cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
hiyo nchi wanaipigania nan anawatawala ?
Mdusi94: Swali ni nani anawatawala ni mfupa mgumu kwa Wapelestina kuujibu! Wemeuza narratives nyingi mno kuhusu hilo.
Halijawahi kuwepo taifa linaloitwa Wapelestina chini ya jua, hakujawahi kuwepo utawala wowote unaotambulikana kama Palestina! Hakuna hata viashiria vyovyote vya utaifa (Soveregnity) Iwe bendera, historia nk! Huu Utambulisho umebuniwa tu along the way, miaka ya mwishoni 60 na 70! Kama njia ya Waarabu kupambana na Israel !
Mpiganaji wa Kipalestina (PLO) Zuheir Mohsen, alipohojiwa na na Gazeti la Trow( Truth), gazeti la Ki Dutch, mnamo mwaka 1977, aliweka wazi, hakuna taifa la Wapelestina! Sisi ni Waarabu tu!
- The Palestinian people do not exist. There are no differences between Jordanians, Palestinians, Syrians and Lebanese. We are part of one people, the Arab nation. Lo and behold, I have relatives with Palestinian, Lebanese, Jordanian and Syrian citizenship. We are one people. It is only for political reasons that we carefully endorse our Palestinian identity. Indeed, it is of national interest for the Arabs to encourage the existence of the Palestinians in the face of Zionism. Yes, the existence of a separate Palestinian identity is only for tactical reasons. The establishment of a Palestinian state is a new means to continue the struggle against Israel and for Arab unity.
Warumi walitawala maeneo hayo muda mrefu kama miaka 635, kutegemea vyanzo mbali mbali vya historia, na Mahali hapo pametawala na mamlaka nyingi, na ujio wa Waislamu mahali hapo nao uko wazi miaka, katika kipindi cha Caliph Umar 635-660 alipouteka mji wa Jerusalem, uwepo wa Uislamu ndio unapata mlango wa kuingilia mahali hapo, ikumbukwe Wakristo na Wayahudi walikuwepo na kuwa chini ya himaya hiyo.
Lakini ujio wa Utawala wa Ottoman Empire ambao ulivamia na kuteka na kutawala mahali hapo unatoa mchangamano mzuri na more documented kuhusu wakazi wa mahali hapo, kwani utawala wa Ottoman Empire ulidumu kwa miaka 600, lakini ulitawala mahali hapo kwa miaka takrabani 402 ( 1516-1918) na kuishia baada ya kushindwa kwenye vita vya kwanza na waingereza 1918.
Kumbuka kuwa Waturiki sio Waarabu, walipokuwa wakitawala sensa inaonyesha wazi wakazi wa mahali hapo walikuwa kama ifuatavyo:
Demographic history of Palestine (region)
https://en.wikipedia.org/wiki/Demographic_history_of_Palestine_(region)Per McCarthy's estimate, in 1914 Palestine had a population of 657,000 Muslim Arabs, 81,000 Christian Arabs, and 59,000 Jews. McCarthy estimates the non-Jewish ...
Ukiangalia demographic data, zozote zile, ukweli unabakia kulikuwa na watu mchanganyiko, Waarabu (Waislamu) Waarabu Wakristo, na Wayahudi!
Hii inaua dhana kuwa Wayahudi HAWAJAWAHI KUWEPO (Kama baadhi ya Waarabu wanavyodai leo) mahali hapo! Ukweli unabakia kuwa hata kipindi cha Mandate ya Waingereza kuisha May 1948, mchanganyiko huu wa wakazi ulikuwepo, Waarabu wakiongoza kwa idadi, na Wayahudi wakiongezeka pia kutokea Ulaya na nchi nyingine za Kiarabu.
Labda kitu muhimu mno kukiweka hapa, ni vigumu kabisa kuiondoa Uingereza katika complexity za mahali hapo! Ili kuwaondoa na kuuishinda Ottoman Empire kwenye vita vya kwanza (Kumbuka Ottoman Empire ) ilkuwa upande wa Ujerumani. Mwingereza alitumia mbinu nyingi! Aliwaahidi Waarabu ( Sio waliokuwepo hapo Palestine tu) Waarabu wote waliokuwa chini ya Ottoman Empire atawapa utawala wao, wakisaidia kuwapiga Waturiki, Kumbuka Iraq, Jordan, Syria na wakazi hao mchanganyiko hapo Palestine wote walikuwa chini ya Waturuki.
Ahadi hiyo ya Waingereza aliitoa mahali hapo kwa Wayahudi pia! Mwamko wa Wayahudi kurudi kwao baada ya matukio matukio mengi huko ulaya uliwaamsha watu kama Theodor Herzl huko Ulaya, kutaka Wayahudi warudi kuungana na wenzao walioko Palestina kwenye kitovu cha asilia yao! Hapo neno ZIONISM linapojitokeza katika historia ya mahali hapo.
Kwa leo nitakomea hapo, kabala kuanza complexity history kulekea 1948......N ahadi tulipo leo, Nikipata nafasi next time, wengi wetu tumeshindwa kukaa chini, kusoma ili hata kuutetea msimamo unaoshikilia kwa kile kinachoendelea leo! Ni Historia inayochosha kidogo, na inataka muda!
Labda take away hapa, ni kuwa Waarabu ( Wapelestina) na Wayahudi wote wana historical attachment na hiyo land! Tatizo kila upande unataka iwe yao yote! Hao extremist wako pande zote! Upande wa Israel na upande wa Waarabu! Wako moderate pia.....Tutawachambua hao baadaye......Na pia kuna factors za Imani! Uislamu, Ukristo na Uyahudi......na una changia mno kuufanya mgogoro huu kukosa tiba ya kudumu....TUTAENDELEA NIKIPATA MUDA!