Kitila Mkumbo: Mkataba wa Bandari unafanana kila kitu na mkataba wa ujenzi wa Mlimani City

Kitila Mkumbo: Mkataba wa Bandari unafanana kila kitu na mkataba wa ujenzi wa Mlimani City

Bahati nzuri sana nilihudhuria mhadhara mojawapo wa Late Professor Seth Chachage, kipindi kile Chachage alikua "very 🔥" na alituambia kuwa mojawapo ya vitu vilivyomo kwenye mkataba wa mlimani city ni Kwamba
1. Maduka yatakua yakiuza bidhaa mbali mbali ambazo zitawasaidia wanafunzi kwenda hapo kufanya shopping
2. Watajenga low cost houses ambazo zitasadia kusuala la malazi Kwa wanafunzi, kama mnakumbuka Adha ya accomodation UDSM ilikua issue kubwa sana,
3. Kuwa watajenga permanent structures hata baada ya mkataba wao kuisha

Sasa Kwa wenye wako na akili, wanaona yanayoendelea Leo hii, zile apartments za mlimani city ndio ambazo wanafunzi walijengewa eti wakae hapo, zile nguo za laki kadhaa ndio hizo wanafunzi wa UDSM wamewekewa wakavae.

Siku chache wakati joto likiwa juu sana Kuhusu mlimani city investment, Professor Seth Chachage akiwa Kibaha alidondoka baadae akatangazwa kuwa roho yake iliacha mwili
Mkuu wewe huendi mlimani City ukanywa juice 🥤 uepeleki watoto wakacheze?
 
Nchi hii inaendeshwa na watu wavivu wa kufikiri, wenye umwinyi mwingi na kutafuta zaidi njia za mkato.

Hivi bandari kama lango kuu na mpaka wa nchi,mkataba wake unaweza kufananishwa na ule wa Mlimani city?

Bandari ni mali ya wananchi wote na sio mali ya Rais au Serikali, ardhi ilipo Mlimani City ni mali ya UDSM ... Tofauti hiyo Kitila haioni?

Aliyesema akili matope wala hakukosea!!.
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamithilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.

Huyu Waziri afahamu kuwa anapozungumzia mambo ya uwekezaji anatakiwa aelezee mambo ya kiuchumi zaidi kama anaweza na sio porojo!! Uwekezaji wa Mlimani city ulighubikwa na rushwa nyingi ambazo ziliwahusisha viongozi wakuu wa UDSM wa wakati huo na mpaka mmoja wao akakimbilia marekani!! Not withstanding kuwa hawakuchukuliwa hatua!

Waziri anaweza kutoa data zitakazoonesha kwamba chuo kikuu kimefaidika na uwekezaji huo mpaka hivi sasa? Kuona hayo majengo na maduka sio ishara ya kunufaika. Anaweza kutuonesha hao wawekezaji wamepata kiasi gani ukifananisha na mapato iliyopata UDSM? Bila kuwa na data hizo hana uhalali wa kusifia uwekezaji wa Mlimani city ; bali ni promo tu za kutetea uwekezaji wa DpWorld!

Kitila Mkumbo ulipewa $$$ na waarabu , itabidi uzitapike kwani wenyewe sasa wamestuka hawataki kuendelea under this hostile climate; mtahangaika sana na mama yenu kuzitapika hizo fedha mlizohongwa.
 
Huyu naye ni wale wale tu. Ni aina ya wale wanaoitwa "wasomi" maslahi. Siku zote hutanguliza maslahi ya matumbo yao mbele, halafu yale ya Taifa huwekwa mwishoni kabisa
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamithilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.

Sasa wewe una akili kuliko Profesa Kitila?

Yeye amekupa kama mfano tuh,chadema Lini akili zenu zitakaa sawa?
 
Mlimani City licha ya kuwa iliingia Mkataba wa hovyo lakini una time frame ya miaka 99, vipi DP World na Bandari zetu wanauziwa kwa kipindi cha miaka mingapi???

Hii Nchi bora iongozwe na Jeshi tu(CDF) kuliko hawa Wanasiasa wa hovyo tulionao 🙌
 
Ukienda pale Dar es Salaam kuna sehemu inaitwa Mlimani City, na wengine wakienda Dar es Salaam na kama hawajafika Mlimani City wanahisi hawajafika Dar es Salaam.

Wakati tunaijenga Mlimani City tuliambiwa tunakiuza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumbe tulichukua eneo dogo na kumpa mwekezaji akajenga Mlimani City na leo wana Dar es Salaam na Watanzania wanajivunia Mlimani City.

Hizi habari za kuambiwa umeuza au haujauza haijaanza leo.

Kama watoa elimu ndo hawa wa kufananisha potential ya bandari yetu na mlimani city mpaka mkataba ufanane tena kila kitu, basi hii nchi maprofesa wengi ni vilaza. Kitila ni miongoni mwa maprofesa hewa duniani
 
Ukienda pale Dar es Salaam kuna sehemu inaitwa Mlimani City, na wengine wakienda Dar es Salaam na kama hawajafika Mlimani City wanahisi hawajafika Dar es Salaam.

Wakati tunaijenga Mlimani City tuliambiwa tunakiuza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumbe tulichukua eneo dogo na kumpa mwekezaji akajenga Mlimani City na leo wana Dar es Salaam na Watanzania wanajivunia Mlimani City.

Hizi habari za kuambiwa umeuza au haujauza haijaanza leo.

Hiyo mlimani City inaungizia serikali kiasi gani
 
Mie nafikiri hawa watu wanafikiri wa Tz ni wajinga sana au hawana akili!
Kwanini hawatembei na mkataba huo kisha wasome kifungu kwa kifungu waone namna wananchi wangewashushua!
Wafanye kama hawa wazalendo wanaoupinga wanavyofanya ktk kuwafafanulia wananchi ili waaibike mchana kweupe!

Badale yake ni blahblah tena kwa watu wa ccm ambao wanajua fika kuwa ni weupe vichwani!
 
Ukienda pale Dar es Salaam kuna sehemu inaitwa Mlimani City, na wengine wakienda Dar es Salaam na kama hawajafika Mlimani City wanahisi hawajafika Dar es Salaam.

Wakati tunaijenga Mlimani City tuliambiwa tunakiuza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumbe tulichukua eneo dogo na kumpa mwekezaji akajenga Mlimani City na leo wana Dar es Salaam na Watanzania wanajivunia Mlimani City.

Hizi habari za kuambiwa umeuza au haujauza haijaanza leo.

Hahaha nani ajivunie mabanda yale. Tunasubiri soko la Africa mashariki pale ubungo
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamithilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.
Huyu ni mnafaki na mpumbavu mkubwa sana.Katika watu wabovu na wenye kufoji foji kila kitu ,ni huyu Kitila.Huyu jamaa na Mafuru Lawrance ,hawajawahi kupata hata div two tu kwenye maisha yao ya kusoma.Hawa ndio ndugai alikuwa anawasema.Lakin eti ndio wanatuo goza.
 
Wa Mlimani city ni miaka 50, huu wa DP world ni wa miaka mingapi?
 
Haya aliyoongea ni matope!!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom