Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Sababu zinaweza kuwa nyingi za variation kwenye bei ya mafuta kati ya nchi mbili.Ndo maana tunasema kwa ujumla mfumo wa kodi sio rafiki kwa walipa kodi na ndo sababu ya biashara nyingi kufa.
Ukiwa burundi kununua gari ni bei nafuu sana! Ukiwa zambia mafuta ni bei nafuu sana! Na vyote vinapitia bandari ya dar!
Hapa kwetu shida ni nn!?
Kwanza uwezo wa biashara kununua moja kwa kwa from refineries, ku-distribute wao wenyewe nchi nzima ili kuwa na standards price.
Tanzania asilimia kubwa ya retailers wa mafuta ni independent ambao hawana advantages za economic scales wala own storage depots hayo mambo yana umuhimu kwenye strategic planning za ushindani kwenye soko huria.
Matokeo yake badala ya bei kupangwa na soko sababu ya ushindani zinapangwa na EWURA (which is ok given the market structure), halafu kuna tozo za mazingira na halmashauri nazo zinachangia kwenye bei.
Kwa maana hiyo tatizo sio TRA pekee inabidi uchunguze tozo zote ambazo Burundi wanaweza wasiwe nazo. Similarly kwenye Tanzania kuna dumping taxes, Burundi wanaweza wasiwe nazo.
Lakini kodi za kibiashara per se yaani za faida kwenye uzalishaji ni standard nchi nyingi vat ni 15-20%, Tanzania ni 18%. Corporate tax ni 30% of profit na kuna allowable expenditures nyingi tu za kupunguza kodi inayolipwa na mfanyabiashara hasa wazalishaji wa ndani vitu kama depreciation, capital allowances, etc.
Ndio maana malalamiko ya kodi yapo sana kwa walipa kodi wadogo tu. Sikatai kuna wafanyakazi wa TRA sio waadilifu, ila tatizo kubwa zaidi ni uelewa wa majukumu yao ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo.
Ukisikiliza wengi awaelewi matakwa ya kisheria kama kutunza hesabu zao kwa miaka kadhaa maana wanaweza kaguliwa miaka ya nyuma, kutii sheria deadlines ambazo zina fines za kikodi usipofuata regulations, kushindwa kutengeneza hesabu zao za mwaka (in short malalamiko yao mengi ni maswala ya kawaida nchi nyingine, sisi kwetu watu wanaona wanaonewa).