Hayo maneno ya kusema sijui vyama vya upinzani havijajipanga kiuongozi au kisera au ni vichanga, Yalitumika kudanganya wananchi mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi, Lakini baada ya mda kidogo tu mabadiliko ya vyama tawala kwenye nchi jirani za Kenya, Congo, Zambia, Malawi na kwingineko, ilibainika wazi na dhahiri kuwa ulikuwa uwongo tu wa kuitaftia ushindi ccm!
Sasa kuendelea kutumia uwongo mwepesi kama huu hadi leo, kunadhihirisha kwamba ccm ilishafilisika sera zote! Wapishe wakae kando ili chama chenye maono mbadala kituvushe tulipokwama!