Pre GE2025 Kitendo cha Mahakama kwenda kutoa hukumu ya TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuzidi kubariki uovu wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mie sio mtu wa ligi mbona mrangi, mie huwa mkweli tu..

naona mnapeana moyo na matumaini na ndugu yako Ben 🤣
Sawa bana mzee wa ligi 😄
Ila ukweli najuwa unaujuwa
One day yes ... 😄

Ova
 
Wewe unatoa amri ya kutokalamika kama nani au ubwege ulionao kichwani ndio tatizo kifupi endelea kudeki vyoo vya lumumba huku ukivizia teuz huku ambazo hutozipata.
 
Jifunze kuandika kwa usahihi lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Hueleweki.
 
Na huu uchaguzi wa mitaaa jamaa atatunyoa kwerikweri 😄

Ova
 
Uko sahihi mkuu
Lakini hii kesi itathibitisha madai kuwa mahakama zetu haziko huru

Pili itadhibitisha madai kuwa ccm inaogopa uchaguzi kiasi kwamba inatafuta unafuu kupitia tamisemi

Nadhashauru baada ya ccm kupewa ushindi batili mahakamani, wapinzani wasusie uchaguzi

Hii itakuwa ni sababu ya maandamano yasiyokoma ya kushinikiza uchaguzi uhairishwe ili maandalizi yafanyike kwanza chini ya tume ili uchaguzi ufanyike mwakani pamoja na uchaguzi mkuu
 
At the end of day kutegemea tume ya uchaguzi, katiba mpya au maamuzi ya mahakama ni kujichelewesha tu.

Watanganyika tukiamua kwa vitendo CCM watatupisha watake wasitake.
 
Umesikia hoja za mapingamizi ya serikali kuhusu kesi hii :
  1. Kesi ni ya kikatiba haiwezi kuamuliwa na Mahakama, maana yake ni bunge la chama kimoja libadilishe katiba
  2. Waliotuma maombi *(Waliofungua kesi ) Bob Wangwe na wenzie 3 watawanyima nafasi mamilioni ya watanzania wasipige kura November 2024
Msikilize wakili kutoka Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali hoja zake kwanini serikali inataka TAMISEMI iendelee kuwa msimamizi wa uchaguzi 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=X-Qk-eBMyxs
 
UMAKINI WA KURIPOTI KESI ZA MAHAKAMANI :
Tatizo hata vyombo vya habari media House kubwa Tanzania , hawana waandishi wa kutoa ripoti za mahakamani ili wananchi waelewe muenendo wa kesi mbalimbali, ikiwemo hii kesi muhimu iliyofunguliwa na wananchi watatu Bob Wangwe na wenzie 2 wakitetewa na jopo linaloongozwa na wakili msomi Jebra Kambole.

Mwisho wa siku watu watashangaa hukumu ikitolewa lakini hawana ufahamu wa mwendendo wa kesi hii siku kwa suku inapisikilizwa


Na hapa JamiiForums uzi huu utaunganishwa fasta, ili kuwapoteza watu wasieleewe nini kinaendelea.
 
Umuhimu wa uwazi (open justice) katika kesi hii na kesi zote kwa umma. Kesi hii siyo ya uhaini au inaingilia faragha ya watu ( kubakwa / rape n.k) hivyo waandishi wanatakiwa kuiripoti kila kinachojiri mahakamani kwa uwazi watu / umma wafahamu hoja za mawakili upande wa waleta maombi na upande wa wajibu ambao ni serikali inangangania kwa sababu gani TAMISEMI iratibu uchaguzi wa November 2024

Mawazo ya watu wengi Tanzania kuhusu kile kinachoendelea katika chumba cha mahakama hutoka kwenye filamu, televisheni, vitabu, au labda kuhudumu kwenye jury wenyewe. Taswira ya chumba cha mahakama iliyoonyeshwa katika filamu, televisheni na vitabu inaweza kuwakilisha au isiwakilishi kwa usahihi mwenendo wa mahakama. Bado, ukiwa mwandishi wa habari au mwana JamiiForums ukielekea kortini, utapata kuelewa vizuri zaidi kile kinachotokea katika chumba cha mahakama na jinsi ya kuripoti kwa usahihi mwenendo wa kesi kama hii dhidi ya TAMISEMI


The open justice principle

The general rule is that the administration of justice must be done in public, the public and the media have the right to attend all court hearings and the media is able to report those proceedings fully and contemporaneously

TOKA MAKTABA:
Fatma Karume nodo zake kali na asema 'rules are made to be broken' na kwanini hutokea anatoa elimu mtambuka kuhusu masuala ya mwenendo mzima wa kesi mbalimbali katika mahakama zetu :

View: https://m.youtube.com/watch?v=K4kVdwF9vrQ
 
Mahakama inaweza kubaliana na waleta maombi, ila baadaye rufaa ikatupilia mbali au kuzuia kwa muda
 
Hakika mkuu ,mahakama ikionesha imeegemea upande mmoja uchaguzi usifanyike tu kutakuwa hakuna haja ya kufanya uchaguzi
 
Kama hoja ya kwanza imetolewa na mawakili wa serikali basi CHADEMA waliona mbali kuhusu hoja hiyo walishasema, hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi pasipokubadili katiba kwahiyo wanasheria wa CHADEMA wapo very seriously sana kuhusu ilo na ndymana walipinga toka mwanzo.
 
Hi i
Hivi sasa hukumu ina andaliwa na Ccm
Jaji ata pelekewa kusoma tuu.
Judiciary imesha compromise na chama tawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…