Kitu cha ajabu chaonekana kikiwa angani jana jioni

Kwa sekunde kadhaa kilikuwa angani kikielekea uelekeo wa mawio ya jua. Lakini tofauti na ndege nyingine ziwapo angani, ambapo husafiri kwa upande mrefu kuwa ndio muelekeo wa chombo, chenyewe kilioneka kama vile kinasafiri kwa ulekeo wa mapana yake
Sijapaelewa hapo
 
Nashauri tuzidi kusubiri kwa mashuhuda wengine pia. Pengine ikawa ni mojawapi ya zana za kisasa za kivita zq makamanda wa JWTZ kutoka Lugalo Barracks. Kwa maana hawapo mbali kutoka hapa.
Kina shape gani??na kina rangi gani?
 

Utakuwa uliona kitu kinafanana na hii drone. Huenda ulikuwa ukichukuliwa picha bila wewe kujua.
 
Wee unamatatizo [emoji1787][emoji23]
kuna jani flani hivi la kipuuzi likichomwa na moshi wake ukiuvuta lina uwezo wa kumkuza mbu hadi kuwa na ukubwa sawa na size ya bombadia!je hapo mlipokuwa watatu kuna moshi wowote ulikuwa unafuka ndugu mtoa ujumbe?
 
Isijekuwa uliona mwanga wa taa za Disco.
 
Mkuu nami pia nakubaliana na wewe. Lakini andiko langu halikujielekeza kwenye ushawishi ili watu wakubaliane nalo. Bali lilikuwa na ujumbe wa kile ambacho nimekishudia kwa macho yangu mwenyewe.

Suala ni muhimu ni kwamba kama ninasema na kushuhudia uwongo basi uwongo huu uwe juu yangu na Mola wangu. Lakini pia kama ninasema ukweli juu ya hili, basi Mola wangu mwenye haki anashuhudia pamoja nami.
 
Sawa
 
Sijapaelewa hapo
Ndege ya kawaida huwa ni nyembamba kwa upana lakini ni ndefu kwa urefu. Lakini hicho ninachokisema mimi ni tofauti nilipokiona kikiwa angani.

Nilikiona kikiwa kinatembea angani kikiwa na muonekano wa upana wake lakini ni kifupi kwa urefu wake.

Mfano labla tuseme rula jinsi ilivyo. Ndege za kawaida hutembea angani kwa kuzingatia urefu wake, lakini hiki ninachokisema ni kama kilikuwa kinatembea kwa upana wake.
 
Unamaanisha kama ni ndege inakwenda upande yaliko madirisha ya abiria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…