Kitimoto kupatikana Zanzibar ni ishara ya uvumulivu

Kitimoto kupatikana Zanzibar ni ishara ya uvumulivu

Japo Zanziba ni sehemu ya Tanzania, inafahamika kuwa asilimia kubwa ya wakazi wake ni Waislamu. Na inafahamika kuwa nguruwe, au MBUZI KATOLIKI kama inavyoitwa na baadhi ya watu, ni wanyama haramu kwa Waislamu.

Lakini unajua hiyo mboga inapatikana hata Zanzibar? Kwa ambaye hajawahi kufika huko, anaweza asiamini. Hata mimi nilikuwa na mtazamo huo. Ulibadilika baada ya kushuhudia kwa macho yangu na kinywa changu.

Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika Zanzibar. Nilipoulizia gesti iliyopo sehemu tulivu, baada ya kutoridhishwa na zilizopo maeneo ya Darajani, niliambiwa niemde kwa BI JANETH, mahali wanakouza kitimoto. Ipo Mbwe, Unguja.

Nilitilia mashaka hayo maelezo, lakini nikaamua kujiridhisha. Hata baada ya kufika kwa BI JANETH, na kuulizia vyakula vinavyopatikana hapo, bado sikuamini nilipotajiwa mpaka kitimoto. Lakini nilipojionea mwenyewe kwa macho yangu na kinywa changu, sikuwa na sababu tena ya kuwa na mashaka, badala yake, nilibaki na mshangao. Niligundua kuwa Mzanzibar si kama nilivyokuwa nikiifahamu, kwa kuambiwa.

Sijui ilifika fikaje hapo kwenye hiyo lodge! Sijui kama nguruwe wanafugwa huko Zanzibar au wametolewa bara.

Lakini naamini Serikali na Raia wanafahamu kuwa kuna biashara kama hiyo huko Zanzibar. Kitendo cha kuruhusu watumiaji wa hiyo mboga kujinafasi bila kubughudhiwa, hata kama ni katika baadhi ya maeneo tu, kinaonesha wazi kuwa Wazanzibar ni watu waelewa na wavumulivu pia.

Wameonesha kwa vitendo kuwa japo wao (wengi wao) hawaitumii kitimoto, wanaheshimu Imani za wengine. Ndiyo maana hawajaweka ukwazo kwa wanaohitaji hiyo mboga. Huo ni ustaarabu wa hali ya juu!!!

Hongereni sana Wazanzibar!
Mwamba Kitimoto utajua Umuhimu wake Ukiwa unatumia ARV Maana zile dawa kali na ukigonga kitimoto. Wewe acha tu .
 
Huwezi kumuepuka nguruwe kizembe.

Saud Arabia pamoja na sheria kali lakini wameshindwa kumdhibiti ndio iwe zenji?

Hata ikitokea watu wakaenda kuweka makazi Mars, mnyama wakwanza kufikiriwa kubebwa atakuwa ni nguruwe.
 
Huwezi kumuepuka nguruwe kizembe.

Saud Arabia pamoja na sheria kali lakini wameshindwa kumdhibiti ndio iwe zenji?

Hata ikitokea watu wakaenda kuweka makazi Mars, mnyama wakwanza kufikiriwa kubebwa atakuwa ni nguruwe.
Saudi Arabia? Aisee!!!
 
Hakuna sheria ya kuzuia kitimoto Zanzibar
Kitendo cha asilimia kubwa ya Wakazi wake kutokuitaka ingeweza kuwa sababu tosha ya kukosekana. Wazanzibar wengi ni Waislamu, na Muislamu na nguruwe ni kama mafuta na maji.
 
Hata kama CD4 Zimeshuka ukitumia hiyo kitu Fasta tu zinapanda. Ikiwa unatumia dawa zozote kali sana mpaka zinakuyumbisha Piga kitimoto utakuja nishukuru.
Kama ndivyo, inapaswa kupitishwa kuwa miongoni mwa lishe maalum kwa watu wenye changamoto za kiafya.
 
Uvumilivu gani wakati walaji wakubwa ni Wazanzibari wenyewe? Tena pale inapotengenezwa pana lodge ambapo wale viongozi na watu maarufu wasiopenda kuonekana wanapoagiza watengenezewa kitimoto huweka na booking ya chumba kabisa ili walie vyumbani wasionekane?
Vijana wa kipemba na wakiarabu waliojizira wale huwa ndiyo wanailia palepale nje ( bar )
Mkuu, si ajabu kwa Mzanzibar kutumia hicho kitoweo kwa sababu si Wazanzibar wote ni wafuasi wa dini ya Kiislamu. Na hao wanaopenda kuila wakiwa vyumbani, mimi nawaona ni wastaarabu. Hawataki kuwakwaza wasioitumia. Hata mimi ningefanya hivyo ikitokea nataka kutumia chakula nikipendacho lakini ni haramu kwa wengine. Si vizuri wengine kukwazika kwa sababu ya starehe zako.
 
Sidhani! Mzee Said Salim Bakressa asingekubali hata kama ingelipiwa nauli ya shilingi bilioni kumi kwa kila "mbuzi"
Acha ubishi... Mimi ni mfanyabiashara wa nyama kwenye kampuni zinazo sindika nyama. Nguruwe inapelekwa Zanzibar na hayo makampuni ila kwenye label ya mzigo inaandikwa Jina jingine la lugha ngumu 🤣🤣🤣 na hakuna kitu kinaingizwa Kwa magendo Zanzibar kama nguruwe. Kila siku kwenye ile mizigo unauona pale bandarini na nguruwe yumo pia😭😭😭​
 
Acha ubishi... Mimi ni mfanyabiashara wa nyama kwenye kampuni zinazo sindika nyama. Nguruwe inapelekwa Zanzibar na hayo makampuni ila kwenye label ya mzigo inaandikwa Jina jingine la lugha ngumu 🤣🤣🤣 na hakuna kitu kinaingizwa Kwa magendo Zanzibar kama nguruwe. Kila siku kwenye ile mizigo unauona pale bandarini na nguruwe yumo pia😭😭😭​
Watanganyika Wana akili sana!
 
Back
Top Bottom