Kitendo cha mzazi kukulazimisha uwahi kuoa husababishwa na nini wana jukwaa tusaidiane hapa?!

Kitendo cha mzazi kukulazimisha uwahi kuoa husababishwa na nini wana jukwaa tusaidiane hapa?!

1. Uache uzinzi
Ingawaje ndoa haizuii MTU kuwa mzinzi.

2. Waone Wajukuu wao.
Hii ndio wengi huipenda zaidi.

3. Wanahofia labda unamatatizo, hawajiamini. Wanahisi sio mwanaume rijali.

4. Wanaona unaakili mgando, hivyo ukioa; majukumu ya Ndoa yatakubadilisha uta-focus na Maisha na utatulia.
Hii Kwa wanaume wengi hufanya kazi. Wakioa na wakiwa Baba hubadilika na kuacha baadhi ya tabia za kitoto.

5. Wengine hutokana na Ukoo wenu kuwa Mdogo. Hivyo uoe na kuzaa uongeze ukoo.

6. Wengine wamechoka kuchangia harusi za wengine. Wanataka warejeshe Pesa zao kupitia harusi yako, kwani Rafiki zake watakuchangia.

Wewe ndio unajua jibu sahihi Kati ya hayo niliyoandika
 
Msikilize mzazi wako. Kuna mengi sana anayowaza ambayo alishapitia hivyo anakushauri ili upite njia sahihi. Mfano ni mwendelezo wa kizazi.

Kwenye maisha kuna steji ambapo kuna wazazi wetu ambao wametuzaa sisi na tunapokuwa watu wazima wanatamani kuona kizazi kijacho yaani watoto wa watoto wao ambao ni wajukuu. Pia kwenye hili kuna suala la timing ili uweze kuwa na familia iliyo bora. Kuzaa mapema kunakuwezesha kutunza na kukuza watoto ukiwa na nguvu za mwili na kipato kuliko kuja kulea uzeeni ambako utakuwa umeshachoka kimwili na kiakili hivyo uzalishaji mali kuwa mdogo

Nina mengi ya kusema ili nimechoka kuchapa
 
1. Uache uzinzi
Ingawaje ndoa haizuii MTU kuwa mzinzi.

2. Waone Wajukuu wao.
Hii ndio wengi huipenda zaidi.

3. Wanahofia labda unamatatizo, hawajiamini. Wanahisi sio mwanaume rijali.

4. Wanaona unaakili mgando, hivyo ukioa; majukumu ya Ndoa yatakubadilisha uta-focus na Maisha na utatulia.
Hii Kwa wanaume wengi hufanya kazi. Wakioa na wakiwa Baba hubadilika na kuacha baadhi ya tabia za kitoto.

5. Wengine hutokana na Ukoo wenu kuwa Mdogo. Hivyo uoe na kuzaa uongeze ukoo.

6. Wengine wamechoka kuchangia harusi za wengine. Wanataka warejeshe Pesa zao kupitia harusi yako, kwani Rafiki zake watakuchangia.

Wewe ndio unajua jibu sahihi Kati ya hayo niliyoandika
Duh ilo nalo neno chief 😂
 
Ndio msingi wa dunia, ilikuwa hivyo, na iko hivyo na itaendelea kuwa hivyo, lazima kizazi kiendelee, ujio wako dunia usiishie kutumalizia hewa, chakula na raslimali kisha ufe bila kutuachia kizazi.
🙄 Htr hii
 
Wazazi wana sababu nyingi kutaka mtoto wao wa kiume aowe.

Ya kwanza kabisa ni kuhakikisha wamezaa na kulea kidume siyo shoga.
Hiyo ni ya kwanza ni sababu ya kwanza kwako tu.
Hujui kua mashoga nao wanaoa pamoja na huko kubanduliwa kwao.

Hitaji lao kubwa hawa kina mama ni mjukuu, basi hawaendi direct kwenye point. Na ya pili huwa ni ile heshima mtaani kua mwanae kaoa.

Yaani mama kabisa uwe na hofu kua mwanao ni punga basi kwenye malezi yako bibie kuna mahali unapwaya.
 
Hali sio nzuri ni Mwaka sasa tangu nimevunja mahusiano kutokana na sababu za kutokua na amani katka mahusiano.

Leo tangu Mwaka ulivyoanza hata kabla mzazi wangu wa kike amekua akiforce niweze kuchukua mwanamke nakuweka ndani nikajua au kwakua yupo kizamani zaidi pamoja nakumwelewesha yote hayo lakini amekua akiharakisha suala la kuoa.

Tena nami nishajua Raha ya kuwa single ndio kabisa sasa naomba msaada wenu ktk hili Mimi kama mtoto nifanye maamzi au ndio niendelee kutulia zaidi ndani ya usimbe maana naogopa hata kupiga sim kuhofia hayo maneno na akianza kuongea Bi Mkubwa lazima usepe mbali kumpisha🗣️
TABIA YAKO YA KUPENDA NGONO HIVYO WANAOGOA KUKUPOTEZA BILA KUACHA MTOTO
 
m nafkir kuoa sio tatizo,tatizo unaoa nani?

Vijana ndoa sio sehem ya kufanyia trials (Majarbio) japo sio busara kuchelewa kuoa lkn kwa upande mwngne maisha ya usingle yana amani yake!
 
Back
Top Bottom