Kitu ambacho Membe hatokaa amsamehe Rais Magufuli maishani!

Kitu ambacho Membe hatokaa amsamehe Rais Magufuli maishani!

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,377
Nawasalimu wanabodi.

Mwaka 2015 Mwanadiplomasia mahiri na kachero mbobezi Bernard Membe alijaribu kuusaka Urais kupitia CCM lakini akakatwa jina lake hatua za mwisho.

Macho na masikio ya wengi yalikuwa ni kwa Edward Lowassa na Membe lakini ngekewa ikamdondokea John Magufuli ambaye sasa ni Rais.

Mwaka 2016 mwezi Machi Jumuiya ya Madola (CommonWealth) ilitoa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ambapo ilikuwa ni zamu ya Afrika Mashariki kumtoa mtu. Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki ilipendekeza mtu huyo atoke Tanzania huku wakipendekeza awe ni Membe. Utarayibu wa Jumuiya hiyo ni kwamba anayependekezwa lazima apate kibali na ruhusa ya mkuu wa nchi yake.

Kinachosikitisha, Rais Magufuli akamwekea "bambi" Membe na nafasi hiyo ikaenda nchi nyingine. Membe akakosa nafasi hiyo.

Kama angefanikiwa kwanza angeenda kuishi jijini London. Angelipwa mshahara wa $50,000 kwa mwezi. Marupurupu $23,000, angesafiri na ujumbe wa watu 25 kila safari ya kikazi. Hizo ni faida binafsi.

Faida za kinchi ni pamoja na kupaa kidiplomasia duniani tofauti na sasa ambapo diplomasia yetu inaishia Buguruni. Tanzania ingezidi kusifika kwa kutoa viongozi hodari katika ngazi ya kidunia baada ya kina Dk. Salim Ahmed Salim, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Mahiga (marehemu) nakadhalika. Unajiuliza ni kwa nini Magufuli alimkatili Bernard Membe?

Namshauri Magufuli, vichwa vya watu kama Membe si wa kuacha kuzurura nje ya utawala. Ni watu wa kuwa nao karibu. Mchukue Membe awe mshauri wako wa masuala ya diplomasia na usalama.

Nawasilisha!
 
..faida nyingine ingekuwa ni Watanzania kupata nafasi za kazi ktk sekretariet ya Jumuiya ya Madola.

..kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola angetoka Tz basi lazima baadhi ya key position ktk Ofisi yake zingejazwa ni Watanzania.
 
Hayo yote ni maccm na roho mbaya ndio sifa yao kuu jiwe kayaharibu maisha ya watanzania wengi sana zaidi ya huyo membe wako

Huyo Membe akubali tu sasa akalime korosho na kuendesha hotel yake. Mambo ya siasa yamekwisha mpita mkono wa kushoto hivyo akubali tu yaishe kwani hakuna jinsi Jiwe atakuja kumfikiria kwa nafasi yeyote!!
 
Sure mkuu
..faida nyingine ingekuwa ni Watanzania kupata nafasi za kazi ktk sekretariet ya Jumuiya ya Madola.

..kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola angetoka Tz basi lazima baadhi ya key position ktk Ofisi yake zingejazwa ni Watanzania.
 
Rubish content ever posted in the Forum.. you better stop dreaming like a frog..here n there..
Kazi kweli kweli, Umeandika lugha gani mkuu usiofuata kanuni za uandishi

English ina miundo na mifumo

"Rubbish content ever posted" unaelewa ulichoandika

"Content" means you have understood concept and details of the writer

"Rubbish" means negation of what you have understood

"Rubbish Content" Hakuna kiingereza kama hicho cha kukubali na kuikataa sentensi labda kama unatafsiri kichaga kwenda kiswahili halafu kwenda kiingereza

Haya ndio madhara ya kutafsiri kiswahili na kuandika kwa kiingereza

Hakika wapumbavu hawataisha nchi hii

Madhara ya shule za kata na vyuo vya kata haya ndio mavuno yake

Utaweza wewe kuongea kiingereza kwa dakika tano kwa uandishi wa hovyo namna hiyo

English ni somo pana sana ukitaka ujifunze nenda kwa watu wanaoongea lugha hiyo tu mwezi mzima bila kuchanganya utajifunza kitu

Achana na walimu wako wa kata hao nao ni vilaza kama wewe
 
Ras Simba anapiga hela sana.
 
Mtu yeyote anayesema ati Magufuli amekua rais kwa ngekewa, kwamba mchuano ulikua kwa lowasa na membe ndio wajumbe wakaamua kumpa Magufuli kwa hasira..
huyo mtu hazijui kabisa siasa za bongo na hajui hata anachokisema.

Magufuli hajawa rais kwa bahati mbaya wala kwa ngekewa
 
Katika hao watu 25 aliotakiwa kusafiri nao wewe ungekuwepo au? Sikia katika vita vya kisiasa kama ahusiki waachie wenyewe wanaocheza huo mchezo wacheze. Usikute Membe ana mabaya aliyomtendea Magufuli na ndiyo maana Magufuli anamuacha tu akihaha na kupotea kisiasa kama ilivyo sasa.
 
Mwanzo mlisema membe anaenda kumuondoa magu na kuwa raisi
Leo mnasema magu amtafutie nafasi membe serikalini.
Nyambaaaf zenu
Wabongo hawaeleweki kabisa, subiri kesho sasa....atakuja kinyago mwingine na habari za kitoto kabisa. Nakumbuka mwaka jana wakati Membe anahaha kutafuta chama cha kugombea urais, akawa anabandikwa mtandaoni na kauli mbiu yake kuwa...."Baada ya kazi, bata." Wabongo wakachanganikiwa na kuanza kueneza ile kauli, sasa kimyaaaaaa! Anyways, katika siasa simuamini mtu yeyote kwani asubuhi wanagombana usiku wanacheka wote na kupanga namna ya kuachezea akili wabongo.
 
Duh, kama ni kweli hii nyundo ilitua vibaya utosini, natamani kujua sababu hasa ya kumfinyanga mwenzake kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom