KITIMOTO nyama tamu ambayo ni zawadi kutoka kwa MUNGU

UWE UNAJARIBU MAPISHI TOFAUTI MKUU ITASAIDIA
 
Maisha yangu yote sijawai kula hiyo kituu na sitadhubutu ni haramu ptuuuuu
 
Yani apa ni kutamanishana jamani chaa
ONA HAWA WATU WALIVOCHOKA...[emoji1]HAITOSHI BADO WANAKUNYWAGA BIA ZA SUKARIGURU
KWA NYAMAFU YENYE KUPIGWA RUNGU...[emoji1] BAHATI MBAYA SIMU ZAO HAZINA SELFIE TU VINGENEVYO HUMU TUNGETAFUTA PAKUTOKEA KWA PICHA ZAO...
HAO BADO WANAJUA HADI LEO RAIS WETU NI MWLM JULIAS KAMBARAGE NYERERE

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Lyaga mayu
 
Kitimoto....

Uipate ile rosti iliyorostiwa mpaka ikageuka kuwa brown, afu pembeni unawekewa pilipili za kukata zile... zimechanganywa zile za kijani na moja inayoelekea kwenye wekundu hiviii. Pemben tena kuna vipande viwili vya ndimu zile kubwakubwa pamoja na chumvi.

Hiyo uipate na dona au ndizi kama 3 hivi zilizokaangwa. Kabla hata hujamaliza kuikagua sahan kama kila ulichoagiza kimefika unaambiwa na mhudumu "naomba unawe".... unamuangalia kidogo usoni then unakinga mikono unanawa, maji vuguvugu saaafi kabisa.

Anamalizaa anaondoka unamsindikiza kidogo na jicho la kiwizi then unairudia sahan yako. Unapiga one touch moja unakamata kipande cha kitimoto kilicholowa rosti zito unakitupia mdomoni na kabla hujatafuna sana unang'ata na kipande cha pili pili. Then baada ya hapo unachukua kipande cha ndimu na kuanza kukamulia taratiiibu kwenye rosti yako huku ukiiangalia kwa madaha beer yako iliyopo pembeni na imefungwa tishu kwa juu.....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…