Kitendo cha mabeberu kufungasha na ongezeko la utitiri wa kodi

Twambie basi huo mlundikano? Mfano double taxation etc. Huwezi kulalamika mlundikano bila kutolea ufafanuzi kuonyesha kwamba kuna kodi hii ambayo haitakiwi au ipo kimakosa etc kutokana na issue hii au ile? Wacha kamba? Usilalamike tu bila kutoa solution ambayo itasaidia kuboresha hizo kodi.
Kwa akili yako unataka kutuambia kuwa hata kama Kodi zikiwa zinaumiza wananchi ili mradi zipo kisheria basi maumivu ya mlipa Kodi hayapo?
 
Hujawahi kuagiza gari ndio Mana unaanzisha thread za kulia Lia
Ukiagiza gari japani,kwenye bei Kuna gharama za ukaguzi,ambazo baadae zinapelekwa Tbs
Tbs wameamua kukusanya wenyewe,ulichokua unalipa japan utalipia Tanzania shida ipo wapi?
Una uhakika na hicho unachosema,
Au umeamua tu kutetea unyonyaji?
Serikali inatakiwa ije na majibu sahihi na siyo ninyi mnaotumika kutetea kila Jambo hata Kama linaumiza watanzani.

Kama ilichosema ni sahihi tusione stika ya ukaguzi toka japan
 
Si kila mtu anafaa kupewa leseni ya udereva.
Awamu umekazia tozo tu Kodi tu bila kuchochea uzalishaji,watu wazalishe Ili walipe kodi.Matokeo yake hata hizo kodi watazikosa sababu haziwiani na vipato vya walipa kodi.Kodi ni kubwa kuliko uzalishaji.
 
Mk
Uko sahihi sana. Na ilipaswa wazalishaji wengine nao wafanye hivyo kuinua zaidi na kwa pamoja pato la nchi yetu. Je, ni eneo lipi mfugaji ambaye ni mzalishaji sawa au zaidi yako kisheria anawajibika kulipa kodi kulingana na idadi ya mifugo yake? Niambie Mkuu, hapo mapori ya Ruvu kuna wamasai na mifugo lukuki,isingekuwa busara tukaona njia nzuri nao wakachangia kisheria kama sisi tunavyofanya? Dhambi ni ipi kama watafanya hivyo?
Labda kwa kukusaidia jiuluze hao wafugaji wanao miliki mamia ya mifugo wanafanya biashara?
Je wakiuza ng'ombe au mbuzi wanalipia ushuru wa mnada?
Mkuu kumiliki shamba au mifugo bila kupata kipato hakuna haja ya kulipa kitu isipokua ukiuza mazao au wanyama hapo serikali inatakiwa ipate chochote
 
Weka ushahidi! Majungu peleka kwenye udaku.
Wewe kweli umeishiwa! Suala la kodi linahusiana na biashara, hali ya kibiashara unavyoona ww ni nzuri? Biashara zinashamiri au zinakufa?

Utakuwa unaishi maleysia ww!
 
....Bora Kodi ndogo inayolipwa na watu wengi kuliko kutegemea Kodi kubwa inayolipwa na watu wachache
Kwa formula gani ?????

Kwa mahesabu gani?

Nionyeshe formula ya kodi, au ya uchumi, au hesabu za darasa la tatu, calculus za form six, statistics za chuo kikuuu, certified accounting au kutoka taaluma yeyote ile inayosema kodi ndogo ndogo ya watu wengi inazalisha hela nyingi kuliko makodi mazito mazito ya watu wachache.

Onyesha!
 
Serikali lazima itoze kodi ili iweze kufikia malengo yake ya kuwatumikia Watanzania. Tozo za magari kila mwaka hata ulaya zipo, huwezi kuwa na gari barabarani ambalo halijaangaliwa kwamba lipo imara kuwa barabarani na ni salama, kila mwaka unless lina miaka mitatu tangu liwe jipya vinginevyo kila mwaka lazima likaguliwe na mwenye gari alipie ukaguzi huo kila mwaka. (Ulitaka nani alipie wakati wewe ndiye unatumia hilo gari?) Tmechoka na ajai ambazo hazina mkia.

Nchi haiwezi kutegemea misaada, kwani Watanzania wote ni vilema? Nchi inatakiwa ijiwezeshe yenyewe hatuna mjomba huko nje wa kutusaidia.

