let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 3,699
- 8,857
Hata Nachingwea kilionekana muda huohuo.Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.
Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.
Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.
Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.
Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.
Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.
Ulikua unaota uko na majirani zako wawili mnaona kitu kinapitaKama ni kuota basi ilikuwa ni ndoto ya pamoja na jirani zangu wawili.
Je kabla ya kutoka nje ya nyumba yako uenye ukuta ulitoka kuangalia katuni za HenryDanger au Stars pace?Picha zikuweza kuchukua kutokana kasi ya mwendo wake. Ila suala la location mimi naishi Mbezi Beach.
Tatizo huwezi kuelewa, sikuwa peke yangu, bali nilikuwa na jirani zangu wawili ambao wote kwa pamoja tulishuhudia tukio hilo.Hivi hata kama ndio wewe unasimuliwa tukio kama hili kwa mazingira tofauti, utajihakikishiaje kwamba hiyo habari niya kweli?
Tatizo sio wewe kusimulia kuonesha ulikua peke yako kwenye hilo tukioTatizo huwezi kuelewa, sikuwa peke yangu, bali nilikuwa na jirani zangu wawili ambao wote kwa pamoja tulishuhudia tukio hilo.
Hata mimi nakubaliana na uwezekano wa kuwa ni "drone" kutokana na sauti yake, lakini kumbuka hatukusikia upepo wote upulizao kutokana na uwepo wake angani.Mkuu itakua ni drone, UFO huwa hazina sauti kwa mujibu wa maelezo ya waliozishuhudia..
View attachment 2018708
View attachment 2018709
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aliens walikutembelea walitaka wakupe maujuzi ...wakaona mnashanga shangaa wakasepa
View attachment 2018729
Mkuu, isiwe shida. Ni mimi ambaye ndiye nimeshuhudia. Lakini pia sikuwa peke yangu. Kwa mtu yeyote anayejali anaweza kufanya kile ambacho mimi nimekifanya, kwa kuwa naamini kupashana habari kunafumbua akili kwa mtu aliye mdadisi.Tatizo sio wewe kusimulia kuonesha ulikua peke yako kwenye hilo tukio
Nachomaanisha ni kwamba leo hii mtu aje asimulie humu kwamba yeye na rafiki zake wameona kobe akikimbia kwa speed ya mwanga, utahitaji kitu gani kwenye ku support hayo maelezo ili uamini hiyo stori ni yakweli?
Je maelezo ya kusema alikua na rafiki yake, kwako yangetosha kukubaliana naye?
Hayo mambo yapo sana kwa mtu anayetumia muda kidogo kuangalia anga ataona maajabu mengi. Pia kuna mavyombo yasiyojulikana yanasafiri angani, wakati mwingine na vitu vya kiroho ambavyo havikusitirika kikamilifu mbele ya wanadamu.Natambua umuhimu wa kuchukua picha, lakini mazingira niliyokuwepo ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo.
Nadhani maana yangu hujaielewaMkuu, isiwe shida. Ni mimi ambaye ndiye nimeshuhudia. Lakini pia sikuwa peke yangu. Kwa mtu yeyote anayejali anaweza kufanya kile ambacho mimi nimekifanya, kwa kuwa naamini kupashana habari kunafumbua akili kwa mtu aliye mdadisi.
Ebu tuchukulie ningeamua kuuchuna, sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu angalijua nini ambacho kilitokea. Lakini pia tujiongeze na tuchukulie pengine jambo hilo lina tishio la kiusalama, huoni kuwa kwa kulisema linaweza kutoa "elerts" fulani.
Weya izi pikiture?Sijui ni mimi pekee yangu na jirani zangu wawili ambao ndiyo tulikishudia chombo hicho, ama ilitokea pia kwa watu wengine. Ilikuwa jana yapata saa moja jioni, giza ndiyo kwanza limeingia, ile tu natoka nje ya geti la uzio wa nyumba yangu kwenda club kuangalia pambano la soka kati ya Liverpool na Arsenal, nikaanza kusikia sauti ya mvumo kama ule wa sauti za nyuki wengi wawapo angani.
Ilikuwa ni sauti ambayo haiko endelevu, bali inasikika kwa muda na hatimaye inakatika na kubakia kimya kwa kitambo. Nilitembea kama hatua kumi na tano, hivi nikawakuta jirani zangu wawili.
Baada ya kusalimiana walinionyesha kushangazwa na kitu hicho cha ajabu kilichokuwa kikitoa mlio wa ajabu. Licha ya sauti yake pia kilikuwa kikitoa mianga ya taa nyingi za rangi ya bluu.
Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake.
Je! Kuna mtu mwingine pia alilishuhudia jambo hili siku ya jana? Ingalikuwa ni mimi pekee yangu ndiye ambaye nilishuhudia jambo hili ningelipotezea, na hata ningevuta subiri ili atokee shuhuda mwingine ambaye angesimulia.
Sasa mashuhuda tulikuwa ni watatu, tena wote watu waxima. Je! Kuna mtu mwingine aliweza kulishuhudia hapa jukwaani.
Muulizeni Bujibuji na mauchawi ya mbezi beach.mbezi beach kuna mauchawi mengi sana usione majumba mazuri ukajua tu yamepatikana bure bure.
its a process