passion_Amo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2023
- 378
- 542
Kwanza kuwa tu na pesa sio kufanikiwa kwa sababu pesa unaweza ukarithi au ukapewa tu nawe ukawa na pesa, mafanikio ni matokeo na hupatikana kutoka kwenye ulichokifanya.
Sasa wewe unachokuzungumzia ni kumiliki pesa kichawi bila kufanya kazi wakati wenzako wanazungumzia mtu kufanikiwa kwenye shughuli zake kwa msaada wa uchawi. Sasa wewe unapinga huo uchawi na kusema kazi tu pekee ndio huleta mafanikio ila umeshindwa kujibu kwanini wengine hawafanikiwi kwenye kazi zao pamoja na kufanya kazi kwa kanuni na juhudi kama wengine wanaofanikiwa?
Ndio maana nikasema kwamba kufanikiwa ni zaidi ya kufanya kazi kwa kanuni na juhudi, kusema hivyo sina maana ya kwamba kila aliyefanikiwa alifanya uchawi ila lazima tukubaliane kwamba kufanikiwa ni zaidi ya kufanya kazi kwa kanuni na juhudi tu.
Kwahiyo wapo watu wamefanikuwa kwa juhudi tu zao na wapo wamefeli pamoja na juhudi zao. Ndio maana kuna wasanii hawafanikiwi pamoja na kufanya vizuri zaidi ya hao wengine ambao wamefanikiwa na hapo ndipo hutumika misemo kuwa "yule hana bahati na yule nyota yake inang'aa" ni kwa sababu kama hizo kwamba mtu anafanya kazi vizuri na juhudi ila hapati mafanikio.
Embu tazama hawa ni majirani wote ni watu wa arusha ni askari POLISi wote hawana cheo.
Wanapokea mshahara Sawa. Lakini huyu mmoja mbali na ufinyu wa muda, ana vibanda vya huduma za kifedha, ana pikipiki 2 zinazomletea hesabu ana kiwanja sehemu moja ipo chanika inaitwa zingiziwa na huwa anakopesha wenzake kwa riba. Huyo rafiki yake yeye ni pombe na pikipiki anayo lakini anasema hawezi kwenda kazini bila pikipiki Wana mwaka wa3 tangu waajiriwe.
Utofauti ni commitment yaani mmoja yupo radhi kuumia kwa muda mrefu kupata matunda endelevu lakini huyu mwingine hayupo tayari.
swali tutajuaje hao unaosema Wana juhudi na kweli wanaweza kuwa na juhudi kazini lakini wakakosa nidhamu, na commitment kwenye mishahara au pesa wanazozipata? Kwanini useme ni uchawi na tusikirie huenda kuna sababu ambazo ni logical?