
 
Yani huyu mama jamani hana busara kabisaaa. Tutalaumu bure washauri ila yeye mwenyewe ni tatizo kubwa sana. Hivi unawezaje kuwa na maamuzi ya kubomoa kila kukicha! Anapenda sana ligi za nipe nikupe. Badala ya kutuliza mambo, yeye ni kurudisha mashambulizi kwa kila anayemchallenge na hajali ni mashambulizi ya kujenga au kubomoa. Kila siku anazidisha chuki mioyoni mwa watu. Hii move ya kwenda kwa masheikh was so unnecessary, zaidi inazidi kuharibu. Akigombana na Gwajima, anaibukia kwa Mwamposa! Badala ya kusolve ya Gwajima! Kwa Hapa kwa kweli tumeingia cha kike. Hii challenge yetu ya safari hii ya uRais ni kiboko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…