Sekta binafsi ilijisahau kwa kufikiria ni lazima Serikali iwape unafuu kufanya shughuli zao. Je, kama sekta binafsi inataka kodi nafuu inafikiria Serikali itapata wapi fedha za kujiendesha? Je, ni nani alipe hiyo gharama? Tanzania ina watu millioni 60 na ushee hatuwezi kuwa wakinga bakuli!

Ni lazima kila sekta ilipe kodi, wafanyakazi wanakatwa kila mwezi kwa nini wafanya biashara wanafikiri wao ni muhimu zaidi kuliko wengine? Kila mahali watu ni lazima walipe kodi stahiki bila kupepesa macho. Nchi haitaendelea kwa sababu kuna watu au kikundi ambacho kinafikiri lazima kihurumiwe kulipa kodi.
Haya tumchinje tu huyu bata anaetaga mayai ya dhahabu ili tupate mengi zaid!

Amandla...
 
Kwa formula gani ?????

Kwa mahesabu gani?

Nionyeshe formula ya kodi, au ya uchumi, au hesabu za darasa la tatu, calculus za form six, statistics za chuo kikuuu, certified accounting au kutoka taaluma yeyote ile inayosema kodi ndogo ndogo ya watu wengi inazalisha hela nyingi kuliko makodi mazito mazito ya watu wachache.

Onyesha!
Hata akikuonyesha hutaelewa. Certified accounting inahusiana nini na alicho ongea?

Amandla.
 
Taxes nyingi za kibiashara Tanzania zipo sambamba na global average; issue labda import duty.
Ndio nn sasa!!?

Import duty... ndo mbaya? Au import duty imeizidi nguvu serikali?
 
Hata akikuonyesha hutaelewa. Certified accounting inahusiana nini na alicho ongea?

Amandla.

Nchi niliyowahi kuishi, ambapo kila mwananchi anatakiwa kufanya kokotoo za kodi yeye mwenyewe na kupeleka mahesabu serikalini akiambatanisha malipo au madai, wengi tulikuwa tunaenda kwa wahasibu, certified accountants, watusaidie.

Kwa hiyo najua mhasibu ni moja ya watu wanaoweza kunieleza hili, pamoja na, labda, mchumi, mtakwimu, mwana taaluma wa biashara, au mwanafunzi wa Calculus za kidato cha sita, au labda ni hisabati ndogo ya darasa la tano.

Sasa nionyesheni - unamshambuliaje mtu aliye widely open minded kujifunza - nionyesheni maelezo ya kitaalam:

ni wapi palipohitimishwa kwamba watu wengi wakitozwa vikodi vidogo vidogo zitapatikana hela nyingi kuliko wachache wakitoa makodi makubwa makubwa ?????
 
Mwaka 2021 umeanza kwa kutangazwa kodi au tozo ambazo awali hazikuwepo. Tumesikia ukaguzi wa magari, garama za kuagiza magari zimepanda mara mia, tozo katika bidhaa nyingi za nje nk.
Gharama ni ile ile
Tofauti no kuwa badala gari kukaguliwa Japan,litakaguliwa Tanzania
Maana yake ni kwamba pesa itabaki Tanzania,na kutanua ajira kwa mafundi wa kitanzania
 
Nchi niliyowahi kuishi, ambapo kila mwananchi anatakiwa kufanya kokotoo za kodi yeye mwenyewe na kupeleka mahesabu serikalini akiambatanisha malipo au madai, wengi tulikuwa tunaenda kwa wahasibu, certified accountants, watusaidie.

Kwa hiyo najua mhasibu ni moja ya watu wanaoweza kunieleza hili, pamoja na, labda, mchumi, mtakwimu, mwana taaluma wa biashara, au mwanafunzi wa Calculus za kidato cha sita, au labda ni hisabati ndogo ya darasa la tano.

Sasa nionyesheni - unamshambuliaje mtu aliye widely open minded kujifunza - nionyesheni maelezo ya kitaalam:

ni wapi palipohitimishwa kwamba watu wengi wakitozwa vikodi vidogo vidogo zitapatikana hela nyingi kuliko wachache wakitoa makodi makubwa makubwa ?????
Huyo CPA ni mtaalam wa kodi za watu binafsi na si uchumi wa nchi. Impact la kodi kwenye uchumi ni eneo la wachumi na sio wahasibu. Hao wanafunzi ndio kabisa hawahusiki.

