Pre GE2025 Kitu gani cha Ajabu wanachofanya CCM Madarakani ambacho vyama Vingine haviwezi kufanya?

Pre GE2025 Kitu gani cha Ajabu wanachofanya CCM Madarakani ambacho vyama Vingine haviwezi kufanya?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna Siri kubwa wengi hamuwajui, CCM kupitia kampuni yake tanzu ya Jitegemee holdings co, limited namiliki migodi mikubwa hasa ya mnakaa ya mawe ambayo imejigawia, na sidhani hata kama bill za umeme wanalipia na watu OSHA na Nemc hawathubutu kukanyaga kwenye migodi hiyo.

Hivi ndio Vitu ambavyo wengi hamvijui hata wanaccm wengi hawajui ndio vinafanya CCM iko tayari kuingiza nchi vitamin kuliko kuachia madaraka Kwa hiyari Wana makandokando ambayo wengi hamuwajui na hata CAG hajui.
Somehow, I concur with you.
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Ccm hawa cha Ajabu tena Vyama vya Upinzani vinaweza kuja na Mapya ambacho CCM hata wakuyajua Mbinu za kuyafanya Hawana

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Nini kilikusukuma kuingia CCM utawala wa Magufuli?
Kwanza haikuingia CCM utawala wa Magufuli, nimeIngia CCM mwaka 1988 nikiwa JKT.

Sababu za kugombea ni kusukumwa tuu na uzalendo kulisaidia taifa letu, serikali yetu ilikuwa inafanya baadhi ya mambo ndivyo sivyo, mwenye jukumu la kuisimamia serikali ni Bunge, nikaandika makala hizi mbili kuhusu Bunge letu Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?

Na Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?

Na ilipotokea issue ya CAG Prof Asad Asad Bunge letu likapitisha Azimio Batili kuwa halitapokea ripoti ya CAG Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG?

Nikawafungua macho Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba

Ndipo Bunge na wabunge wetu, wakalifutika uvunguni lile Azimio lao batili kimya kimya, wakaipokea ripoti ya CAG.

Hivyo nikaguswa kugombea ili nikasaidie, nikaweka wazi agenda zangu
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared
P
 
Tuambie unadhani kwanini wajumbe wa Kawe walikutosa ?...na pia unadhani kwanini wenye Ccm yao walikutosa tena na kumpa kijiti Gwajima apeperushe bendera ya chama japo naye alitoswa na wajumbe kama wewe ?

Karibu...
 
Mosi kuna familia zimenufaika kuanzia kwa baba hadi wajukuu wanaendelea kutengenezewa mirija sababu ya CCM.

Pili watu wamejipatia utajiri chini ya mgongo wa CCM hivyo siku CCM ikitupiliwa mbali utajiri huo bandia utaishia hapo hapo.

Wafanyabiashara wakubwa ndio wakwepa kodi wakubwa hawa ndio huisaidia CCM katika damu na jasho , giza na mwanga ibaki madarakani iwe kwa fedha na mawazo.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanazo kadi za CCM ulaji na mafao yao hutegemea CCM hawako tayari utawala mwingine uje kwani unaweza kuja na mipango tofuauti na hizi dezo wanazopata chini ya CCM.

Siku hivyo vitatu vikithibitiwa CCM kwisha habari yao.
 
Kuna Siri kubwa wengi hamuwajui, CCM kupitia kampuni yake tanzu ya Jitegemee holdings co, limited namiliki migodi mikubwa hasa ya mnakaa ya mawe ambayo imejigawia, na sidhani hata kama bill za umeme wanalipia na watu OSHA na Nemc hawathubutu kukanyaga kwenye migodi hiyo.

Hivi ndio Vitu ambavyo wengi hamvijui hata wanaccm wengi hawajui ndio vinafanya CCM iko tayari kuingiza nchi vitamin kuliko kuachia madaraka Kwa hiyari Wana makandokando ambayo wengi hamuwajui na hata CAG hajui.
Wengine hawajui ila wewe unajua! Ahahahahaha!!!
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Siku wakifanyia KAZI haya mawazo ya CAG Ccm laana utaacha kuwatafuna watabaki na misukosuko tu
 
Mkuu Allen Kilewella, mimi ni miongoni mwa wana JF wachache humu wenye uwezo wa kitu kinachoitwa graphology, huu ni uwezo wa kubaini the motives behind andiko lolote, hivyo nimehisi bandiko hili linanihusu kwasababu mimi ni miongoni mwa wanaosimama na CCM itatawala milele kwasababu hakuna replacement.

Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, no, siasa ni Sayansi, social science, political science, inafuata kanuni za scientific theory ya the Newton's first law of motion ya "The body in motion" ili kitu ki move from hapo kilipo lazima kwanza kutokea forces nyingine, ikimovuzishe, na kikiwa kwenye mwendo, lazima itokee forces nyingine ikisimamishe.

CCM ndio our body as a still body iliyo stands kwenye Ikulu yetu, ili CCM iweze kuondoka Ikulu yetu, lazima iondoshwe!, kwa katiba yetu hii, na sheria zetu hizi, na tume yetu ya uchaguzi hii, kwa vyama vyetu hivi vilivyopo, hakuna chama chenye uwezo huo wa kuiondoa CCM kwenye Ikulu yetu, hivyo kusipotokea mabadiliko, CCM Itaendelea kutawala milele!. This is a fact.

Na kwenye Political dynamics za siasa zetu, CCM ndio iliyopo kwenye motion ya kuiendesha nchi yetu, CCM ndio the body in motion, kitaendelea kuitawala Tanzania mpaka kitokee chama kingine chenye uwezo zaidi to stop CCM!. Vyama vilivyopo hata vikiungana vyote, vikasimamisha mgombea mmoja, bado they can't beat CCM kwenye urais ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mitaa, vitaambulia ambulia.

Kinachofanya CCM iendelee kuwepo ni kukosekana kwa replacement, nothing can exist in hollow, there must be a replacement kwanza ndipo CCM iwe replaced.

Wengi tunakutana tuu humu lakini hatujuani vizuri, sisi wenzenu wengine ni ma Political Consultants, nimefanya projections zangu kuhusu lini CCM inaweza kuanza kuondoka, Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!

Ule uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni fursa muhimu na adimu kwa upinzani kuingia Ikulu, mimi as a political consultant, nikajitole kuwasaidia bure CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Nikawaeleza jinsi njia ilivyo nyeupe Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni!

Nikawashauri to be focused Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
Wangefuata ushauri huo, saa hizi Chadema wangekuwa Ikulu toka ile 2015!.

P
Si useme Tu kuwa uchaguzi wa 2015 CCM waliiba kura... unaogopa nini mkuu?

Any way umesema kweli.
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Wewe umesomeshwa na chama gani

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
kitendo cha kuwasombelea wanachama wake sehemu mbalimbali ili waende kwenye mkutano wao halafu wanatangaza kwamba wanapoendwa!!!!!!!
 
Kula Hela za umma waziwazi Hadi Sasa wameamua kuwalipa Hadi watoto wao wadogo wakiwanadi Kwa jina la "ccm chipukizi"
 
Kila siku tunaambiwa ikitoka CCM Madarakani hakuna chama kingine cha siasa chenye uwezo wa kuchukua nafasi yake.

Hivi CCM inafanya kitu gani chanya kwa Tanzania ambacho vyama vingine vya Siasa havitaweza kufanya CCM ikitolewa madarakani?
Labda nikupe oroza ya matukio halafu uamue kama NCCR wangeweza.
1. Taifa moja, kwingine kote ni mkusanyiko (motley collection of tribes) wa makabila.
2. Luga moja, Kiswahili, hakuna kwingine hata Ujerumani kuna Huegnots. Japan kuna Shanshu na South Africa wana jamii ya Wasandawi na UK wana Wawelsh. India wana Watelugu.
3. Uhuru 1961 Nyerere. Futa utumwa 1964 Karume
4. Azimio la Arusha 1967
5. CCM 1977
6. Vita vya Kagera 1978
7. Kung'atuka 1985 Mwinyi
8. Multiparty 1992 ingawa watu walikataa 80%
9. Amani na utulivu 1995 Mkapa
10. Ditto 2005 Kikwete
11. Ditto 2015 Magufuli
12. Ditto 2021 Samia

Sasa nipe ya CUF. Nipe ya NCCR. Hawa ndiyo wakongwe, CHADEMA ilianzia CCM Mtei akaja CCM Lowassa. Hapa tumekwepa Muungano kuvunjika, Waarabu kurudi Zanzibar, Udini wa CUF, kabila wa CHADEMA hadi leo Ilani yao ina serkali za Makabila na ushoga na uraipacha. Niendelee?

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom