Kama ushahidi upo kwamba alipokea hela lazima naye atapata kipande chake, lakini kama ni tetesi tu zitabakia kuwa tetesi tu mpaka zitakapothibitishwa, jamani twende mbele turudi nyuma; kabla ya mechi ya jmosi Azam alishawafunga Yanga mechi tatu hizo nazo walitoa hela? Lawama zipelekeni kwa viongozi na wachezaji kwa kulishana sumu na kufanya matendo yasio kuwa ya kianamichezo, mie nlikuwepo uwanjani kadi zote hizo Niyonzima alistahili, nakumbuka kuna mechi ya Simba na Yanga Mrwanda alipata red mazingira kama yale ya aliyopata red Niyonzima, kwa hiyo mimi nasema bado Niyonzima alistahili alichopata ndo maana kwa kutambua hivyo kawaomba radhi wanachama, washabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira kwa ujumla na kama ameonewa kwa nini aombe radhi?