Argument ni kuwa kodi ziwe realistic na sio za kuumizana. Nchi ambazo zinakusanya kodi sana zinawatoza wenye vipata vikubwa vya ziada kiasi kikubwa na wenye kipato cha ziada kidogo kodi kidogo. Kiasi cha kodi kinapangwa kulingana na uwezo wa watu kulipa na sio mahitaji ya nchi.

Amandla...
 
Ndio nn sasa!!?

Import duty... ndo mbaya? Au import duty imeizidi nguvu serikali?
Kuna vi tax vingi vat, rail duty, port duty na saa zingine storage charges; they all add up. Kama kiwanda kinahitaji mitambo ya millioni kumi + those taxes add up a lot.
 
Huyo CPA ni mtaalam wa kodi za watu binafsi na si uchumi wa nchi. Impact la kodi kwenye uchumi ni eneo la wachumi na sio wahasibu. Hao wanafunzi ndio kabisa hawahusiki.

Argument ni kuwa kodi ziwe realistic na sio za kuumizana. Nchi ambazo zinakusanya kodi sana zinawatoza wenye vipata vikubwa vya ziada kiasi kikubwa na wenye kipato cha ziada kidogo kodi kidogo. Kiasi cha kodi kinapangwa kulingana na uwezo wa watu kulipa na sio mahitaji ya nchi.

Amandla...
Uchumi, finance (banking and insurance), business management and accounting; hizo degrees zake zina relation.

Nchi kama UK mtu aliesoma diploma ya accounting vyuo vingi vinaweza mpokea mwaka wa tatu (sio vyote) kufanya hizo degree zingine kwa mwaka mmoja; lakini hao wengine awawezi jiunga accounting mwaka wa tatu, it’s considered superior of the business majors.
 
Kuna vi tax vingi vat, rail duty, port duty na saa zingine storage charges; they all add up. Kama kiwanda kinahitaji mitambo ya millioni kumi + those taxes add up a lot.
Ndo maana tunasema kwa ujumla mfumo wa kodi sio rafiki kwa walipa kodi na ndo sababu ya biashara nyingi kufa.

Ukiwa burundi kununua gari ni bei nafuu sana! Ukiwa zambia mafuta ni bei nafuu sana! Na vyote vinapitia bandari ya dar!

Hapa kwetu shida ni nn!?
 
Serikali lazima itoze kodi ili iweze kufikia malengo yake ya kuwatumikia Watanzania. Tozo za magari kila mwaka hata ulaya zipo, huwezi kuwa na gari barabarani ambalo halijaangaliwa kwamba lipo imara kuwa barabarani na ni salama, kila mwaka unless lina miaka mitatu tangu liwe jipya vinginevyo kila mwaka lazima likaguliwe na mwenye gari alipie ukaguzi huo kila mwaka. (Ulitaka nani alipie wakati wewe ndiye unatumia hilo gari?) Tmechoka na ajai ambazo hazina mkia.

Nchi haiwezi kutegemea misaada, kwani Watanzania wote ni vilema? Nchi inatakiwa ijiwezeshe yenyewe hatuna mjomba huko nje wa kutusaidia.

Sekta binafsi ilijisahau kwa kufikiria ni lazima Serikali iwape unafuu kufanya shughuli zao. Je, kama sekta binafsi inataka kodi nafuu inafikiria Serikali itapata wapi fedha za kujiendesha? Je, ni nani alipe hiyo gharama? Tanzania ina watu millioni 60 na ushee hatuwezi kuwa wakinga bakuli!

Ni lazima kila sekta ilipe kodi, wafanyakazi wanakatwa kila mwezi kwa nini wafanya biashara wanafikiri wao ni muhimu zaidi kuliko wengine? Kila mahali watu ni lazima walipe kodi stahiki bila kupepesa macho. Nchi haitaendelea kwa sababu kuna watu au kikundi ambacho kinafikiri lazima kihurumiwe kulipa kodi.
Swala la muda, kwa curves cross against each other, tutakuja kuwasikia hapa mkileta hizi hoja.
 
Back
Top Bottom