Pre GE2025 Kitu gani cha Ajabu wanachofanya CCM Madarakani ambacho vyama Vingine haviwezi kufanya?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
 
Kuna Siri kubwa wengi hamuwajui, CCM kupitia kampuni yake tanzu ya Jitegemee holdings co, limited namiliki migodi mikubwa hasa ya mnakaa ya mawe ambayo imejigawia, na sidhani hata kama bill za umeme wanalipia na watu OSHA na Nemc hawathubutu kukanyaga kwenye migodi hiyo.

Hivi ndio Vitu ambavyo wengi hamvijui hata wanaccm wengi hawajui ndio vinafanya CCM iko tayari kuingiza nchi vitamin kuliko kuachia madaraka Kwa hiyari Wana makandokando ambayo wengi hamuwajui na hata CAG hajui.
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
CCM ni Mbuyu unaopaswa kukatwa maana umejaa mashetani mengi sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Siku raia wengi wakijitambua na kuacha uoga, watagundua hakuna watakacho kosa CCM wakiondoka. CCM inalindwa na maslahi binafsi ya watu fulani.

Raia wametishwa wakatishika kuona kana kwamba kuitoa CCM ni hatari kwa nchi, kuwa nchi itaingia kwenye matatizo.. full propaganda. Na ujinga huu ndio faida kwa CCM.
 
Ndiyo maana Kenya inatupita kimaendeleo.Kama udhahidi upo iwe ajenda kwenye campaign.
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Vyama vingine Bado vinagombea madaraka hivyo haviwezi kuleta mshikamano wa Taifa.

Ni Vyama watu na sio taasisi
 
Kuzalisha "Chawa wengi" Aisee Kuna machwa mtaani kibao....ni hatari Sana natudia
Kuna machwa wengi sana mtaani...namaanisha Chawa.
Chawa anakaa sehemu yenye uchafu. Mtu akiwa na chawa maana yake sio mtu safi.
 
Ina maana JPM alivumilia haya ?
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Ufisadi
 
wana Taasisi ingawa uimara wake kwa sasa ni wa mashaka kwani unaonekana kuporomoka kwa kasi
wana mikakati mahiri ya kuwafanya waendelee kuwepo walipo
wana umoja kwenye uchaguzi
wanakubalika na mifumo muhimu
wananufaika greatly. Kikundi chochote kiwe cha kisiasa au laa kikishika dola huwa kinanufaika katika njama mtambuka na huwa hakipo tayari kuachia fursa husika.
 
CCM wanachofanya ni kuwatisha wananchi na wananchi wakitishika ndio inakuwa Mtaji wa wao kubaki madarakani. Kiufupi CCM ni waoga wa kuachia madaraka. Ukomovu wa kisiasa ni pamoja na kukubali matokeo yawaye yote kitu ambacho CCM hawana 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…