Kitu gani kilisababisha usijiunge na UDSM?

Chuo Kikuu cha Taifa

Almost 90 ya Viongozi wote tangu kupata Uhuru wametokea hapo
Sasa wangesomea wapi na chuo kilikuwa ni hicho tu mkuu. Ni sawa na kusema muhimbili imefanya pasuaji za kibingwa nyingi kuliko hospitali yoyote wakati pengine yenyewe ilikuwa ikitegemewa kwa jukumu hilo..

Sijawahi kuelewa utukufu wa UDSM unatoka wapi unless mtu awe ni mwanamkoa mwenzetu ambaye ndoto ya kufika mjini dar isingefanikiwa bila kupitia UDSM
 
True &fact
 
Kuna nyumbu mmoja mimi nilienda udom yeye udsm akanicheka nipo chuo cha kata , now yupo huko karatu anapanda
ma cruza kwenda job na anakunywa vumbi la kutosha😁😁😁
UDSM sikuijaza popote na wala sikuwahi kuwa na wazo la "lazma nisome chuo flani". Niliangalia course na mkoa wa chuo kilipo na chaguo langu la kwanza ndilo nilililolipata
 
Nami nilifika DSM kwa mara ya kwanza kupitia Chuo miaka ile πŸ€—

Wakati wa Likizo, nawapa stori za Mjini jamaa zangu wakiwa wamenizunguka kule Kijijini kwetu πŸ˜…πŸ™Œ

Hata hivyo Kwa sisi tuliosoma Engineering, bado Chuo kikuu cha DSM kina workshop nzuri zenye vifaa kuliko vyuo vikuu vingine kule Mikoani.

Bila kusahau Walimu wazuri wabobevu jamii ya Profesa Alex Mrema ama Profesa Ninatubu Lema
 

Engineering field sina encounter nao sana Ila kuna products za DIT nilikutana nazo sehemu flani πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ..

Very professional, practical na wanapambana sana.

Kuhusu DSM, mimi nilifika mapema na sikupapenda kabisa mwanzoni. Life la hekaheka, joto etc

Japo nikirudi mkoa haswa shuleni, baadhi ya watu wanakuona kama umetoka New York. Rangi flani inakubali lakini sikuwahi kubrag 😁😁😁
 
DIT ilitoa maTechnician wazuri sana wa Telecom/Computer/Mechanical

Wakati wenzao wa Arusha Tech, walisifika Kwa kutoa wataalamu wengi wazuri wa barabara na majengo

Kwa level ya Shahada za Uhandisi, DSM imefanya vizuri sana

Kusoma DSM ilikuwa ni fahari sana, hata kama Kuna mchumba ulikuwa unammendea Kijijini akijua ulikuwa unasoma DSM lazima akukubali πŸ€—

Kama ulivyosema, hata rangi ya ngozi ukitoka DSM inakuwa inang'aa hivi

Kwahiyo Kijijini inakuwa full ujiko πŸ˜…
 
Mada za kulinganisha vyuo mara nyingi huzungumzwa na wanafunzi wa chuo

Malizeni chuo, njooni mtaani muone kama ajira portal inatofautisha UDSM/UDOM/SUA/mzumbe

Acheni ujinga, kwenye interview unakuta anafaulu mtu wa MUM/TEOFILO KISANJI/SAUT halafu wewe na UDSM yako not selected
 
Wasiwasi wangu huko kijijini kukuonea kijicho na kuku waisha yaani kuku R.I.P kabla ya WAKATI kufika.πŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…