Kitendo cha Museveni na Kagame kutokuja kumuaga hayati Rais Magufuli kinaashiria nini?

Kitendo cha Museveni na Kagame kutokuja kumuaga hayati Rais Magufuli kinaashiria nini?

Unakuja sehemu kuna kiwanda cha COVID-19...why risk?
 
Ndani ya muungano wa EAC nchi ya Kenya imekuwa mstari wa mbele katika kuleta chokochoko za hapa na pale, hasa ikiichokonoa Tanzania mara kwa mara. Ingawa hivyo, Rais wa Kenya Hon Uhuru Kenyatta amefika yeye mwenyewe mubashara kuja kumuaga hayati Dr Magufuli.

Nchi za Uganda na Rwanda hazijawahi kujiingiza kwenye utata wowote ndani ya EAC mbali na lile tukio ambalo Kenya iliishawishi Uganda kusaini makubaliano ya ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Kampala pasipo kuishirikisha Tanzania.

Utawala wa hayati Rais Magufuli ulikuwa unafanana sana na ule wa Kagame, hadi watu kufikia hatua ya kudhani kuwa huenda staili yake ya utawala alikuwa ameinakili kutoka kwa Kagame. Pia Museveni amekuwa mara kwa mara akiitembelea Tanzania na amesikika mara nyingi akiufagilia utawala wa hayati Magufuli.

Sasa swali ni ni: Je, kwanini Kagame na Museveni wametuma wawakilishi kuja kuomboleza kifo cha Magufuli lakini Kenyatta amekuja yeye mwenyewe mubashara? Hawa majirani wawili wanaogopa nini kuja Tanzania? Is there any hidden agenda behind their absecnce in this crucial occasion?

Marais wametoka all the way from Southern Africa up to Tanzania lakini hawa jamaa wapo hapa karibu wame-mute tu! Kama nauli ya ndege ni tatizo wangeweza kusafiri hata kwa basi na kufika Dodoma mapema kabisa kumuaga kiongozi mwenzao aliyelala mauti. Hata wangeweza kukodi basi moja wakasafiri wote kwa pamoja ili kuokoa gharama. Lakini wameamua, kwa makusudi kabisa, kutuma wawakilishi. Je, hii ni sawa?
Naamini watakuwa Chato katika kumalizia shughuli!!
 
Ratiba yao haipo Chattle mkuu. Viongozi wote wa nchi wamealikwa Dodoma. Kwanini wao waende Chattle kupitia mlango wa nyuma? Mimi nadhani uoga wao unawaambia waje baada ya maziko. Wanateseka bure.....kamwe huwezi kukikimbia kifo.....kitakujia huko huko uliko na sio lazima mtu afe kwa korona; anaweza kufa hata kwa kansa, malaria, maradhi ya moyo, etc (JPM, 2021).
Kama ni hivyo, basi ile amri ya usiue Mungu asingetuwekea. Au kusingekuwa na haja ya kuwa huku u waliouwa kwa kuwa wametimiza Mpango wa Mungu..!!
 
Hawa ni majirani wa Marehemu, kutoka nyumbani kwao (Kigali - Kagame, Ankole - Museveni), mpaka Chato ni kama 200 km. Ni Kama Dar-es-salaam na Morogoro. Hivyo wameona ni heri kuhudhuria mazishi Chato na kukaa siku tatu au nne kama majirani wanavyo fanya ukanda ule, wakiwaliwaza wafiwa.
Vuta subira mpaka msiba uishe.
 
Kitendo cha hao kutokuja kinaashiria kwamba wanaheshimu taratibu za kupambana na maambukizi ya Covid-19 kwa kuepuka misongamano.
 
Wakenya ndio washirika wetu wa kweli japo tunagombana sana ila wagombanao ndio wapatanao,kwa kuthibitisha hilo nimefuatilia karibu Tv zao zote zimafanya coverage live tukio la kuaga mwili wa jpm toka msiba unaanza lakini uganda na rwanda hamna cha ajabu hadi malawi walikuwa live lakini hao niliotaja walikuwa wanaendelea na mambo yao kama kawaida,asanteni wakenya.
 
Viongozi wote wa Afrika wamekuja Dodoma wao waende Chattle kusababisha usumbufu wa kiusalama kwani wao ni sehemu ya familia?

Sidhani kama hata huko Chattle wataenda ikiwa wameshindwa kuja Dodoma. Hawa jamaa ni wanafiki wakubwa, leo ndio nimewagundua.

Mungu hamfichi mnafiki. Wameumbuka mchana kweupe. Walikuwa wanasifia utawala wake kumbe walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Wanafiq wakubwa!🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
Kumbuka museven
Viongozi wote wa Afrika wamekuja Dodoma wao waende Chattle kusababisha usumbufu wa kiusalama kwani wao ni sehemu ya familia?

Sidhani kama hata huko Chattle wataenda ikiwa wameshindwa kuja Dodoma. Hawa jamaa ni wanafiki wakubwa, leo ndio nimewagundua.

Mungu hamfichi mnafiki. Wameumbuka mchana kweupe. Walikuwa wanasifia utawala wake kumbe walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Wanafiq wakubwa!🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
Kumbuka museven hata msiba wa Mwl Nyerere maziko ya kitaifa dar hakufika lakini siku ya mazishi rasmi Butiama jamaa alishuka Kwa elkopita na bade tena akaenda Butiama Kwa gari kutoka Uganda Hadi Butiama hivo usiwe na shaka na huyo musera Chato lazima aje.Kagame sina uhakika.
 
Mi nadhanu hiii mada mngeijadili siku ya maziko au baada ya maziko
 
Wanaogopa cvd.kama umemsikiliza uhuru amesema aliona liwalo na liwe lakini lazima aje
Wanaogopa cvd.kama umemsikiliza uhuru amesema aliona liwalo na liwe lakini lazima aje
Kagame si alichanjwa hadharani kumbe chanjo hasizaidii?
JPM katuachia imani na kutupa nje hofu,hakuna cha barakoa wala chanjo tunakanyagana kuliaga Jogoo la dunia.
 
Back
Top Bottom