Story ya miss corridor ndo naisikis leo mtu mwingine anaisimulia. Back in o level days nilikutana na tukio kama hilo, kulikuwa na sauti very specific ya mtu anatembea na high heels kuja uelekeo ya chumba nilichokuwa, nimekomaa zangu kusoma wakati tunaenddela na mitihani ya taifa, alipokaribia usawa wa chumba changu hofu ilishanishika nikakimbilia kitandani, vuta shuka na kuziba masikio na kufumba macho, nilikuwa nasikilizia mapigo ya moyo wangu yakienda mbio, na usingizi ukanishika moja kwa moja shortly, sikuwahi kuielewa hiyo hali mpaka leo, na sikumsimulia mtu, nashangaa kumbe kuna hadi term wanaita miss corridor, ila shetani , asante Yesu kwa ulinzi. That was very real, ilianza ghafla kwa mtu kufungua na kufunga mlango wa nje (ulikuwa unafungwa always, na giza likiingia wadada wa bweni wanabana kwa kufuli yaani tunafungiwa ndani) na movement ikawa specific inakuja straight nilipokuwa, akifuata corridor la bweni chumba chetu kilikuwa mwisho kabisa, partition za vyumba hazikuwa na milango so ningekomaa ningeona kwa macho who or what was walking namna ile, sidhani kama ningebaki timamu I swear. Na ilishakuwa usiku wa manane yapata saa nane au tisa unajua ile mnasoma unamwambia rafiki yako akuamshe anapolala nawe unaamka unaendelea na kitabu. Kilichonivuta attention ni kwanza ile high heels, hakuna mtu anaamka usiku avae high heels, hivyo viatu vilikuwa haviachwi kwenye corridor, ila kulikuwa na ndala nyingi sana unaweza kuvaa za yeyote mnayeshare chumba, na pili hakukuwa na sababu ya mtu kuja chumba chetu maana sisi form 4 tulishare room moja, na madogo wote walikuwa wanalala mapema kabisa, vyoo vililikuwa nje na watu walitoka kwa kusindikizana wanaoshare chumba that time hakuna mtu alikuwa ametoka , na tatu, muda uliotumika kufunga na kufungua mlango ulikuwa just a matter of seconds mind you tayari ile milango imefungwa kufuli ile milango mipana ya vipande viwili, mauza uza yalikuwa mengi sana, it was far from normal.